Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Wagombea ubunge mkoa wa Mara Nyangwine na Gaudencia Kabaka wamedaiwa kuanza faulo kwenye kura za maoni baada ya karatasi za kupigia kura zaidi ya elfu ishirini kukamatwa zikiwa zimeshapigwa tiki za kuwachagua. Wagombea wenzao wamegomea zoezi hivyo zoezi litafanyikaupya kesho.

SOURCE: ITV Breaking News

Ndicho wanachoweza
 
Mambo ya magamba msilete huku ... hao wamezoea magoli ya mkono siku zote
 
Huu mfumo wa maccm tumeuuchoka
Waondolewe tuu October tumewachoka
 
Mathias Byabato

Umefanya vyema kutuwekea live updates, kuna watia nia hapo sioni kama wana sifa...mfano Karamagi,Kamala alitutukana kuwa tule nkende kama wanatusumbua shambani.

Dr. Aman na Kagasheki nao wapumzishwe walau siasa za Bukoba zirudi katika mstari.

Nkende ni ngedere....wengine wataelewa vibaya
 
Last edited by a moderator:
Tutafahamu jioni kati ya Sendeka na Toima....maana iko wazi kuwa Sendeka hatakiwi kabisa.
 
Kutoka Mkoani Kagera nakuletea LIVE UPDATES ikiwemo na matokeo kadri nitakavyoyapata.

Historia kidogo
Mkoa wa Kagera una majimbo tisa ya uchaguzi ambapo wabunge wawili tu wametangaza kung’atuka ambao ni Deogratias Ntukamazina wa Jimbo la Ngara na Bw Esutace Katagira wa jimbo la Kyelwa.

Saa 12:02 Adhuhuri
Hizi ni baadhi ya picha kutoka vituo mbalimbali katika kata zilizoko manispaa ya Bukoba.
wengine kutoka vyama tofauti na CCM.


View attachment 272870

View attachment 272871

View attachment 272872

Saa 10:38 Asubuhi
.Wanachama wa CCM wanaendelea na upigaji kura ingawa katika maeneo mbalimbali ya kata ya Kanyigo wilyani Missenyi wasimamizi wanalalamikia kuwepo kadi za ccm ambazo hazipo katika kitabu cha orodha ya wanachama

.Kata ya Nshambya Bukoba Mjini na maeneo mengine ya mji wa Bukoba zoezi linaendelea ingawa kuna wanachama wachache sana katika vituo.

.Mgombea mmoja katika jimbo la Bukoba(jina lake nitalitaja baada ya kupiga kura)jana aligoma kusaini makubaliano ya kutaka kila mgombea kukubaliana na matokeo na kuwa tayari kumuunga mkono atakayepitishwa .

.Wilayani Karagwe wanachama bado hawaamini macho wao kukuta wagombea wawili maarufu Gosbert Blandes(mbunge wa sasa) na Karimu Amri ambao walidaiwa kujitoa majina yao hayamo katika orodha ya wanaotakiwa kupigiwa kura.Hivyo hao wanachama siyo wagombea,baadhi ya akina mama wamegoma kupiga kura baadhi ya maeneo kwa kukosekana wagomea hao.

Wagombea kwa kila Jimbo

Bukoba Mjini:
Wagombea ni
1:Balozi Khamis Kagasheki,
2:Bw.George Rubaiyuka,
3:Bw. Josephat Kaijage,
4:Bi.Elieth Projestus
5: Dr.Anathory Amani,
6:Bw.Philbert Katabazi,
7:Bw.Mujuni Katarahiya
8: Bi.Celestina Rwezaura.

BukobaVijijini
Wagombea ni
1:Bw.Jasson Rweikiza ,
2:Bw. Nazir Karamagi
3:BW.Nelson Itagasa.

Muleba Kaskazini
Wagombea ni
1: Charles Mwijage
2: Bw.Ambrose Nshala.

Muleba Kusini
Wagombea ni
1😛rofesa Anna Tibaijuka,
2😀r Adam Nyaruhuma,
3:Bw.Stivin Tumaini,
4:Bw.Flavius Kahyoza,
5:Mhandisi Buruani Rubanzibwa,
6:Muhaji Bushako
7:Kaino Mendesi
8: Bw. Erick.

Jimbo la Ngara
Wagombea ni
1:Syprian Gwassa,
2😀r Philemon Rugumiliza,
3:Bi.Helen Adrian n
4:Bw.Wilbald Ede
5: Bw.Alex Gashaza,
6:Bw.Jelard Muhile,
7:Johakim Nchunda ,
8:Bw.Issa Samma
9: Bw.Ladslaus Bambanza.

Jimbo la Nkenge
Wagombea
1:Asumpta Mshama,
2😀iodorous Kamala,
3😀r Mazima,
4:Bw Frolent Kyombo,
5:Bw Julius Rugemalira
6:Bw......

Jimbo la Kyerwa
Wagombea ni .Innocent Seba Bilakwate,Stephano Edward Katemba
3.Lameck Chacha Ng’ang’a
4.Norbeth Kobwino
5.Sinsibath Kashunju Runyogote
6.Pancrace Shwekelela
7.Awaam Ahamada Ngalinda

Jimbo la Karagwe.
1.Mwalimu Dagobati Deogratias
2.Audax Christian Rukonge
3.Innocent Luga Bashungwa
4.Gosbert Begumisa Blandes
5.Alfred Rujwahuka
6.Amoni Chakushemeire Eustad
7.Karimu Amri

Duuu...huku ni kina muganyizi tuuu ...
hapa kuna kitu tofauti nimejifunza
maana sijaona hapo kina
Simba Mpunda (kutoka songea)
Mushi Kileo (wachaga)
Mwakatumbula Mwakyambiki (wanyakyusa)
Kikoti Kufakunoga (wahehe)
Ngosha N'gwanangwa (wasukuma)
Sanga Chengula (wakinga) n.k
hiyo ni baadhi tu ya mifano niliyoitoa ....wadau mnaweza toa zaidi.
 
Wameanza kuchanganyikiwa kabla ya oktoba.
 
Duuu...huku ni kina muganyizi tuuu ...
hapa kuna kitu tofauti nimejifunza
maana sijaona hapo kina
Simba Mpunda (kutoka songea)
Mushi Kileo (wachaga)
Mwakatumbula Mwakyambiki (wanyakyusa)
Kikoti Kufakunoga (wahehe)
Ngosha N'gwanangwa (wasukuma)
Sanga Chengula (wakinga) n.k
hiyo ni baadhi tu ya mifano niliyoitoa ....wadau mnaweza toa zaidi.

Unamaanisha.........!!!!
 
Dalili za kushindwa zimeanza kuonekana mapema
 
Niko hapa Majengo mapya Shy, nimepita kituo cha Shitta shule ya Msingi wasimamizi wanapapasana tu yaani watu hawapo kabisa! Magamba hapa mini wanapigwa tena!!! Safari hii ushindi wa kura 1 haukubaliki!

Wewe utakuwa umesahau hand goal
 
Back
Top Bottom