Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

jimbo la kibakwe simbachawene anagawa fedha kama njugu Jana hapa kwenye kitongoji cha msangambuya Kata ya mtera mnapanga foleni unapewa 10000/_ unaambiwa chagua simbachawene kwakweli mkoa wa Dodoma takukuru imelala kuliko mkoa wowote walikuwa wameuchuna tu naamini hata wao walipoozwa kwani simbachawene na mawakala wake wamegawa fedha mchana kweupe.binafsi nimepewa 10000 na kula simpi.

Tafuna mzee,kula ccm kura kwa ukawa
 
Adui namba moja wa taifa hili ni CCM. Mwenyezi Mungu tunusuru na janga hili Amen.
 
shaibu-aug1-2015.jpg

Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe

Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoani hapa kimetengua uteuzi wa aliyekuwa katibu wa chama hicho wilaya ya Newala, Juma Namkoveka, baada ya kukutwa akichapisha kura za maoni kwenye ofisi ya mmoja wa watia nia ya ubunge.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe, alisema katibu huyo alikutwa akichapisha karatasi hizo juzi saa 4 usiku katika ofisi ya Haroun Maarifa, ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha Radio Safari cha mjini Mtwara na mgombea ubunge wa jimbo la Newala mjini kupitia CCM.

Alisema kitendo cha karatasi hizo kukutwa katika ofisi ya mgombea ubunge hakiwezi kuaminiwa na wagombea wengine wanaowania jimbo hilo na hakistahili kufanywa na mgombea yeyote ili kuepusha migongano ya kimasilahi baina yao.

Alisema baada ya kukamata karatasi hizo zilipelekwa katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuzihifadhi, na kwamba jana alizichukua na kuzipeleka wilayani Newala ambako ndiko eneo sahihi lililotakiwa kuchapisha na sio mjini Mtwara kama ilivyofanywa na katibu huyo.

"Katika mazingira kama hayo kwa wagombea wengine wanaweza wakapata mashaka...Sasa baada ya kuchukua hizi hatua za mwanzo za kuhakikisha kwamba karatasi zinakuwa salama, tumeamua kwamba zikitoka polisi zile karatasi nitakabidhiwa na nitakwenda nazo Newala," alisema.

"Nikifika Newala nimemteua kaimu katibu wa wilaya mwingine, anaitwa Jenifer Chingwile, ni katibu msaidizi na muhasibu wa wilaya ya Tandahimba na nimeagiza nimkute Newala..lakini wakati huo huo aliyekuwa katibu wa wilaya ya Newala nimetengua mamlaka yake ya kiuchaguzi kuanzia leo na nimekwishampa barua yake..."

Alisema katibu huyo alikosa umakini kwa kile alichokifanya, na kwamba kwa mtu makini hawezi kuchukua karatasi za kupigia kura na kuzipeleka nyumbani au ofisini kwa mgombea kwa namna yoyote, kwani kila wilaya inapaswa kutengeneza karatasi hizo kwa gharama zake.

Aidha, alisema waligundua kuwa karatasi za jimbo la Newala vijijini ambako Maarifa anakogombea zilikuwa zimepungua kutoka karatsi 26,000 hadi 21,000.

Katibu aliyesimamishwa, Juma Namkoveka, alipotakiwa kuzungumzia suala hilo alikanusha na kukataa kuzungumza chochote.
NIPASHE ilimtafuta Maarifa ambaye ni katibu mwenezi wa CCM mkoa, na kukana kutambua taarifa hizo.


CHANZO: NIPASHE
 
Huku kata ya Luhundwa Simbachawene na diwani aliyeko madarakani wameiba fomu za kupigia kura kutoka kijiji cha ikuyu kupeleka vijiji wanapokubalika, hata hivyo baadhi ya matawi wanachama wamegoma kupiga kura hadi fomu 400 zilizoibwa zirudi

Hiyo ndio dawa kwa majizi ccm
 
Kwa hali niliyoiona kwa jimbo LA Segerea na jimbo LA Ukonga Dar es Salaam, CCM wana mpasuko mkubwa sana, wanapigana wenyewe kwa wenyewe mchana kweupe huku wengine wakitamka wazi wazi kuwa hiki chama bora kife, hivyo UKAWA wakiweka watu makini katika majimbo haya ushindi ni wao asubuhi na mapema...Ujio wa Lowasa upinzani umepelekea wengi CCM kujiamini kuwa kama haki haitendeki bora twende upinzani ili chama dola CCM Kijifie zake

Ccm ishakufa imebakia na kivuli chake tbc
 
Kagera tunako compile tutaweka hadharani, baada ya ngumi za karagwe. Wa kijani wanabamizana!!! Ujanja kuwekeana mamluki wa kuzomeana kwenye kampeni za ndani hata kurushiana mawe jukwaani mpk jana zilikuwepo mjini.
 
Bavicha nawataka mtulie. Mda wenu tulikaa kimya huu ni mda wetu wa maoni. Tulieni sindano iwaingie sawa sawa.

Sindano bila dawa haisaidii,nyie ma ccm ndio mtulie dawa ikolee maungoni ili kichaa chenu kipone
 
Back
Top Bottom