Updates za Kimbunga Hidaya: Ulipo hali ikoje?

Updates za Kimbunga Hidaya: Ulipo hali ikoje?

Kwa hapa dar upepo ni mkali sana ulioambatana na baridi kali, ni mwendo wa kukoga mivumbi kipande hichi Cha Goba😅.

Tafadhali ni muhimu sana wakuu, tuepuke kukaa karibu na majengo mabovu ama vitu vya kuegeshwa. Unaweza kujikuta umebondwa na kitu kizito utosin!
 
Wakuu, ingekuwa vyema tukapata updates za kimbunga Hidaya kama kilivyotabiriwa hapa kwenye huu uzi.

Kwa wale walio mikoa ya pwani hali ikoje uliko? Ni tahadhari gani umechukua?

Kufuatilia hali ya kimbunga hiki mubashara bofya hapa: Live Weather Satellite Map | Zoom Earth

====

Pia soma: TMA: Uwepo wa kimbunga “Hidaya” katika bahari ya Hindi Mashariki mwa Pwani ya Mtwara
Dar Watu juzi mmetoka kwenye mafuriko,saiv mnapambana na kimbunga tena
taaabu juu ya taabu
Hakuna kupumzika
🙆😝
 
Mimi nimeshinda mahali hapa dar nikiwa ghorofa ya sita, upepo unaopiga ukiwa juu utadhani cioo vinataka kuvunjika

Ila ukiingia kwenye map unaona bado eneo kubwa ni baharini ndio linaonyesha kuwa na mgandamizo mkubwa

Screenshot_20240503_201940_Windyapp.jpg
 
Huu upepo unaanza kunitisha ...

Kigamboni kuna rasha rasha za upepo, kanakuja kaupepo na kukata, ukizidi zaidi ya hapa itakuwa CHANGAMOTO kubwa.
 
Back
Top Bottom