Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Leo ni August 1,2015 Wanachama wa chama cha Mapinduzi (CCM) nchi nzima wanakusanyika katika maeneo ya matawi yao kuchagua mgombea mmoja atakayeshindana na wagombea wengine kutoka vyama tofauti na CCM.

Mchakato wa kampeini katika mkoa huu zimetawaliwa na vituko,udhalilishaji kwa baadhi wa wagombea hivyo hata upigaji kura za maoni utakuwa hivo hivyo,hii ndiyo sababu inatufanya tufuatilie live kura hizi..






kumekucha
 
MWAKYEMBE AWABWAGA MWAKALINGA, LOWASSA NA KYELA FM KWA KISHINDO
Na Malikira S.

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Kyela aliyemaliza muda wake, Dk. Harrison Mwakyembe, amewabwaga kwa kishindo kikubwa wahasimu wake wa kisiasa kwenye kura za maoni zilizofanyika wilayani Kyela leo.

Muda wa saa kumi jioni ulipotimu wa kukamilisha upigaji kura, Mwakyembe alikuwa tayari anaongoza kwenye vituo karibu vyote kwa zaidi ya asilimia 75, akiwaacha kwa mbali wagombea ubunge wenzake 9 akiwemo George Mwakalinga anayeishi Uingereza na kuitumia redio yake, Kyela FM, kinyume na taratibu kwa kujitangaza kwa wiki mbili mfululizo kuwa chaguo bora na kumkandia Dk. Mwakyembe kuwa hafai.

Mwakalinga, mhandisi aliyekosa kabisa haiba ya uanasiasa kutokana na uongeaji wake wa taratibu usio na mvuto na hasira kali za papo kwa papo, anadaiwa kuwa karibu na Edward Lowassa, mwanasiasa mkongwe nchini aliyehamia CHADEMA kutoka CCM hivi majuzi, kutokana na kaka yake Mwakalinga kuoa Monduli.

Pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) kumtahadharisha asiitumie kisiasa redio yake aliyoisajili kama redio ya jamii kwa kukejeli, kutukana na kudhalilisha wengine, Mwakalinga kwa kushirikiana na wanasiasa wenzake wanane walioungana naye kumkabili Mwakyembe, ameendelea kuitumia Kyela FM kumshambulia Dk. Mwakyembe na kuwasihi wananchi wasimpe kura.

Mwakalinga kwa kushirikiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kyela, Gabriel Kipija, mwanasiasa mchanga anayefundisha Chuo cha Uhasibu Mbeya, John Mwaipopo na mkandarasi anayetuhumiwa kuchelewesha miradi mitatu ya barabara wilayani Kyela, Vincent Mwamakimbula, wamekuwa wakiwalipa fedha wafuasi wa CHADEMA kumfanyia fujo Dk. Mwakyembe kwenye mikutano ya kujinadi kwa nia ya kumvunja moyo.

Dk. Mwakyembe kama ilivyo kwa wanasiasa wazoefu, hakuteteleka na aliendelea kuelezea utekelezaji wa Ilani za Uchaguzi za CCM za 2005 na 2010 na kuwathibitishia wananchi Kyela kuwa wilaya yao imepiga hatua kubwa ya maendeleo.

Idadi kubwa ya wananchi Kyela hawajafurahishwa na udhaifu wa TCRA wa kushindwa kusimamia sheria zake, hivyo kuiacha Kyela FM ikivuruga mchakato wa kidemokrasia ndani ya CCM kwa zaidi ya wiki mbili.

Taarifa tulizopokea toka kwa mawakala wa vituo karibu vyote wilayani Kyela zinaonyesha Mwakyembe akiwa mbele ya wagombea wengine na huenda akapata zaidi ya asimilia 75 ya kura zote.

viva Dr Mwakyembe.
Erythrocyte , Ndalama niliwaambia mwakyembe akishindwa ntatembea uchi kutoka dsm mpaka matema.

Nyie watoto acheni nyege za kisiasa watu wazma tupo tunaijua system
 
Last edited by a moderator:
We mwenye ID ya ihanda vipi matokeo jimbo la kongwa kata ya mlali nghumbi iduo na sagara. Ndugai kavuna nini?
 
viva Dr Mwakyembe.
Erythrocyte , Ndalama niliwaambia mwakyembe akishindwa ntatembea uchi kutoka dsm mpaka matema.

Nyie watoto acheni nyege za kisiasa watu wazma tupo tunaijua system

mkuu mwakyembe atachakazwa vibaya sana na mwanyamaki , Mungu atupe uhai .
 
Last edited by a moderator:
Wana Musoma mjini wamezoea kwa jina baisikeli yakujifuniza ya Nyerere.Veda Mathayo ameshinda kwenye uchaguzi wa ndani ccm jimbo la Musoma mjini.tukutane October 25✌✌ hapa naona Nyerere hana mpizani kabisaaa..,
 
Miukawa imejazana humu wakati ya ccm hayawahusu . Kikosi kazi ndio kinaundwa leo. Tutakutana kwenye kampeni hapo baadae.
 
viva Dr Mwakyembe.
Erythrocyte , Ndalama niliwaambia mwakyembe akishindwa ntatembea uchi kutoka dsm mpaka matema.

Nyie watoto acheni nyege za kisiasa watu wazma tupo tunaijua system

Umenimention japo hatukupinga na mimi, hata hivyo kwani kachaguliwa? Kapendekezwa kugombea?
 
Last edited by a moderator:
mkuu mwakyembe atachakazwa vibaya sana na mwanyamaki , Mungu atupe uhai .

kijana bado hukubalian na mm eeeh?! Sasa subir mwanyamaki akishinda njoo unidai laki5 na ngwenda ikitali ukufuma kumbwan mpaka matema
 
Miukawa imejazana humu wakati ya ccm hayawahusu . Kikosi kazi ndio kinaundwa leo. Tutakutana kwenye kampeni hapo baadae.

mrembo wasikunyime usingiz hao. Tunawajua akili zao sawa na nyumbu. Kwahyo nyumbu asikuumize kichwa
 
Umenimention japo hatukupinga na mimi, hata hivyo kwani kachaguliwa? Kapendekezwa kugombea?

mkuu huyo ndio tapeperusha bendera ya ccm.
Hapo muhesabie kuwa ndo mbunge wako maana huyo wa chadema ataambulia %2 tu
 
Huyu Mama Kabaka anajisumbua na kupoteza fedha zake bure. Hamwezi hata kidogo Mhe. Esther Matiko. Tarehe 25.10.2015 mtakuja kuamini maneno yangu. CCM Tarime Mjini na Vijijini ilikwishakufa.
 
Matokeo ya kura za maoni jimbo kuu la kibakwe mpaka sasa yamepatikana katika kata saba , zote Eng. Mwikola amemgalagaza Mh Simbachawene kwa kura nyingi mno, Eng ameshinda kwa fujo sehemu zote ambapo matokeo yametangazwa mfano WOTTA, WANGI, KIBAKWE ZOTE MBILI CENTER NA JUU, WINZA

Mpaka mshindi ni ENG Mwikola akifuata kwa mbali Simbachawene,
 
Back
Top Bottom