UPDATES: Madhara ya mvua iliyonyesha jijini Dar - Desemba 17, 2019

UPDATES: Madhara ya mvua iliyonyesha jijini Dar - Desemba 17, 2019

Wewe jamaa umeandika kwa hasira sana.

Wakati hapo jibu ni moja tu.

Huyo uliyemsifia ndio anaratibu kila kitu, ndio mwenye kubea lawama zote na ndio mwenye maamuzi ya kila kitu.

Kwa hio inawezekana dish lako lime shake.
Relax punguza munkari usiwe kama musiba usipayuke payuke.

Serikali na wanasiasa ndio wana maamuzi kwenye kila jambo.

Na ndio wasimamizi wakuu ndio maana unawaona na makamera na misifa yote wakiwananga makandandari mpaka wanazimia
 
Mafuriko hata California yapo

Wapinzani acheni kuokoteza matukio
Kwa hiyo mafuriko yakiwepo huko California ndiyo na hapa Dar es Salaam kwetu lazima yawepo? Nyie mkiambiwa mnamuabudu Mzungu aka Beberu mnaruka kimanga wakati matendo na maneno yenu yanaonesha Beberu ni mungu wenu.
 
sajo, Umetoa mchango mzuri sana wa hoja. Nimependa mchango wako na nakushukuru sana. Ningefurahi zaidi endapo wahusika wangeweza kuzingatia haya uliyo yasema bayana na kuufanyia kazi ushauri wako. Nafikiri tungepiga hatua kubwa sana towards self confince kama nchi.

Mungu akubariki sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Rais wetu Dr. John Joseph Magufuli kwa jitihada nyingi anazo zifanya katika kuipeleka nchi yetu kwenye nchi ya uchumi wa kati. Hata hivyo sina budi kutoa masikitika yangu kwa watendaji wake anao waamini kuto kuwa na uwezo wa kukabilina na janga la mafuriko ya kila mwaka.

By the way by definition:
Civil engineering is an engineering science that deals with the conception, planning, design, construction, calculation, manufacture and operation of buildings in civil engineering, transport and hydraulic engineering.

Sasa mbona inakuwa ni aibu kubwa sana kwa wasomi wetu wa hicho kitivo cha Civil Engineering kuendelea kujiona kama ni Ma-Professor na Ma-Engineer wakati ambapo hamna uwezo wa kulisaidia Taifa letu kutatua matatizo kama haya ya mafuriko yanayo tokea kila mwaka. Ni maengineer gani nyie ambao hmtambui wajibu kama wabobeaji wa maswala haya? Mnatia aibu kiasi kwamba hata sisi maengineer wa Faculties nyingine kama Mechanical, Elictrical na wengineo tunaoneka vilaza kama nyie.

Masikitiko yangu makubwa yawaende watu wanao jiita Ma Professor, wahandisi na wasomi wa vyuo vikuu vyetu vya Faculty ya Civil Engineering nchini kwa kushindwa kukabilina na changamoto kama hii ambayo kila mwaka ina wahathiri wakazi wa jiji letu la Dar es salaam na hivyo kuifanya nchi nzima iwe paralyzed.

Professor Mbalawa, Engineer Kamwelwe, Maprofessor na wahandisi wote mlio maliza na ambao bado mko masomoni kwenye Kitivo cha Civil Engineering wa vyuo vikuu nchini, mnadhani kuna umuhimu wa watanzania kuendelea kugharamia Faculty hii ya Civil Engineering kwenye vyuo vyetu?

Mimi inaniwia vigimu sana kuelewa kwa nini wasomi na wataalam walio bobea wa kitengo hiki cha ujenzi kushindwa kuthibiti hali hii ambayo kila mwaka hutokea na kuathiri maisha, mali na shughuli zetu wenyewe. Kama wasomi na wataalam mnaweza kulala vizuri na kwa amani kweli?

