Neta L zaja za aina
nne (4)
Hizi ni Hybrid SUV, zenye engine ya 1.5L na zinakuja na battery kuanzia 30 kWh (LFP), top speed 180 km/h, acc 0-100 km/h ndani ya 7.3 sec. Hii kwa EV mode itaenda range ya kilometa 220.
Nyingine itakuja na battery kubwa 40 kWh LFP battery, speed max ile ile 180 km/h, na acc ya 0-100 km/h ni 8.2 sec. Hii kwa EV mode itaenda mbali zaidi kilometa 310.
Neta wamesema kwa dk 19 utachaji kutika 30% to 80% kwa kutumia Level 3 DC fast charging.
Kuna kitu kinaitwa vehicle to load (V2L) hii tumeiona kwenye EV mfano Cybertruck, Hammer, Ford F150L etc kwamba gari inaweza kuact kama powerbank au power source ukatoa umeme kwa vifaa vya umeme mbalimbali, hii inatoa hadi 3.3, kW.
Kwa ndani kuna screen mbili za inch 15, moja kwaajili ya infotainment, na nyingine abiria wa mbele apate kuinjoy.
Pia kuna instrumental cluster kwaajili ya dereva ikiwa na Snapdragon 8155P SoC ambayo inaruhusu Digital Voice Assistant, OTA, etc.
Features nyingine ni hizi gari zina karibia color ambient 64 (hizi rangi za ndani yenye mood tofauti tofauti), 360 degree camera, powered seat (unaweza kupasha joto seat kwa mikoa ya baridi, zina pokea AC kwakua na ventilation, na massage), pia kuna friji, spika 16, kuna USB type C zenye 60W, dual climate zone na powered tailgate.
Kuhusu ADAS, Neta L inaendeshwa na Horizon Journey chip (wao wanaiita ivo sijui kwann), ikiwa na ultrasonic sensors 12, radars 5, camera 4 za pembeni na moja mbele.
Pia ADAS itakusaidia kwenye emergency braking, full speed adaptive cruise control, kusaidia gari kukaa kwenye mistari yake, kukuambia ukichepuka kwenye mistari, kukupa taarifa za gari ikikusogelea mbele na nyuma, kukuambia wapita njia na itaoark yenyewe gari (automatic parking) ukiamua.