BilioneaPATIGOO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 12,320
- 11,327
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyie mnajenga mtoni halafu eti makonda awatetee. Mtu Akisikia mbezi Beach roho inamtoka amesahau kabisa kuwa kuna njia za maji. Mtu yupo bize kuwatania watu wa Mbagala Gongo la Mboto na Buza. Haya sasa wezenu wamevaa raba zao wanadunda nyie mnaogelea kwenye mavi mnalala juu ya Bati. Pumbavu makonda awafanyie nini. hameni mabondeni acha kufuata jina la eneo. Usalama wako kwanza mtakufa maji nyie kunguru wa sinza na misifa yakijingaView attachment 1296605
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Disemba 18 ametembelea na kukagua miundombinu iliyoharibiwa na Mvua ambapo amewahakikishia Wananchi kuwa Serikali ipo katika hatua ya kukarabati miundombinu yote iliyoharibiwa na Mvua ili irudi katika hali ya kawaida na kuwaondolea wananchi kero.
RC Makonda amesema Serikali imejitaidi kwa kiasi kikubwa Kujenga miundombinu ya kupitisha maji ya Mvua ikiwemo upanuzi wa Mito, Madaraja na Mifereji lakini kinachotokea ni tabia chafu ya baadhi ya Wananchi kutupa taka kwenye miundombinu hiyo jambo linalosababisha maji kushindwa kupita kwenye njia yake na kusababisha mafuriko.
Aidha RC Makonda amewataka wananchi waliojenga na wanaoishi katika maeneo hatarishi kuhakikisha wanahama kwakuwa Mvua bado zitaendelea kunyesha kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa.
Hata hivyo RC Makonda amesema Serikali kwa sasa inaendelea kutekeleza miradi mikubwa Ujenzi wa Mito na Mifereji kwa lengo la kupunguza kero mafuriko kwa wawananchi ambapo kwa Wilaya ya Ilala kuna ujenzi wa Mito yenye urefu wa Km 16, Temeke Km 14 na Kinondoni Km 8 ili maji yaende moja kwa moja Baharini.
Pamoja na hayo RC Makonda amesema miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na Ujenzi na Upanuzi wa Mto Ng’ombe, Mto Msimbazi, Ujenzi wa Daraja la Juu eneo la Jangwani pamoja na Maboresho ya eneo hilo ili liweze kutumika kwa shughuli za utalii wa Boti.
Kwa mujibu wa BASHITE anauwezo wa kuongea na mola na mvua isinyeshe. Kwahiyo mambo ya kudhibiti mafuriko yy atamaliza.
Sent using Jamii Forums mobile app
1.Nini ni gharama ya kutengeneza hiyo miundo mbinu ya kuondoa kero ya mafuriko Dar vs gharama za hilo daraja la coco..kichwa cha habari husika.
..kwanini tunatumia mabilioni kujenga daraja la Coco beach badala ya ku-mobilise fedha za kujenga miundombinu ya kudhibiti mafuriko ktk mji wetu?
..mnaounga mkono kila kitu mnakaribishwa kuchangia.
..na wale mnaopinga kila kitu karibuni pia.
..mimi nimeuliza swali tu.
Ujenzi wa kujenga daraja Jangwan Hivi hamkulijua mapema au ndy Mnataka muwe mnapiga Hela tu kwenye miradiAmefanya vizuri kuwajali Wananchi wake
Una hoja nzuri sana, nionavyo mimi baada ya awamu yenyewe kupita tunaweza kuwa na structures nyingi za maonyesho lakini zisizotatua changamoto za jiji,..kichwa cha habari husika.
..kwanini tunatumia mabilioni kujenga daraja la Coco beach badala ya ku-mobilise fedha za kujenga miundombinu ya kudhibiti mafuriko ktk mji wetu?
..mnaounga mkono kila kitu mnakaribishwa kuchangia.
..na wale mnaopinga kila kitu karibuni pia.
..mimi nimeuliza swali tu.
..kichwa cha habari husika.
..kwanini tunatumia mabilioni kujenga daraja la Coco beach badala ya ku-mobilise fedha za kujenga miundombinu ya kudhibiti mafuriko ktk mji wetu?
..mnaounga mkono kila kitu mnakaribishwa kuchangia.
..na wale mnaopinga kila kitu karibuni pia.
..mimi nimeuliza swali tu.