Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Elections 2015 Updates: Mchakato na Matokeo ya kura za maoni ya Ubunge CCM nchini kote

Hata angepita wala wanaMbozi wasingemchagua maana aliwasaliti kwa kupokea 50.0M na kuliuza jimbo mikononi mwa maccm. Matokeo ya usaliti ni mabaya sana.
 
Manyoni mashariki Daniel Mtuka ameshinda ila matokeo hayajatangazwa Mbunge aliyepita Chiligati kwa kushirikiana na Dr. Chaya wamehonga milioni 30 kwa viongozi wa wilaya ili wachakachue matokeo leo ndo yanaweza kutangazwa rasmi

Manyoni Magharibi kwa Lwanji vipi??
 
Aliyekuwa mbunge wa Tabora mjini na mwenyekiti wa timu maarufu ya mpira wa miguu nchini Bwana Aden Rage amekatwa katika kura za maoni CCM.
 
Mtela umetumia pesa nyingi sana uku mbozi ili upitishwe kwenye kura za maoni but umeangukia pua vibaya mno.

Umetumia milioni 6 umepata kura 3,
ccm ina wenyewe na wenyewe ndio sisi,hivi from nowhere utoke utokako uje kuivamia ccm ovyo,

Nasikia unalalamika kuchezewa rafu,sasa ndugu yangu wewe ulipokua cdm ulilamika and now unalia tena,ebu rudi shule kafundishe.

MILIONI 6=KURA 3

Wenzake huku dar mali kwa mali mshiko hautoki mpaka umeonyesha picha ya kura uliyopiga.hapana chezeaa wazee wa goli la mkono
 
Friends Of Hon.Membe wapeta nafasi za ubunge.

Katika hali ya ushindani wa makundi hasimu ya kambi za urais ndani ya Ccm hadi sasa kundi la Bernard Membe limeonesha kung'ara dhidi ya kundi la Edward Lowassa.

Ushindi mkubwa unaovunja rekodi waliopata marafiki na mashabiki wa Bernard Membe kwenye kura za maoni nafasi za ubunge umezidi kuwaumiza vichwa marafiki na wapambe wa Edward Lowassa walioangukia pua.

Baadhi ya makada waliopo kwenye kambi ya Bernard Membe wameangusha "mibuyu" iliyojimilikisha majimbo na vyeo ndani ya Ccm kwa kutumia hela chafu.

Mmoja wa wanachama wa Ccm alisema,"Bernard Membe kasaidia kusafisha uozo kwenye chama.Wachafu waliomuunga mkono Edward Lowassa waanguka na kuhamia upinzani na waliobaki wamekosa dira na sasa wanasubiri huruma ya Ccm.Bernard Membe anazungukwa na waadilifu.Waliomuunga mkono ilikuwa lazima washinde kutokana na ukweli kwamba wana dhamira ya kusaidia nchi kama aliyonayo Bernard Membe mwenyewe ambaye pamoja na kukosa urais ila bado anaheshimu maamuzi na kukiheshimu Ccm".

Baadhi ya makada wanaomsapoti Bernard Membe na walioangusha "mibuyu" ya ufisadi iliyokuwa na Edward Lowassa ni Bona Kaluwa aliyemwangusha Dk.Makongoro Mahanga,Dc Masala aliyemwangusha Mathias Chikawe,Aboubakar Asenga aliyemwangusha Abdul Mteketa,Mnec Miraji aliyemwangusha Pereira Ame Silima na Nape Nnauye aliyemwangusha Suleiman Mathew.

Kwa uchache tu hapa imedhihirika Bernard Membe ana nguvu kuliko Edward Lowassa.Mzizi wa fitina umekatwa na bado matokeo mengine yapo loading.....tutazidi kuwaletea!
 
Manyoni Magharibi kwa Lwanji vipi??

Manyoni magharibi Lwanji kapigwa chini kashika nafasi ya 3, Kaongoza jamaa mmoja wa kiwanda cha magogo na wa pili ni Dr. Mwanga. Ila jamaa wa magogo amekatwa live na TAKUKURU so kuna uwezekano wa kukatwa akipita Dr. Mwanga
 
  • Thanks
Reactions: BMW
wale jamaa wa escrow wote wameshinda uchaguzi ndani ya ccm
u
1. prof Anna Tibaijuka
2. Prof Sospeter Muhongo
3. William Ngeleja
4. Andrew Chenge
5.n.k

Makengeza si alijiapiza kutogombea tena? Nini kimetokea?
 
Namelok Sokoine ameshinda kura za maoni kupitia CCM hivyo anatajwa kuwa mrithi wa Lowassa jimbo la Monduli.
 
Rungwe.

Matokeo Tukuyu.jpg
 
Hela za nani zilikamatwa Dodoma, kweli CCM ni wababaishaji wanaoshindwa wote. Njoo UKAWA maana tumechoka kulea mafisadi.
 
Mwanzon mlibisha ila sasa mmekubali kua nape alkua anatumwa na membe kutukana lowasa...nape huyo huyo aliyeshkwa na takukuru akigawa rushwa ndye msafi...asenga Abubakari huyo huyo ambaye kilombero waarabu walkua wanamfadhili kugawa rushwa ad wenzake kukata rufaa. ..habari ya mjini ni UKAWA subirin tarehe 25 October mtajua
 
angekua ukawa sawa..alakini huko aliko amelamba garasha.
asubiri nafasi ya viti maalum
 
Mnachekelea kupasuka kwa chama?

Nilidhani mtu yeyote mwenye akili atathamini kura za kila mtu, mmoja mmoja bila kuangalia alikuwa kambi gani...

Wenye akili sasa hivi wanaongea kauli za "kuunganisha" sio za kuzomeana...
 
Manyoni magharibi Lwanji kapigwa chini kashika nafasi ya 3, Kaongoza jamaa mmoja wa kiwanda cha magogo na wa pili ni Dr. Mwanga. Ila jamaa wa magogo amekatwa live na TAKUKURU so kuna uwezekano wa kukatwa akipita Dr. Mwanga

Ahsante Kiongozi
 
Back
Top Bottom