Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
Ukimwangalia mkuu wa mkoa wa Dar unaweza dhani viongozi ndio wanavyofanya kazi kwa kujiamulia tu.Paragraph ya mwisho tu ndio nimeielewa mkuu,haaaa
Ila kama hujaona uzito wa wafanya maamuzi yaani wanasiasa walioshikilia mpini kwenye hili tutasubili sana na mambo yataendelea hivi hivi
Binafsi ningekuwa mkubwa kuanzia level ya katibu mkuu,waziri and above jambbo la kwanza kulishikia bango lingekuwa la kuunda mamlaka au tume ya ardhi na mipango miji ili kupata fedha na kudhibiti ujenzi holela hii ya kuwaachia serikali za mitaa imeshashindwa kitambo
Kama unatazama video za ziara za Magu utaona serikari inavyofanya kazi. Akiona mkuu wa wilaya anasua sua na majibu next mkurugenzi na yeye akishindwa anaenda kwa wataalamu husika iwe engineer wa maji, TANROAD, etc kutoa ufafanuzi kuhusu maswala husika.
Halafu baada ya hapo akiamua anawarudia kuwaponda mkurugenzi na mkuu wa wilaya kwa kutokuwa updated na shughuli zao.
Maana yake nini wakuu wa wilaya na hata mawaziri kwenye maamuzi wanategemea ushauri wa wataalamu, ivyo ndio serikari zinavyoendeshwa duniani katika nafasi za utendaji.
Sasa mkuu wa wilaya au mkoa asielewa impact za river erosion, soil saturation, umuhimu wa kuta za mito mjini, uelewa wa maswala flow rates etc to do with physical geography risk aversion na engineering sehemu za makazi atachukua maamuzi gani ya kinga. Anaweza pita sehemu inayohitaji attention asijue mpaka madhara yanapotokea.
Hapo ndio wataalamu wanapoingia kama engineers, jamaa wa mipango miji, environment; etc with government experts.