Updates za Mazao ya msimu wa 2022

Huu uwekezaji mkubwa..sana hongera sana..

#MaendeleoHayanaChama
 
Hata Iringa hali ya mahindi si nzuri saana...
 
Kwa sasa baadhi ya mazoa kwa SONGEA -Ruvuma yameanzwa kuvuna ikiwemo ufuta,soya , mpunga na mahindi.Kwa upande wa maharage kwa soko la sodeko yanaonekana yapo mengi na kufanya Bei Hadi wiki iliyopita unaweza pata kwa Tsh 1000
 
Kwa sasa baadhi ya mazoa kwa SONGEA -Ruvuma yameanzwa kuvuna ikiwemo ufuta,soya , mpunga na mahindi.Kwa upande wa maharage kwa soko la sodeko yanaonekana yapo mengi na kufanya Bei Hadi wiki iliyopita unaweza pata kwa Tsh 1000
Vipi ufuta umeanza na bei gani na mfumgo wa ununuzi Uko je? Au ndio mpaka upitie Amcos?
 
Afadhali ya nyie kama mtavuna kidogo wengne kwenye mpunga tumekula za kichwa mazima aisee... alaf ndio bei ya mpunga kubwa hatar.
Ngoja tukanunue tu alzeti ili tufidie hasara japo nao mwaka huu wameanza na bei kubwa balaa.

Alizeti unapanda shambani au mafuta ya kuuza mkuu...?
 
Morogoro, shamba ni la kwangu nilinunua takribani miaka takribani 15 iliyopita. Ila cheki na waliopo mikoa ya pwani along Rufiji River. Unaweza kubahatisha good deal. Na mimi nikisikia nitakucheki pia.

Hivi maeneo hayo kilimo cha alizeti kinakubali mkuu...?
 
Mwaka huu sikuwaza kuingia shambani kabisa,ila zile mvua za May nilizitumia ipasavyo nilipanda milimao size ya kati mpaka muda huu yote imeshika na naomba naomba mvua za Vuli zianze mapema ishamili zaidi ili mwakani ikimpendeza Mnyazi niipige kisu.
 
Wakulima wenzangu hifadhini mazao nawaambia hufadhini hata kama mna shida mvumilie kuanzia November tutatafutana. Nashukuru Mungu mahindi na maharage nimelima ekari 400 nabahatisha kidogo. Ila sitegemei kuuza mapema hata kilo moja. Umwagiliaji ndio ila bado ni gharama kubwa sana Kwa wa kulima wengi.
Tupambane wakulima achaneni na kina Diamond na Zuchu hao watatulipa kwenye sahani hawana ujanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…