Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Kwa habari nilizozipata kutoka Bunda mjini ni kwamba Wasira anaenda kupita. Pia jimbo la Mtama Lindi mheshimiwa Nape Nnauye Mambo yamemunyookea...nitawaletea kura zilivyo kwa kila mgombwa soon.Kama una ukweli wa sehemu yako tuwekee..pia naambia naibu spika Mh Ndugai upepo upo vizuri kwake.
 
jimbo la kibakwe simbachawene anagawa fedha kama njugu Jana hapa kwenye kitongoji cha msangambuya Kata ya mtera mnapanga foleni unapewa 10000/_ unaambiwa chagua simbachawene kwakweli mkoa wa Dodoma takukuru imelala kuliko mkoa wowote walikuwa wameuchuna tu naamini hata wao walipoozwa kwani simbachawene na mawakala wake wamegawa fedha mchana kweupe.binafsi nimepewa 10000 na kula simpi.

Mkuu..simbachawene analindwa na system..takukuru hawana nguvu kabisa mpaka malalamiko ya hosea juu ya sheria ya takukuru ilekebishwe kujtoa kwa mwendesha mashtaka ya serikali
 
Babu masatu wanzita wasira bado "YUPO" tu hadi wakati wa utawala wa Lowasa -By mako nyerere
Mzee wa goli la puchu nae kaona ile nafasi yake ya uvuvuzela iko mashakani kaamua
aanze kutafuta hifadhi (kwa miaka 5 ) ili walau vugu vugu lipoe kwanza.
 
Last edited by a moderator:
Bavicha nawataka mtulie. Mda wenu tulikaa kimya huu ni mda wetu wa maoni. Tulieni sindano iwaingie sawa sawa.
 
Wakuu habari, leo ndio leo, ccm nchi nzima wanafanya kura za maoni ya kuwapitisha wagombea wake, ili waweze kupeperusha bendera ya ccm kwenye uchaguzi mkuu, kila mmoja hapo alipo ataweza kutupa matokeo ya jimboni kwake, ili tujue vigogo gani wamekatwa na nani ameingia na nani ametoka, mie nipo mkuranga hapa jimbo la adam malima, nitawapa matokeo, bado kura zinapigwa.

Kutoka Arusha ccm hali tete wafuasi wake wamejitokeza wachache sana na waandikishaji wanasinzia kwa kukosa watu source: radio sun rice 94.85 arusha
 
Bavicha nawataka mtulie. Mda wenu tulikaa kimya huu ni mda wetu wa maoni. Tulieni sindano iwaingie sawa sawa.
Sindano iwaingie nyie mnaopigana wenyewe Kwa wenyewe
 
Huku Serengeti mwamko ni mdogo wa wapiga kura, wagombea wawili wamesusa baada ya yule mwenzao (Kebwe) kugawa rushwa ovyo. Inasemekana zoezi linaweza simama.
 
Kuna mtu yupo moshi mjini ananipa taarifa kuwa Davis Mosha anagawa rushwa kama njugu
 
Kamanda Byabato nikumbushie mother wa ml kumi za mboga aniliniahidi kunipa binti yake ili nami nipatiemo kamugawo
 
Kamanda Byabato nikumbushie mother wa ml kumi za mboga aniliniahidi kunipa binti yake ili nami nipatiemo kamugawo maana amekuwa kimya sijui ndo nimetoswa
 
Kiongoz makini anajua idad ya wagonjwa wa serikali kuliko hata mimi.by anne makinda spika bunge la jamhuri ya wasikivu
 
Leo itakuwa mwanzo au mwisho wa historia ya Juliana Shonza na Mtela mwampamba ndani ya CCM. Vijana hawa walivamia chama chetu kwa pupa na kuwa karibu na viongozi wa juu wa chama kama wapiga propaganda lakini leo ndio mwanzo au mwisho wa safari yao ndani ya CCM. Unajua kwanini nasema hivyo?

1, Vijana wanawania kupeperusha bendara ya CCM katika nafasi za Udiwani, Hivyo wakishinda utakuwa mwanzo mzuri wa kujipenyeza ndani ya CCM na wakishindwa kwenye kura za maoni bhasi huo nao utakuwa mwisho wao ndani ya siasa za ccm

2. Vijana hawa walikuwa wanapewa shavu na kushikwa mkono na vigogo wa chama wa juu ambao nao hao vigogo wapo katika mchakato wa kura za maoni hivyo vigogo hao wakipata nafasi ya kupeperusha bendera ya ccm itakuwa ahueni kwa Mtela na Juliana lakini ikitokea vigogo hao wataangshwa kwenye kura za maoni za ubunge basi Mtela mwampamba na Juliana shonza watasahaulika kabisa katika siasa za ccm.

Ndugu wana JF tuwaombee makada hawa wa ccm wasipatwe na dhoruba la kisiasa katika mchakato wa kura za maoni leo hii

Tuwaombe ili iweje?
 
Tuwaombe ili iweje? Maana hata wakipataa badala ya kutetea wananchi wanatetea chama
 
Back
Top Bottom