UPDATES: Madhara ya mvua iliyonyesha jijini Dar - Desemba 17, 2019

Wewe jamaa umeandika kwa hasira sana.

Wakati hapo jibu ni moja tu.

Huyo uliyemsifia ndio anaratibu kila kitu, ndio mwenye kubea lawama zote na ndio mwenye maamuzi ya kila kitu.

Kwa hio inawezekana dish lako lime shake.
Relax punguza munkari usiwe kama musiba usipayuke payuke.

Serikali na wanasiasa ndio wana maamuzi kwenye kila jambo.

Na ndio wasimamizi wakuu ndio maana unawaona na makamera na misifa yote wakiwananga makandandari mpaka wanazimia
 
Mafuriko hata California yapo

Wapinzani acheni kuokoteza matukio
Kwa hiyo mafuriko yakiwepo huko California ndiyo na hapa Dar es Salaam kwetu lazima yawepo? Nyie mkiambiwa mnamuabudu Mzungu aka Beberu mnaruka kimanga wakati matendo na maneno yenu yanaonesha Beberu ni mungu wenu.
 
sajo, Umetoa mchango mzuri sana wa hoja. Nimependa mchango wako na nakushukuru sana. Ningefurahi zaidi endapo wahusika wangeweza kuzingatia haya uliyo yasema bayana na kuufanyia kazi ushauri wako. Nafikiri tungepiga hatua kubwa sana towards self confince kama nchi.

Mungu akubariki sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umetoa povu kweli kweli.Lakini je,unajua kwamba mradi wowote unahitaji fedha na kusimamiwa vizuri katika utekelezaji na haya hayakuwepo katika awamu zilizopita?Na je,unajua kwamba ni awamu hii tu kumekuwa na nia ya kweli ya kuwasaidia Watanzania katika matatizo yao,ikiwa ni pamoja na eneo la miundo mbinu ya maji safi na taka?Unajua pia kwamba tenda za miradi katika awamu zilizopita zilikuwa zinatolewa kwa upendeleo na hata kampuni isiyokuwa na weledi ilikuwa inapata tenda,na hili liliathiri sana ubora wa miradi?Naomba utafakari kwanza kabla hujawanyooshea mainjinia vidole,huwezi kujipeleka mahali ambapo hutakiwi.Kwa awamu hii,civil engineers wanapata kazi na naweza kusema wanafanya kazi nzuri.Nategemea kwamba civil engineers wetu wataendelea kupewa kazi ili wapate uzoefu,walitengwa sana.
 
Ukweli mtupu mambo mengine ukiangalia hizo clips unajiuliza hivi afisa wa mipango miji, jamaa wa mazingira na wataalamu wengine hiyo mishahara wanapewa kwa shughuli gani.

Geography ya darasa la nne tunafundishwa mambo ya soil/river erosion na moja sababu kubwa ni maji.

Sasa wewe kweli unamwacha raia ajenge pembeni ya mto ambao unapita mjini auna buttress wall for soil protection, hakuna buffer zone for safety measure ili mali na uhai wa watu vilindwe just in case mto ukizidiwa na volumes maji wakati wa mvua kubwa; halafu tutegemee nini?

Atukatai kuna wakati mvua zinazidi njia za maji hila vitu vingine pamoja na kwamba vinasikitisha ila ukiona mazingira yenyewe ya watu walipojenga ukweli ni kwamba zilikuwa ni ajali tayari zinazosubiri muda wake tu zitokee; na viongozi wapo.
 
Jamaa naona unamtetea Mhe Jiwe. .. kwa utetezi wako huo wa kujipendekeza , huu Uzi hautokuwa na maana endapo tukafanya nadharia kuwa kwa Sasa Rais awe JK halafu waziri ni Magu..!

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1][emoji1][emoji1] Nimekupata mkuu. Si unamaanisha Mh. Jiwe alipo kuwa na wadhifa wa uwaziri wa ujenzi? Au nimekuelewa vibaya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endeleeni kusifu kwa Mapambio Tupo kwenye Laiti traki.
 
Kujenga ajenge mchina ,lawama apewe mkandarasi mbongo, this is not fair.
 
Kwa hiyo mafuriko yakiwepo huko California ndiyo na hapa Dar es Salaam kwetu lazima yawepo? Nyie mkiambiwa mnamuabudu Mzungu aka Beberu mnaruka kimanga wakati matendo na maneno yenu yanaonesha Beberu ni mungu wenu.
Hahaa ukitaka kujua jiwe na wafuasi wake wanaabudu wazungu ni pale balozi wa nchi ya kizungu akiongea Kiswahili, jiwe anachanganyikiwa na kuanza kumsifia hadi basi
Lakini balozi wa Zambia au Zimbabwe akiongea hata hamsifii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kwenye Luninha tuu, pamoja na kushusha bendera za Chadema maana ndizo zimeleta mafuriko
 
Asante sana! Hicho ndicho nilicho kuwa nasubiri kukisikia. Nilikuwa najiuliza haya yana tokea tatizo liko wapi?

Sitaki kuamini kuwa nyie maengineer na mnashindwa kutekeleza wajibu wenu kwa ufanisi, tatizo kumabe ni mgogoro kati yenu na wana siasa katika malipo.

Natumia kuwa vyombo vinavyo husika na uratibu wa maswala ya malipo linaweza zingatia malalamiko yako wakaangalia uwezekano wa kuikabili hii itilafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sababu ndo hiyo,Aliyekubali kupitisha ramani ya kujenga barabara pale Jangwani alitakiwa anyongwe tu!!! Narudia kwa sauti ANYONGWE!!! hivi wakati jeshi wanakuja kuwaokoa raia mwaka 2014 kama sikosei hakuona madhara ya kuipitisha chinichini vile.China imeendelea kwa sababu haikopeshi wapuuzi wa dizaini hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…