Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Huku Serengeti mwamko ni mdogo wa wapiga kura, wagombea wawili wamesusa baada ya yule mwenzao (Kebwe) kugawa rushwa ovyo. Inasemekana zoezi linaweza simama.

Wacha yatowane ngeu
 
Leo itakuwa mwanzo au mwisho wa historia ya Juliana Shonza na Mtela mwampamba ndani ya CCM. Vijana hawa walivamia chama chetu kwa pupa na kuwa karibu na viongozi wa juu wa chama kama wapiga propaganda lakini leo ndio mwanzo au mwisho wa safari yao ndani ya CCM. Unajua kwanini nasema hivyo?

1, Vijana wanawania kupeperusha bendara ya CCM katika nafasi za Udiwani, Hivyo wakishinda utakuwa mwanzo mzuri wa kujipenyeza ndani ya CCM na wakishindwa kwenye kura za maoni bhasi huo nao utakuwa mwisho wao ndani ya siasa za ccm

2. Vijana hawa walikuwa wanapewa shavu na kushikwa mkono na vigogo wa chama wa juu ambao nao hao vigogo wapo katika mchakato wa kura za maoni hivyo vigogo hao wakipata nafasi ya kupeperusha bendera ya ccm itakuwa ahueni kwa Mtela na Juliana lakini ikitokea vigogo hao wataangshwa kwenye kura za maoni za ubunge basi Mtela mwampamba na Juliana shonza watasahaulika kabisa katika siasa za ccm.

Ndugu wana JF tuwaombee makada hawa wa ccm wasipatwe na dhoruba la kisiasa katika mchakato wa kura za maoni leo hii

Duuu from kugombea ubunge to udiwani
Hongera mwampamba kichwa kikubwa akili hamna
 
Kutoka Arusha ccm hali tete wafuasi wake wamejitokeza wachache sana na waandikishaji wanasinzia kwa kukosa watu source: radio sun rice 94.85 arusha

Hizo ni salaam tosha kwa magamba kuwa mwaka huu ni mwaka wa shiida
 
Kutoka Arusha ccm hali tete wafuasi wake wamejitokeza wachache sana na waandikishaji wanasinzia kwa kukosa watu source: radio sun rice 94.85 arusha

Niko hapa Majengo mapya Shy, nimepita kituo cha Shitta shule ya Msingi wasimamizi wanapapasana tu yaani watu hawapo kabisa! Magamba hapa mini wanapigwa tena!!! Safari hii ushindi wa kura 1 haukubaliki!
 
Mathias Byabato

Umefanya vyema kutuwekea live updates, kuna watia nia hapo sioni kama wana sifa...mfano Karamagi,Kamala alitutukana kuwa tule nkende kama wanatusumbua shambani.

Dr. Aman na Kagasheki nao wapumzishwe walau siasa za Bukoba zirudi katika mstari.

Nguvu ya Dr kamala ni kubwa kwa kipindi hiki.
 
Huku Bukoba Vijijini wagombea kwa CCM ni Karamagi na Rweikiza,kila mmoja kagawa manoti!mfano ktk kata moja ya Izimbya Karamagi amegawa 5000/= kwa kila mwananchi,ila ametoa angalizo kuwa kama akikatwa anahamia CHADEMA na kumfata swahiba wake el the don.

Kwa upande wa udiwani ktk kata ya Izimbya wako wagombea wanne,mmoja ni diwani anayetetea kitu chake,ila wote wametembeza karanga,na wote wameapiana kuwa iwapo mmoja wapo atakatwa basi wale wote watatu waliokatwa watampa kura mgombea wa chadema,wao na wafuasi wao,ahahaha
 
Mtu mmoja amekamatwa akiwa ktk harakati za kuingiza kura zilizotikiwa tayari kwenye box la Kura.

Katika kata hii ya Kaloleni wagombea wenye upinzani mkubwa ni Tojo na Seif Simba.

Kura zilizokamatwa zilitikiwa jina la Seif Simba.

Baada ya vurugu kutokea mjumbe wa halmashauri kuu Ndugu Godfrey Mwalusambo aliweza kumuokoa Mtu huyo na kumpeleka Polisi.
 
Back
Top Bottom