Ji Yue 07 (kutoka kwa Jidu Auto)
Hii kampuni Jidu Auto unaweza ukawa hauijui, ila ipo uko China. Ikiundwa 2021 ikiwa ni muungano wa kibiashara wa makampuni mawili Geely (hii kampuni ya magari) na Baidu (hii kampuninya technology wana search engine kubwa kama Google uko China na wana online market kubwa kama Alibaba).
Sorry nawachosha. Ila hizi joint venture mnagawana majukumu. Mfano, kwenye hizi gari Geely yeye anatengeneza gari (sijui tuseme hardware) hafu Baidu anatengeneza software (
ADAS (Advanced Driving Assistant System) na Connectivity kama Bluetooth na WiFi etc)
Jidu Auto wana magari mawili hadi sasa. La kwanza mwaka jana Ji Yue 01 ambayo ni full EV SUV ila mwaka huu wametuletea Ji Yue 07 ambayo ni Premium Sedan.
View attachment 2974727
Kwa nje chuma ni ya moto. Ina muonekano mzuri, na ina cameras, radars na sensors za kutosha.
View attachment 2974728
Kwa ndani kuna screen ya inch 35 yenye 6K resolution na ina chip (SoC) ya Qualcomm Snapdragon 8295 na steering ya kishua ya Yoke aka Halfmoon.
Jiyue kwenye presentation yao pia wamesema wameanza kushirikiana na NVIDIA kutengeneza smartcars zenye FSD (Full Self Driving) capabilities.
Hii gari imepata tuzo mbili, IF Design Award na Red Dot Design Award.