UPDATES: Madhara ya mvua iliyonyesha jijini Dar - Desemba 17, 2019

Saint Ivuga, [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Unajitambua wewe kwa haya uliyo yandika?

Naomba nikuulize swali; Civil Engineering iko mda gani nchini? Ma kuna Maengineer, Ma PHD na Ma-Professor wangapi wamehitimu shahada zao na kuingia katika System kwa malengo ya kuboresha maisha ya wananchi na kuleta maendeleo ya nchi?

Huyo Mheshimiwa unaye mpa lawama siku za nyuma alikuwa kama nani? Mbona hushangai kuwa vitendo hivi vya Maengineer kuhujumu uchumi si vilikuwepo pia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
areafiftyone, Nakushukuru mkuu kwa kunijuza.

Ni kweli nimetoa povu kweli kweli, hii imesababishwa na kukereka kwa kiasi kikubwa kuona kwamba wananchi masikini wanajitahidi kwa kidogo walicho nacho kuwa saidia nyie wakufunzi wa elimu ya civil Engineering mhitimu shahada zenu ili hatimaye mje kusaidia kujenga Taifa letu kwa kuwarahisishia wananchi masikini maisha yao kwa kuweka miundo mbinu iwe mahiri.

Lakini matokeo wanayo yapata watu hao masikini kwa jitihada zao zote hizo, is a kick on a buttock. Wahenga walisema; "Fadhila za punda ni mateke". Badala ya kujenga mna bomoa. Sasa hii maana yake ni nini?

Kama kweli ni awamu hii tu kumekuwa na nia ya kweli ya kuwasaidia Watanzania katika matatizo yao, ikiwa ni pamoja na eneo la miundo mbinu ya maji safi na taka, sasa haya matatizo ya mafuriko tunayo yaona mnashindwa nini kukabilina nayo?

Na kama tenda za miradi katika awamu zilizopita zilikuwa zinatolewa kwa upendeleo na hata kampuni isiyokuwa na weledi ilikuwa inapata tenda, na kulingana na kauli yako, kuathiri sana ubora wa miradi, sasa mbona nyie hamkuweza ku take appropriate measures in oder to make people aware of this kind of feudalism, kiasi kwamba wananchi wakaungana mkono na nyie katika kumshauri Rais wa wakati huo kuchukua hatua stahiki kukomesha ulaini huo?

A can only hope that siku za mbele mtakuwa mmejifunza kuchukua hatua zinastahili ili kurahisisha ufanis wa kazi zenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tokyo massive flood protection facility
View attachment 1295951View attachment 1295952View attachment 1295953Mnaweza kwenda YouTube weyewe mjionee sina cha kuongeza mtoa mada
Hii System haipo Japan tu bali nchi nyingi za Europe wana System hii. Ni Afrika zu na hasa Tanzania bado tuna solve Problems zetu kwa dhana za kikoloni ambazo zimepitwa na wakati. Na ndiyo maana ni kitu cha kushangaza kwanini Ma- Civil Engineer wetu wanashindwa kuiga solution za nchi zilizoendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilatha,
Watu wa mipango miji hawawezi kupita kila mahali na kila sehemu kukataza matumizi yasiyo sahihi ya ardhi maana wao ni watekelezaji ila sio wmiliki

Sheria za kuzuia ujenzi holela zipo ila wenye mamlaka ya kusimamia sheria ni watu wa utawala na polisi sasa kama wanasiasa wako kimya hao wengine huwa hawana nguvu maana hawana maamuzi ya moja kwa moja.Tuanze na wewe umejenga kwenye plot au squatter? kama ni squatter kwa nini hukufuata sheria? Ni lazima jambo hili litiliwe mkazo na uongozi wa nchi kwanza ndio law enforcers watawajibika bila bughudha
 
Duuh! Hiyo kali! Haya tutajitahidi tufike huko!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni mipango miji na watu kujenga bila ya ushauri wa kitaalamu.
Kwa mfano wewe uliyeleta Uzi huu nyumba yako umeijenga kwa kufuata utaratibu/kibali?
 
Mkuu huoni kama umetoka nje ya mstari? Hakuna mtu katika mada hii amezungumzia kuhusu watu wa mipango miji na matumizi holela ya ardhi.

Kwa upande mwingine naona kama unaji-contradict mwenyewe vile? Kama wewe mwenyewe unasema kuwa sheria za kuzuia ujenzi holela zipo, sasa itakuwaje watu wa utawala na wana siasa wanahusika katika mamlaka ya kusimamia na vizui sheria hizo?
Mimi nilifikiri Judiciary, polisi na magereza ndiyo wahusika wakuu?

Nafikiri sina ulazima wa kujibu personal question, hasa tukizingatia kuwa maswala yaliyongelea kwenye hii mada ni kuhusu legitimacy ya wananchi kuendelea kugharimia kitivo cha Civil Engineering kwenye vyuo vyetu kikuu, wakati out come yake ni very small.