Professor Mbalawa na Engineer kamwelwe, Maprofessor na Ma-Engineer wengine wa hii Fuculty ya Civil Engineering na watu wa mipango miji wa mkoa au Taifa mnashindwa kweli kushauriana na Rais Magufuli na mawaziri wengine wanao husika kuacha mara moja miradi yote mingine ambayo iko katika pipe line ya mpango wa kutekelezwa, ili kuanza mara moja uwezekano wa kutafuta jawabu la hii changamoto ambayo ina wafanya wananchi wote kuwa paralyzed na maafa haya ya mafuriko kila mwaka? Kama mvua ya masaa machache inasababisha maafa ya aina hiyo je mvua za siku tatu mfululizo zita leta maafa ya namna gani?

Hivi, hamjitabui kuwa nyie ndiyo malaika wa nchi yetu, na kwamba ustawi wa miji yetu inawategemea nyinyi? Sasa kama nyie malaika wetu kwa vipaji mlivyo navyo, uwezo mlio nao na utashi wenu collectively mnashindwa kujituma kukabilina na matatizo haya, mnategemea nani atayatatua? Na je, mnategemea serikali inayo tawala na wananchi kwa ujumla wataweza kuwaamini nyie na kuwapa miradi ambayo kila mara mnashindwa kuitekeleza kwa ufanisi unao takiwa? Mnataka watu wawe wanawazomea kama wana CCM awamu ya nne walivyo kuwa wakinyanyasika kwa kuzomewa na kuwa mocked wakionekana wamevaa magwanda yao ya kijani na yellow?

Hivi, kitendo cha kukahidi au kushindwa kutekeleza wajibu wenu kama wataalam, mnadhani mnamkomoa nani? Hamjui kuwa nyie ndiyo watu mnaotakiwa kulisimamia Taifa letu lika imarika kwa manufaa yetu sote na vizazi vyetu vya baadae?
Kwenye daraja kama hili la Mbezi ya chini kuna ugumu gani kulitengeneza likawa imara na kudumu mda mrefu? Na hela ambazo serikali inge serve zingeweza kutumika katika maeneo mengine ambako hakuna miundo mbinu mizuri na watu kupata shida?

Lawama nyingine ningependa ziwaendee watendaji na watumishi wa serikali wanao husika na maswala ya uokoaji. Ina maana vitengo vyote vya serikali vinavyo husika na maswala ya uokoaji kama Zimamoto na vinginevyo vilishindwa kweli kupeleka wataalam na vifaa kwenye maeneo ambayo wana yaona critical?
Scene kama hii ina maana kikosi cha zimamoto kilishindwa kweli kupeleka wataalam na vifaa vinavyo husika kwa kazi hiyo ili kumwokoa huyu mwana dada kutoka kwenye hilo janga? Kama huyu mwana dada alikaa mda mrefu bila kuokolewa na Fire Briged, kunafaida gani kuendelea kuwa na kitengo kama hiki ambacho hakina faida kwa wananchi? Si afadhali hiyo kazi ikapewa private sector ikatoa Service nzuri kwa umma? Jangwani yote sijaona gari la zimamoto na wanajeshi wa zima moto wakiwa stand by. Ni polisi tu ambao walikuwa wakizuia watu wasipite na hiyo baadae sana.

Mimi nashindwa elewa inakuwaje mtu anapewa mafunzo ya kuperform task fulani na kuwa specialist, halafi kwenye incidents kama hizi, ambapo anatakiwa kuwajibika, anashindwa kutekeleza wajibu wake ambao umma umemwamini na badala yake kujichimbia kwenye ofisi zao au nyumba zao. Watu kama hawa watakuwa na akili gani hasa ya kukosa uelewa na wajibu wa kutekeleza kazi zao?

Kwa swala hili la kukosa utendaji wa majukumu waliyo pewa, ningependa kusikia majibu ya watumishi wa serikali wanao husika na maswala ya uokoaji, nini hasa mpangilio wao wa kazi, kiasi kwamba wakakosa ile uhodari na ujasiri wa kujituma kufanya kazi zao kwa Passion?

