Updates za Beijing Auto Show 2024 (25 April - 4 May)

Updates za Beijing Auto Show 2024 (25 April - 4 May)

Mchina ni hatari sana
Mchina hatari sana na bado China ni soko kubwa la magari kutoka nchi za Ulaya na Marekani.

Pamoja na China kuwa na brands nyingi sana, China-based auto companies bado zinashika soko la China kwa 60% ina maana 40% ni kutoka nje

Juzi kati CEO wa Mercedes Benz alikuwa analaumu nchi za Magharibi kuzuia EV kutoka China

Unajua kwa nini?

CEO anajua China nao wakilipiza inakula kwao maana China ni mojawapo ya soko kubwa la luxury autos kutoka Magharibi

Ni sawa na Apple mauzo makubwa ya simu za iPhone ni soko la China

Kwa sasa China ndio taifa linaloongoza duniani kwenye GDP per capita on Purchasing Power Parity. Kampuni zote zenye brand kubwa duniani zinajua umuhimu wa soko la China

Ndio maana hata makampuni ya West yameaingia joint ventures na ya China ili kulinda soko
 
Nasikia Bwana Elon Musk yupo China, kaenda kwa issues mbili, moja kuendesha gari ya Xiaomi (SU7) na pili, kuongea na serikali ya China kuhusu kuruhusiwa FSD - Supervised (Full Self Driving Supervised).
Katika game la Full Self Driving (FSD) Tesla ana kibarua kigumu sana kushindana na tech ya Huawei

Hii ni chuma ya Kichina inaitwa AITO wameingia mkataba na Huawei wa kutumia FSD tech yao

Inafanya parking bila msaada wa dereva na nyingine ikiwa road


 
Chery Omoda 7
Chery wamezindua Omoda 7 ambayo ni SUV kubwa wakisifia sana mambo matatu ambayo inayo:
  • dynamic,
  • avant-garde na
  • futuristic.
Msilale kwanza tuone sifa zake kama zitagusa izo pillars tatu.

Kwa muocnekano, ina swag za Harrier hizi latest model + Range Rover Velar flani.
Chery_Omoda_7-2.jpg
Chery_Omoda_7-3.jpg


Utamu upo ndani bwana.
Chery_Omoda_7-19.jpg

Steering wao Chery wamesema imekua inspired na controllers za PS5. Na seat za mbele pia zimekua inspired na gaming chairs.
Chery_Omoda_7-17.jpg


Kuna screen ya inch 15 ambayo unaweza icontrol kwa gesture, voice command au touch na abiria wa mbele anaweza kuislide ikasogea upande wake kabisa.

Pia kuna mahala pa kuweka perfumes, ambayo itakua integrated na air conditioning system ya gari lako (kama kwenye Mercedes Benz), speaker 14 za Sony, na kama haitoshi kuna engine noise cancelling system. Yaani ukiwa ndani kama upo makaburini.

Kuhusu ADAS, Kuna zaidi ya system 18 za driving assistance.

Kwenye engine, ni 1.5L 4 cylinders engine, ambayo ni PHEV. Battery peke yake (EV mode) linaweza kukupeleka kilometa 95 na wakati in Eco Mode (Hybrid Mode) gari una fuel consumption ya 22 km/L.
 
Xiaomi wao wanajisifu na SU7 yao.

Kwenye press conference, CEO wa Xiaomi Group kasema tokea wazindue SU7 watu walioweka non-refundable orders ni 75,723 na hadi kufika April wamesha safirisha kwenda kwa wateja magari 5,781.
SU7-Beijing-Auto-Show.jpg
Weixin-Image_20240425113831.jpg

Xiaomi SU7 ni gari kali kutoka China, zikiwa na models tatu. Basic, Pro na Max. Ukichaji full zina range kuanzia 700 km hadi 830 km.

Xiaomi_SU7_Max_001.jpg
Interior_of_of_Xiaomi_SU7_Max-20240413.jpg

Gari ni nzuri nje na ndani. Kama zilivyo simu nimeipenda option ya Power Save mode. Ukiweka on inamaanisha battery itadumu chaja zaidi, inapunguza matumizi yasio ya lazima kama kulimit AC, kupunguza ADAS, na comfort features, speed mwisho 90 kph etc.

Kwenye maonesho aya, Xiaomi ndio waru wamekaa foreni wakisubiri kuliangalia ili gari.
 
Bentley wazionesha Luxury cars zao Mulliners
beijing2024-1.jpg

Wamekuja na hizo Mulliners nne kwenye show.
Wamekuja na Batur, Continental GT Convertible S, na izi mbili Exclusive Ru Yi Collection na Koi Karp Collection.
beijing2024-continentalgtc-3.jpg
beijing2024-3.jpg

Kwa lugha nyepesi, hawajaja na gari mpya ata moja, ila ni za zamani sema izo gari una customize unavyotaka wewe mteja kuanzia rangi, ata ukitaka liandikwe jina lako kila pahala hadi kwenye rims. Wewe tu.
 
BYD Seagull
Gari dogo kutoka kwa BYD imekua upgraded. Hizi Seagull ndio gari ndogo kabisa kutoka kwa BYD zinashare platform na E series (mfano E2). Ni ndogo kidogo kwa Dolphin.
byd-seagull.jpg
byd-seagull (1).jpg
byd-seagull (2).jpg


Kilichompa umaarufu uyu gari sio muonekano, bali ni bei (value for money).

