Updates: Misri vs Tanzania [Michuano ya makundi kufuzu AFCON 2017]

Updates: Misri vs Tanzania [Michuano ya makundi kufuzu AFCON 2017]

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
73,773
Reaction score
102,126
egypt-vs-tanzania.jpg

Karibuni katika uzi huu tujumuike kwa ajili ya matukio na matokeo yatakayojiri katika pambano la soka baina ya Taifa Stars waliopo ugenini kupambana na Mafarao wa Misri.

Huu ni mchezo wa pili wa kundi G lenye timu za taifa za Nigeria, Chad, Tanzania na Misri. Pambano la kwanza katika kundi hili lilifanyika jana siku ya jumamosi huko Kaduna baina ya Nigeria na Chad, na Nigeria waliibuka na ushindi wa goli 2.

Mchezo huu utachezwa jijini Alexandria na utaanza majira ya saa 1 juu ya alama usiku kwa saa za Misri wakati huko Tanzania itakuwa ni saa 2 kamili usiku.

Misri 3 - 0 Tanzania
Fulltime


thumb



Tazama hapa Livestream:

Link 1
: http://www.yallakora-online.com/2015/06/egypt-vs-tanzania-live.html

Link 2: http://goatd.net/113771/watch-egypt-vs-tanzania

Link 3: http://www.yalla-shoot.com/live/5943/egypt-vs-tanzania.html

 
Naaam asante asante Watu8....mechi ni lini hii...
 
Last edited by a moderator:
Mechi ni usiku wa leo 2 usiku kwa masaa ya Tanzania mkuu...

Taarifa zote muhimu naendelea kuwajuza hapo juu....

asante kaka ngoja nifanye utaratibu wa kula mapema ili muda ukifika nisicheze mbali...who knows bana huenda leo mto akatiririka kuelekea mlimani!!!
 
Nidhamu ya mchezo ndio itakayo tuokoa, tunaweza fanya maajabu kwa waarabu leo hii
 
mkuu chanel gan watarusha hayo matangazo maana mi nina kig'amuzi startimes

channel gani itaonyesha hii mechi?

Hivi mechi hii itaonyeshwa vituo gani vya TV??

Hadi sasa nafahamu Bein Sport Channel 10 ndio watakaoonesha mechi hii...

Sina uhakika na ving'amuzi vya hapo Tanzania kama watakuwa wakionesha...

Muda ukikaribia nitaweka link ya internet kwa wale wenye uwezo wa kustream watazame kupitia link hiyo...

Kuna jamaa kanambia kuwa Azam TV wataonesha so walio na Azam Kaz kuenjoyyy

Kupitia ukurasa wa facebook wa AzamTv walibainisha kuwa hawataweza kuonesha hii mechi...

Sababu ilikuwa ni kukosa kibali, sina uhakika kama wamepata kibali sasa...

azamtv.JPG
 
Kwa tabia hii ya timu ya Taifa inacheza nje huku tv zote watanzania hatuna uhakika Wa kurushiwa mechi safari yetu bado ni ndefu sana kwasababu katika hari ya kawaida mpaka sahivi hata kabla hatujaangaika kuuliza tulitakiwa kuwa tushaambiwa ni kituo gani kinarusha ila mpaka sahivi hamna, watanzania uzalendo umeisha kabisa
 
Back
Top Bottom