Rais Magufuli nakuomba hii hali ya kutopenda kjituma na kuwajibika kwa watu walio pewa dhana na umma inayoendelea nchini, kuiangalia kwa makini sana, maana inaonyesha kana kwamba kwenye jamii yetu kuna ugonjwa umetuingia ambao unatufanya sisi kuwa unconcerned. Hatu react ipasavyo katika Situation knapp bidi kufanya hivyo.

Watanzania tumekuwa watu wa porojo sana na wavivu katika kuwaza na kutenda pindi inapo bidi. Tukiendelea hivi sita shangaa wala kustaajabu kusikia kuwa vizazi vyetu huko mbele vinashindwa kukabilina na matatizo yanayo wahusu wao, na hivyo kukubali kirahisi kuwa watumwa tena wa vizazi vya wenzetu tunao dai wametuzidi maarifa.

Ombi langu kwa Rais Magufuli, tafadhali itisha mkutano wa wahandisi wote na maprofessor wote nchini ili tuli jadili hili tatizo la kukosa uwajibikaji wa wahandisi wetu. Huo mkutano usiwe wa siku moja unaweza ukachukua hata wiki moja ili wahandisi wengi wapate nafasi ya kujieleza na kutoa mawazo yao ili tujie nini kifanyike ili kurudisha ile hali iliyo kuwepo enzi ya Mwalim Nyerere.

Kingine wape maengineer wetu wajibu wa kusimamia na kuchimba bonde la Msimbazi kwa uwezo wao wenyewe na kulifanya liwe bahari mpaka Surrender na kuwa tuorist attraction. Wakishindwa hiyo project basi ningekushauri kitivo chote cha Civil Engineering kwenye vyuo vyetu kifutwe completelly na wanafunzi watakao chukua masomo hayo wapelekwe kusoma nje.

Inatisha! Maengineer wazima wanashindwa hata kuweka Dimensions za kutengeneza ma-Culvert?
Ni aibu kubwa sana!
Ni aibu kubwa sana!
Ni aibu kubwa sana!
Ni aibu kubwa sana!
Ni aibu kubwa sana!





Sent using Jamii Forums mobile app

Umetoa povu kweli kweli.Lakini je,unajua kwamba mradi wowote unahitaji fedha na kusimamiwa vizuri katika utekelezaji na haya hayakuwepo katika awamu zilizopita?Na je,unajua kwamba ni awamu hii tu kumekuwa na nia ya kweli ya kuwasaidia Watanzania katika matatizo yao,ikiwa ni pamoja na eneo la miundo mbinu ya maji safi na taka?Unajua pia kwamba tenda za miradi katika awamu zilizopita zilikuwa zinatolewa kwa upendeleo na hata kampuni isiyokuwa na weledi ilikuwa inapata tenda,na hili liliathiri sana ubora wa miradi?Naomba utafakari kwanza kabla hujawanyooshea mainjinia vidole,huwezi kujipeleka mahali ambapo hutakiwi.Kwa awamu hii,civil engineers wanapata kazi na naweza kusema wanafanya kazi nzuri.Nategemea kwamba civil engineers wetu wataendelea kupewa kazi ili wapate uzoefu,walitengwa sana.
 
Huko Dar pambaneni na hali yenu maana mumelundikana kama nyumbu
By the way ukweli ni kwamba wakulaumiwa sio tu hao wasomi bali viongozi wa kisiasa pia,haiingii akilini nchi yote imejengwa ki slums yaani watu wameblock mikondo ya maji au namna ya kupitisha drainage structures ni ngumu kutokana na ujenzi holela
Serikali haitaki kutoa pesa ili kupima na kupanga matumizi sahihi ya ardhi nchini yaani ishu ya kupima viwanja inaonekana ni kwa ajili ya tabaka la wenye nacho huu kama sio ujinga ni nini.Kuna tatizo gani serikali kupima maeneo yote iwe la mtu binafsi au vyovyote ili mtu akitaka matumizi afuate kilichokuwa planned ili kukabiliana na matatizo kama hayo na mengine mtambuka ?
Ukweli mtupu mambo mengine ukiangalia hizo clips unajiuliza hivi afisa wa mipango miji, jamaa wa mazingira na wataalamu wengine hiyo mishahara wanapewa kwa shughuli gani.

