UPDATES: Madhara ya mvua iliyonyesha jijini Dar - Desemba 17, 2019

UPDATES: Madhara ya mvua iliyonyesha jijini Dar - Desemba 17, 2019

Tunasubiri Daraja la Mita 300 kwenda juu kujengwa pale Jangwani.
 
View attachment 1296605
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Disemba 18 ametembelea na kukagua miundombinu iliyoharibiwa na Mvua ambapo amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali ipo katika hatua ya kukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa na Mvua ili irudi katika hali ya kawaida na kuwaondolea wananchi kero.

RC Makonda amesema Serikali imejitaidi kwa kiasi kikubwa Kujenga miundombinu ya kupitisha maji ya Mvua ikiwemo upanuzi wa Mito, Madaraja na Mifereji lakini kinachotokea ni tabia chafu ya baadhi ya Wananchi kutupa taka kwenye miundombinu hiyo jambo linalosababisha maji kushindwa kupita kwenye njia yake na kusababisha mafuriko.

Aidha RC Makonda amewataka wananchi waliojenga na wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhakikisha wanahama kwakuwa Mvua bado zitaendelea kunyesha kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Hata hivyo RC Makonda amesema Serikali kwa sasa inaendelea kutekeleza miradi mikubwa Ujenzi wa Mito na Mifereji kwa lengo la kupunguza kero mafuriko kwa wawananchi ambapo kwa Wilaya ya Ilala kuna ujenzi wa Mito yenye urefu wa Km 16, Temeke Km 14 na Kinondoni Km 8 ili maji yaende moja kwa moja Baharini.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi na Upanuzi wa Mto Ng’ombe, Mto Msimbazi, Ujenzi wa Daraja la Juu eneo la Jangwani pamoja na Maboresho ya eneo hilo ili liweze kutumika kwa shughuli za utalii wa Boti.
Nyie mnajenga mtoni halafu eti makonda awatetee. Mtu Akisikia mbezi Beach roho inamtoka amesahau kabisa kuwa kuna njia za maji. Mtu yupo bize kuwatania watu wa Mbagala Gongo la Mboto na Buza. Haya sasa wezenu wamevaa raba zao wanadunda nyie mnaogelea kwenye mavi mnalala juu ya Bati. Pumbavu makonda awafanyie nini. hameni mabondeni acha kufuata jina la eneo. Usalama wako kwanza mtakufa maji nyie kunguru wa sinza na misifa yakijinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..kichwa cha habari husika.

..kwanini tunatumia mabilioni kujenga daraja la Coco beach badala ya ku-mobilise fedha za kujenga miundombinu ya kudhibiti mafuriko ktk mji wetu?

..mnaounga mkono kila kitu mnakaribishwa kuchangia.

..na wale mnaopinga kila kitu karibuni pia.

..mimi nimeuliza swali tu.
 
Kwa sababu daraja la zamani la Salender linatakiwa kutanuliwa, hawawezi kufanya hivyo bila njia mbadala.

Mwenge Morocco barabara inatanuliwa na kuwekwa mwendo kasi, hiyo njia ya mwendo kasi inatakiwa mpaka stesheni ya SGR. Inamaana Salender bridge lazima libomolewe ili lijengwe lingine lenye njia 8 au 6 na barabara ya mwendokasi, njia mbadala inatakiwa ili salender iweze bomolewa na kujengwa upya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hua hafanyi kitu bila yeye kunufaika, daraja la Coco Wala sio mbadala wa foleni, Ni kwaajili ya matajiri wachache wasiotaka kero, daraja linapotokea Kuna makazi ya swahiba wake lukuvi, yule mmiliki wa shivacom, Ana nyumba yake pia, Kuna azim dewji..shtuka!
 
..kichwa cha habari husika.

..kwanini tunatumia mabilioni kujenga daraja la Coco beach badala ya ku-mobilise fedha za kujenga miundombinu ya kudhibiti mafuriko ktk mji wetu?

..mnaounga mkono kila kitu mnakaribishwa kuchangia.

..na wale mnaopinga kila kitu karibuni pia.