Hakuna faida yeyote ile tunayo pata kutokana na hiki kitivo. Kwa kukosa umakini wao wa kufanya kazi kwa kujiamini hiki kitivo kina isababishia serikali hivyo umma kugharamia ujenzi wa miradi ya mabarabara, maculvert na madaraja mara dugu zaidi kuliko ilivyo tegenewa kwa kuroa tenda kwa makampuni ya nje ana kuwasomesha wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Civil Engineers ndio ambao wanatoa vibali kujenga makazi ya watu kwenye njia na makazi ya maji?
Liko wapi 'ziwa Mwananyamara'?
Liko wapi 'ziwa Tandale'?
Liko wapi 'ziwa magomeni'?
Uko wapi 'mto Sinza'?
Kweli 'Ngwini' hamnazo!
 
ChoiceVariable,
Kuna vitu vingine vinawezekana Tanzania tu.

Kabla ata ujajenga ili kupata hati ya kiwanja ardhi inapimwa na surveyors wa serikari.

Ukiangalia hizo video haswa hiyo ya jamvi TV kuna sehemu huyo dada katembelea Sinza Kamanyola: unaona mtu analalamika kupoteza mali zilizochukuliwa na maji wakati jengo la biashara yake lipo on the edge of the ‘river bank’.

Cha kujiuliza huyo surveyor alieenda kuwapimia watu viwanja hayo maeneo hajui kwamba hiyo sehemu ipo juu ya saturated soil ambayo hata bila ya mvua chances ya hiyo ardhi kumomonyoka ni high, aoni hakuna buffer zone, aoni risk luluki zilizokuweko hapo.

Wanasiasa sio wataalamu per se in many cases ndio maana kuanzia kwenye ngazi za serikari za mitaa mpaka serikari kuu kila sehemu ina mwanasheria, kila aina wa engineer, surveyor; etc na wataalamu. Bado tena wanashirikiana na taasisi zingine kama NEMC ni jukumu lao kumshauri kiongozi actions gani muhimu za kuchukua katika kulinda usalama wa raia.

Sasa inakuwaje hadi inafikia hatua watu wanajenga maeneo kama hayo na hakuna anae liongelea, kuna lawama za kutosha hapo kugawanywa kwa wahusika mbali mbali zaidi ya wanasiasa.

Kuhusu mimi ninapoishi kwa kweli mafuriko hayajawahi kutokea wala umeme kukatika hata miaka ambayo mgao ulipokuwa tatizo sugu nchi nzima; kwa hilo nashukuru mungu.
 
Watu wa dar sijui wakoje yaani mvua kidogo tu wanalalamika, alafu nashangaa mvua inaweza nyesha mikoa mingine sana tu nani mvua ya nguvu lakini husikii watu wa mikoa hiyo wakilalamika jamani mvua jamani mvua, lakini watu wa mkoa wa dar kamvua kadoo tu basi dunia nzima itajua mvua imenyesha dar kwa kulalamika na kupicha picha mvua utadhani hawajawahi ona mvua, mi wananikera sana , kamvua ka jana kidogo tu basi watu wanalia lia sana utafikiri yatima
 
Kilatha,
Paragraph ya mwisho tu ndio nimeielewa mkuu,haaaa
Ila kama hujaona uzito wa wafanya maamuzi yaani wanasiasa walioshikilia mpini kwenye hili tutasubili sana na mambo yataendelea hivi hivi

Binafsi ningekuwa mkubwa kuanzia level ya katibu mkuu,waziri and above jambbo la kwanza kulishikia bango lingekuwa la kuunda mamlaka au tume ya ardhi na mipango miji ili kupata fedha na kudhibiti ujenzi holela hii ya kuwaachia serikali za mitaa imeshashindwa kitambo
 
Tokyo massive flood protection facility
View attachment 1295951View attachment 1295952View attachment 1295953Mnaweza kwenda YouTube weyewe mjionee sina cha kuongeza mtoa mada
Hizo nyumba za Dar ebu fanya kama unaziwekea hiyo massive flood protection.
Issue sio Civil Engineering, issue ni Mipango Miji na sisi wenyewe kujenga nyumba zetu pasipo ushauri wa kitaalamu,lakini pia tukiambiwa tuhame tupishe uboreshaji wa miji hatutaki tunataka kuishi mjini.
75% ya wakazi wa Dar hasa mjini kati inabidi waamishwe ili kujenga miundombinu imara.
 
Hivi hili swala la mafuriko limeshashindikana kabisa hapa Dar es Salaam?
 
Hivi hili swala la mafuriko limeshashindikana kabisa hapa Dar es Salaam?
 
Hivi hili swala la mafuriko limeshashindikana kabisa hapa Dar es Salaam?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…