Updates za Mazao ya msimu wa 2022

Updates za Mazao ya msimu wa 2022

Niko mbali na shamba hivyo picha wakati wa kumwagilia kwa sasa sina isipokuwa mfumo niliotumia wa umwagiliaji ni very simple. Umwagiliaji kwa sasa haifanyiki cause mahindi yamekomaa yakiendelea kukauka tayari kwa kuvunwa. Shamba linapakana na mto mkubwa usiokauka mwaka mzima hivyo nachofanya ni kulekeza pipes mtoni na kuchukua maji na kumwagilia kwa mashine inyorusha juu na kufanya mazao kama yananyeshewa mvua. Mashine hii kwa Tanzania inauzwa around milioni 40. Haina complication. Ni simple kabisa.
Huu uwekezaji mkubwa..sana hongera sana..

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa mkoa wa Iringa hali ya mavuno hasa ya mahindi nakadiria kuwa 70%. Kuna maeneo mavuno ni mazuri na mengine ni wastani. Ila kwa zao la Alizeti halijaathirika na upungufu wa mvua uliojitokeza.

Kwa mkoa wa Mbeya kuna mtu kaniambia hali si nzuri sana kwa baadhi ya maeneo japo watavuna.
Hata Iringa hali ya mahindi si nzuri saana...
 
Kwa sasa baadhi ya mazoa kwa SONGEA -Ruvuma yameanzwa kuvuna ikiwemo ufuta,soya , mpunga na mahindi.Kwa upande wa maharage kwa soko la sodeko yanaonekana yapo mengi na kufanya Bei Hadi wiki iliyopita unaweza pata kwa Tsh 1000
 
Kwa sasa baadhi ya mazoa kwa SONGEA -Ruvuma yameanzwa kuvuna ikiwemo ufuta,soya , mpunga na mahindi.Kwa upande wa maharage kwa soko la sodeko yanaonekana yapo mengi na kufanya Bei Hadi wiki iliyopita unaweza pata kwa Tsh 1000
Vipi ufuta umeanza na bei gani na mfumgo wa ununuzi Uko je? Au ndio mpaka upitie Amcos?
 
Afadhali ya nyie kama mtavuna kidogo wengne kwenye mpunga tumekula za kichwa mazima aisee... alaf ndio bei ya mpunga kubwa hatar.
Ngoja tukanunue tu alzeti ili tufidie hasara japo nao mwaka huu wameanza na bei kubwa balaa.

Alizeti unapanda shambani au mafuta ya kuuza mkuu...?
 
Morogoro, shamba ni la kwangu nilinunua takribani miaka takribani 15 iliyopita. Ila cheki na waliopo mikoa ya pwani along Rufiji River. Unaweza kubahatisha good deal. Na mimi nikisikia nitakucheki pia.

Hivi maeneo hayo kilimo cha alizeti kinakubali mkuu...?
 
Habari wakulima na wafugaji wenzangu, kutokana na hali ya hewa kubadilika na mvua kuwa chache nimeona ni bora tupeane updates za maendeleo ya Mazao hapa nchini ili watu wajipange kwa kununua Mazao sehemu yatakapopatikana kwa wingi

Huku maeneo ya Tanga hasa maeneo ya Muheza naona kama mvua ishakimbia na Mahindi yameachwa stages ambayo si Rafiki, yameachwa mengi yakiwa na umri wa mwezi mmoja na wakulima wengi wamepanda Mbegu za kienyeji ambazo zinachukua mpaka siku 120 mpaka kukomaa

Vip eneo lako Mazao yanaendaje?
Mwaka huu sikuwaza kuingia shambani kabisa,ila zile mvua za May nilizitumia ipasavyo nilipanda milimao size ya kati mpaka muda huu yote imeshika na naomba naomba mvua za Vuli zianze mapema ishamili zaidi ili mwakani ikimpendeza Mnyazi niipige kisu.
 
Wakulima wenzangu hifadhini mazao nawaambia hufadhini hata kama mna shida mvumilie kuanzia November tutatafutana. Nashukuru Mungu mahindi na maharage nimelima ekari 400 nabahatisha kidogo. Ila sitegemei kuuza mapema hata kilo moja. Umwagiliaji ndio ila bado ni gharama kubwa sana Kwa wa kulima wengi.
Tupambane wakulima achaneni na kina Diamond na Zuchu hao watatulipa kwenye sahani hawana ujanja.
 
Back
Top Bottom