..mimi nimeuliza swali tu.
1.Nini ni gharama ya kutengeneza hiyo miundo mbinu ya kuondoa kero ya mafuriko Dar vs gharama za hilo daraja la coco
2.huko nyuma mbona kulikuwa hakuna hayo mafuriko ya kuhitaji uwekezaji mkubwa kama huu, tatizo ni nini, ili tuwe tuna panga mipango kabla ya hatari??
3.je uwekezaji huu wa mifumo ya kutoa maji utakuwa na tija ukilinganisha ni mara ngapi matatizo haya hutokea
 
..kichwa cha habari husika.

..kwanini tunatumia mabilioni kujenga daraja la Coco beach badala ya ku-mobilise fedha za kujenga miundombinu ya kudhibiti mafuriko ktk mji wetu?

..mnaounga mkono kila kitu mnakaribishwa kuchangia.

..na wale mnaopinga kila kitu karibuni pia.

..mimi nimeuliza swali tu.
Una hoja nzuri sana, nionavyo mimi baada ya awamu yenyewe kupita tunaweza kuwa na structures nyingi za maonyesho lakini zisizotatua changamoto za jiji,
 
Haya ni mambo ya upangaji vipaumbele vyetu,
Nini daraja la Kigamboni, mimi sio mchumi ila ukiangalia kiasi cha fedha kinachotumika ku fund strategic project; uka imagine kama such amount zingekuwa invested kwenye kilimo ambacho ndio tegemeo la walio wengi, ni wapi tungepata multipliers effect kubwa, wenzetu hawaoni.

Tulipoanza kuhubiri Tanzania ya viwanda, akina sisi tukauliza where is the blue print ya Tanzania ya viwanda?, tunataka viwanda gani, kuzalisha nini, kwa malighafi gani, technology gani, nguvu kazi gani na capital injection kutoka wapi, wanakuwa wakali na kuelezwa hata Cheregani 4 ni kiwanda!.

Tukasema kwa vile Tanzania tunategenea kilimo, Tanzania ya viwanda vya kweli ni Tanzania ya agro processing industries, hivyo the focus of Tanzania ya viwanda should have been kuanza kwa ku invest kwenye kilimo, kizalishe malighafi ya viwanda tuzalishe bidhaa tujitisheleze na ziada tu export, wenzetu wakaamua tununue ndege kwa cash!, tena bila business plan, ndege zikishafika ndipo tunaoanga!.

Baada ya miaka mitatu ya rais Magufuli ndipo tumekumbuka kilimo, rais Magufuli akazindua ASDPIi. Sasa tunaelekea mwaka wa 5 wa rais Magufuli ndipo Blue Print ya Tanzania ya viwanda itatoka!.

Hii ndio Tanzania yetu na hivi ndio vipaumbele vyetu. "Sipangiwi!".

P
 
..kichwa cha habari husika.

..kwanini tunatumia mabilioni kujenga daraja la Coco beach badala ya ku-mobilise fedha za kujenga miundombinu ya kudhibiti mafuriko ktk mji wetu?

..mnaounga mkono kila kitu mnakaribishwa kuchangia.

..na wale mnaopinga kila kitu karibuni pia.

..mimi nimeuliza swali tu.

Nadhani kuna tatizo kubwa zaidi kuliko uchaguzi wa vipaumbele hapa. Maintenance ya barabara mijini hasa uzibuaji wa mitaro ya maji kimsingi linapaswa kuwa zoezi endelevu (routine) ambalo halipaswi kushindanishwa na mradi mwingine wowote. Hili halikifanyiki na ndicho chanzo kikubwa cha mafuriko hasa katikati ya jiji la Dar. Hivyo tatizo hapa ni kukosekana kwa maintenance culture.

Kwa upande mwingine, daraja jipya la Salender linajengwa kwa fedha aidha za msaada au mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Korea Kusini na ni tatokeo ya urafiki wa Rais Kikwete na aliyekuwa waziri wa nje wa Korea/katibu mkuu UN, Ban Ki Moon.

Sasa kwa nini hili daraja likawa kipaumbele hilo ni suala lingine. Hata hivyo wazo la kuwepo kwa hili darala ni la muda mrefu kama njia ya kupunguza foleni Bagamoyo Rd. Nafikiri uwepo wa ubalozi wa Korea Kusini eneo la Masaki umechangia kushawishi huu kuwepo kwa huu mradi.
 
Back
Top Bottom