Updates za Beijing Auto Show 2024 (25 April - 4 May)

Updates za Beijing Auto Show 2024 (25 April - 4 May)

East or west bado naamini Elon musk ata kuja pindua meza.
Japo zile cyber truck watu Wana zilalamikia sana
Elon kazingua. Alitakiwa aje na Tesla Model 2 ambayo ni cheap. Kasua sua miaka anasema ivo ivo.

Tesla ya bei ndogo kabisa unakuta $30k kwenda juu bado makodi hapo.

Angeweka gari ya $15k to $20k hapo
 
Elon kazingua. Alitakiwa aje na Tesla Model 2 ambayo ni cheap. Kasua sua miaka anasema ivo ivo.

Tesla ya bei ndogo kabisa unakuta $30k kwenda juu bado makodi hapo.

Angeweka gari ya $15k to $20k hapo
Mzee hivi vitu sio poa, hapo penyewe Ali ahidi semi lakini hakuna kitu.
Na Kuna wateja washa weka order kabisa 😂 😀
 
Kwa maelezo haya tupambane na hybrid.
Mkuu pia nilitaka kupata ufahamu kuhusu PHEV na Hybrid. Nimetafuta mitandaoni nipate uelewa kwa lugha rahisi lakini sijatosheka.
Kama mdau wa magari na kwa kuzingatia mazingira yetu ya kibongo na huu umeme wetu mwingi usio na ubora unashauri gari aina gani haitasumbua kati ya PHEV na Hybrid.
Unaonekana muoga wa magari ya umeme. Sio mbaya, uwoga ni akili.

Basi wewe ishi na pure Hybrid. Mfano Aqua, Prius (isiwe Prius Prime), Honda Fit etc. Hizo ni zile zina Engine + Battery basi. Battery inachajiwa kwa regenerative braking system. Simple tu. Kama Dynamo ya Baiskeli. Hizi EV mode zinakuaga na range fupi, mfano unakuta Kilometa 5-8 tu.

Hizo PHEV ni Plug-in Hybrid. Izo zina Engine + Battery lakini Battery inachajiwa regenerative kama zingine Plus ukitaka unachomeka kwenye umeme. Hizi zinakuaga na battery kubwa na range inaweza kufika ata km 30.

Hapo nimeongelea magari yetu used Hybrid, mfano ukiwa Prius 2009 hadi 2014.
 
Mzee hivi vitu sio poa, hapo penyewe Ali ahidi semi lakini hakuna kitu.
Na Kuna wateja washa weka order kabisa 😂 😀
Ana ahadi kama demu wa Kibongo:
1. Semi kasema hadi 2025
2. Full Self Driving alisema 2018/19 hadi leo vibali haijapata.
3. Autonomous Taxi (robotaxi) sound hadi leo.
4..
 
Haja mlinda mtu, shida ni kupata minimum cost katika uzalishaji.
At the same time Wana struggle kupata kitu sahihi.

NIme fatilia mahojiano ya tim cook, Ali kubali Hali bado ni ngumu.
Yah Hiyo ni moja ya Sababu cost ya uzalishaji USA iko juu Sana,
Ila hizi Gari za mchina, body za Gari zao Sio laini kama balon, Hata ikigongana na bicycle body inapinda.

Hapa Chima ni mjerumani mjerumani na Tesla sema hizo prices Zake sasa
 
Yah Hiyo ni moja ya Sababu cost ya uzalishaji USA iko juu Sana,
Ila hizi Gari za mchina, body za Gari zao Sio laini kama balon, Hata ikigongana na bicycle body inapinda.

Hapa Chima ni mjerumani mjerumani na Tesla sema hizo prices Zake sasa
Acha uwoga we chuma kama izo hazitaki shida. Haugongani na mtu. Boda akizingua sema ndi jau.
 
Ana ahadi kama demu wa Kibongo:
1. Semi kasema hadi 2025
2. Full Self Driving alisema 2018/19 hadi leo vibali haijapata.
3. Autonomous Taxi (robotaxi) sound hadi leo.
4..
Semi Tesla mbona kashatoa , Tena Pepsi America ndio wakwanza kununua.

Self driving western countries bado hawaamini AI.

Sema mchina si unajua yy Anajali kuuza Tu 😂
 
Sio mbaya kama Tesla price $80,000 alafu Kodi $7,000
Haa wapi. Nasemea used hapa 2018/2019 Model 3.

Beforward napata kwa $20-25k

Hapo ndio utata unakuja. Ninunue Tesla ya 2018 yenye Kilometa 100k.

images (8).jpeg
au ninunue Prius ya 2023 yenye 50 kilometa (sio 50k, 50 iyo ya kutoa Ubungo hadi Kibaha na kurudi),.
images (9).jpeg


Bei na ushuru sawa.
 
Ji Yue 07 (kutoka kwa Jidu Auto)
Hii kampuni Jidu Auto unaweza ukawa hauijui, ila ipo uko China. Ikiundwa 2021 ikiwa ni muungano wa kibiashara wa makampuni mawili Geely (hii kampuni ya magari) na Baidu (hii kampuninya technology wana search engine kubwa kama Google uko China na wana online market kubwa kama Alibaba).

Sorry nawachosha. Ila hizi joint venture mnagawana majukumu. Mfano, kwenye hizi gari Geely yeye anatengeneza gari (sijui tuseme hardware) hafu Baidu anatengeneza software (ADAS (Advanced Driving Assistant System) na Connectivity kama Bluetooth na WiFi etc)

Jidu Auto wana magari mawili hadi sasa. La kwanza mwaka jana Ji Yue 01 ambayo ni full EV SUV ila mwaka huu wametuletea Ji Yue 07 ambayo ni Premium Sedan.

View attachment 2974727
Kwa nje chuma ni ya moto. Ina muonekano mzuri, na ina cameras, radars na sensors za kutosha.

View attachment 2974728
Kwa ndani kuna screen ya inch 35 yenye 6K resolution na ina chip (SoC) ya Qualcomm Snapdragon 8295 na steering ya kishua ya Yoke aka Halfmoon.

Jiyue kwenye presentation yao pia wamesema wameanza kushirikiana na NVIDIA kutengeneza smartcars zenye FSD (Full Self Driving) capabilities.

Hii gari imepata tuzo mbili, IF Design Award na Red Dot Design Award.
Hii nimeikubali sana licha ya upya wao sokoni.
 
Semi Tesla mbona kashatoa , Tena Pepsi America ndio wakwanza kununua.

Self driving western countries bado hawaamini AI.

Sema mchina si unajua yy Anajali kuuza Tu 😂
Mzee semi Tesla zili achiwa chache mno, pepsi mwenyewe Ali agiza 100 toka 2017, aka pewa 36.

Shida hakuna battery za kutosha Mzee, na kasema mpaka 2025 labda.
 
Deepal G318 Zingatia double e sio Depal
Hii ni SUV ya kibabe wameifacelift wakiitangaza ata mwaka jana.
2024_Deepal_G318_(China)_front_view_01.png
Deepal_G318_002.jpg

2024_Deepal_G318_(China)_interior.png

Hii ni Hybrid lakini ina engine yenye 1.5L turbo, wenyewe wanasema hii ni kama generator (range extender).

Yaani wao Changan Automobile wanaamini kwamba, battery za kwenye gari ili 18.4 kWh au 35.1 kWh kutegemea na utakavonunua, zikishirikiana na motor, zinatosha kuendesha gari hii kama EV na engine itatumika tu kuongeza nguvu (kuchaji) battery ndio maana wao wanaiita generata.
 
Back
Top Bottom