Geography ya darasa la nne tunafundishwa mambo ya soil/river erosion na moja sababu kubwa ni maji.

Sasa wewe kweli unamwacha raia ajenge pembeni ya mto ambao unapita mjini auna buttress wall for soil protection, hakuna buffer zone for safety measure ili mali na uhai wa watu vilindwe just in case mto ukizidiwa na volumes maji wakati wa mvua kubwa; halafu tutegemee nini?

Atukatai kuna wakati mvua zinazidi njia za maji hila vitu vingine pamoja na kwamba vinasikitisha ila ukiona mazingira yenyewe ya watu walipojenga ukweli ni kwamba zilikuwa ni ajali tayari zinazosubiri muda wake tu zitokee; na viongozi wapo.
 
Jamaa naona unamtetea Mhe Jiwe. .. kwa utetezi wako huo wa kujipendekeza , huu Uzi hautokuwa na maana endapo tukafanya nadharia kuwa kwa Sasa Rais awe JK halafu waziri ni Magu..!

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1][emoji1][emoji1] Nimekupata mkuu. Si unamaanisha Mh. Jiwe alipo kuwa na wadhifa wa uwaziri wa ujenzi? Au nimekuelewa vibaya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kujenga ajenge mchina ,lawama apewe mkandarasi mbongo, this is not fair.
 
Kwa hiyo mafuriko yakiwepo huko California ndiyo na hapa Dar es Salaam kwetu lazima yawepo? Nyie mkiambiwa mnamuabudu Mzungu aka Beberu mnaruka kimanga wakati matendo na maneno yenu yanaonesha Beberu ni mungu wenu.
Hahaa ukitaka kujua jiwe na wafuasi wake wanaabudu wazungu ni pale balozi wa nchi ya kizungu akiongea Kiswahili, jiwe anachanganyikiwa na kuanza kumsifia hadi basi
Lakini balozi wa Zambia au Zimbabwe akiongea hata hamsifii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kwenye Luninha tuu, pamoja na kushusha bendera za Chadema maana ndizo zimeleta mafuriko
 
Sasa wewe mishahara yenyewe kiduchu visipoharbika tutakula wapi. Bora viharbike harbike Mara nyingi ili tule Mara nyingi. Nasisi ndy kula yetu mana tumesoma kuliko wanasiasa na tunafanya kaz ngumu kuliko wao lakini wao wanapata mahela kuliko sisi. The world isn't Fair!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana! Hicho ndicho nilicho kuwa nasubiri kukisikia. Nilikuwa najiuliza haya yana tokea tatizo liko wapi?

Sitaki kuamini kuwa nyie maengineer na mnashindwa kutekeleza wajibu wenu kwa ufanisi, tatizo kumabe ni mgogoro kati yenu na wana siasa katika malipo.

Natumia kuwa vyombo vinavyo husika na uratibu wa maswala ya malipo linaweza zingatia malalamiko yako wakaangalia uwezekano wa kuikabili hii itilafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa wewe mishahara yenyewe kiduchu visipoharbika tutakula wapi. Bora viharbike harbike Mara nyingi ili tule Mara nyingi. Nasisi ndy kula yetu mana tumesoma kuliko wanasiasa na tunafanya kaz ngumu kuliko wao lakini wao wanapata mahela kuliko sisi. The world isn't Fair!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sababu ndo hiyo,Aliyekubali kupitisha ramani ya kujenga barabara pale Jangwani alitakiwa anyongwe tu!!! Narudia kwa sauti ANYONGWE!!! hivi wakati jeshi wanakuja kuwaokoa raia mwaka 2014 kama sikosei hakuona madhara ya kuipitisha chinichini vile.China imeendelea kwa sababu haikopeshi wapuuzi wa dizaini hizo
 
Back
Top Bottom