Kwa $10,000 tu unapata 74 hp kutoka kwa either 30 kWh (range = 305 km) au 38 kWh (range ni 405 km) LFP BYD Blade Battery.

Hii wakiitumia tumia itashuka bei hadi $4,000 hafu ndio wandava tunanunua.
 
Unaonekana muoga wa magari ya umeme. Sio mbaya, uwoga ni akili.

Basi wewe ishi na pure Hybrid. Mfano Aqua, Prius (isiwe Prius Prime), Honda Fit etc. Hizo ni zile zina Engine + Battery basi. Battery inachajiwa kwa regenerative braking system. Simple tu. Kama Dynamo ya Baiskeli. Hizi EV mode zinakuaga na range fupi, mfano unakuta Kilometa 5-8 tu.

Hizo PHEV ni Plug-in Hybrid. Izo zina Engine + Battery lakini Battery inachajiwa regenerative kama zingine Plus ukitaka unachomeka kwenye umeme. Hizi zinakuaga na battery kubwa na range inaweza kufika ata km 30.

Hapo nimeongelea magari yetu used Hybrid, mfano ukiwa Prius 2009 hadi 2014.
Shukran mkuu, woga nakuwa nao kwa sababu ya mazingira yetu.
Nilikuwa napitia gari za hybrid tofauti tofauti ingawa Mitsubishi Outlender imenikaa sana sasa nikakutana na Mitsubishi Outlender PHEV na Hybrid. Baada ya kuchungulia kwa Zakayo nikakuta kodi imeshuka imekuwa rafiki kidogo ukilinganisha na hapo awali ambapo ilikuwa ni 21+m kwa sasa inachezea 13-14+m. Kwa kweli natamani nijiweke kwenye hizo gari ndio maana natafuta taarifa za kutosha kabla ya kufanya maamuzi.
 
Shukran mkuu, woga nakuwa nao kwa sababu ya mazingira yetu.
Nilikuwa napitia gari za hybrid tofauti tofauti ingawa Mitsubishi Outlender imenikaa sana sasa nikakutana na Mitsubishi Outlender PHEV na Hybrid. Baada ya kuchungulia kwa Zakayo nikakuta kodi imeshuka imekuwa rafiki kidogo ukilinganisha na hapo awali ambapo ilikuwa ni 21+m kwa sasa inachezea 13-14+m. Kwa kweli natamani nijiweke kwenye hizo gari ndio maana natafuta taarifa za kutosha kabla ya kufanya maamuzi.
Okay, nitakuchekia specifically kwenye iyo gari.
 
Neta L zaja za aina nne (4)
Hizi ni Hybrid SUV, zenye engine ya 1.5L na zinakuja na battery kuanzia 30 kWh (LFP), top speed 180 km/h, acc 0-100 km/h ndani ya 7.3 sec. Hii kwa EV mode itaenda range ya kilometa 220.
2024_AutoChinaBeijing_Neta_L-1.jpg

Nyingine itakuja na battery kubwa 40 kWh LFP battery, speed max ile ile 180 km/h, na acc ya 0-100 km/h ni 8.2 sec. Hii kwa EV mode itaenda mbali zaidi kilometa 310.

Neta wamesema kwa dk 19 utachaji kutika 30% to 80% kwa kutumia Level 3 DC fast charging.
2024_AutoChinaBeijing_Neta_L-2.jpg

Kuna kitu kinaitwa vehicle to load (V2L) hii tumeiona kwenye EV mfano Cybertruck, Hammer, Ford F150L etc kwamba gari inaweza kuact kama powerbank au power source ukatoa umeme kwa vifaa vya umeme mbalimbali, hii inatoa hadi 3.3, kW.
2024_AutoChinaBeijing_Neta_L-10.jpg

Kwa ndani kuna screen mbili za inch 15, moja kwaajili ya infotainment, na nyingine abiria wa mbele apate kuinjoy.

Pia kuna instrumental cluster kwaajili ya dereva ikiwa na Snapdragon 8155P SoC ambayo inaruhusu Digital Voice Assistant, OTA, etc.

Features nyingine ni hizi gari zina karibia color ambient 64 (hizi rangi za ndani yenye mood tofauti tofauti), 360 degree camera, powered seat (unaweza kupasha joto seat kwa mikoa ya baridi, zina pokea AC kwakua na ventilation, na massage), pia kuna friji, spika 16, kuna USB type C zenye 60W, dual climate zone na powered tailgate.

Kuhusu ADAS, Neta L inaendeshwa na Horizon Journey chip (wao wanaiita ivo sijui kwann), ikiwa na ultrasonic sensors 12, radars 5, camera 4 za pembeni na moja mbele.

Pia ADAS itakusaidia kwenye emergency braking, full speed adaptive cruise control, kusaidia gari kukaa kwenye mistari yake, kukuambia ukichepuka kwenye mistari, kukupa taarifa za gari ikikusogelea mbele na nyuma, kukuambia wapita njia na itaoark yenyewe gari (automatic parking) ukiamua.
 
Waafrika tuna jifunza nini katika huu uzi ? Mfano tuchukulie nchi yetu Tanzania.

Ningependa kuona hili swali likijibiwa na watu humu.
Kwa upande wangu, naumia sana na "uwezo" wa kitechnolojia kwenye viwanda vyetu. Sisi tumekua end users tu.

Viwanda vyetu vinatengeneza bidhaa ndogo ndogo tu juice, etc.

Serikali ingeruhusu wawekezaji wa kigeni waje aisee.
 
Back
Top Bottom