Huna kazi ya kufanya?Yamkini wachambuzi wa soka wameligundua hilo mapema lakini wanaogopa kusema.
Kinachofanywa na Rais dhidi ya Simba na yanga ni kama kulea watoto wawili wa kufikia kinafiki!
Mtoto wa kambo (simba ya champion) akiwa darasa la juu kabisa la ushindani (champion) anapewa motisha sawa sawa na mtoto wa chekechea (yanga ya shirikisho)
Wanasaikolojia kwenye hili watanielewa vizuri! MOTISHA Ya Rais kwenye timu hizi mbili ilichangia sana kushusha Saikolojia ya Simba na kupandisha Saikolojia ya Yanga!
Yanga walijikuta wanapata nguvu na ari ya kufanya vizuri hasa Walipocheza baada ya simba! (Yaani Simba akicheza Leo, basi iliwapa hamasa wao kucheza vizuri kesho yake)
Niwape mfano mwingine mtanielewa vizuri! Washindani wa Movie bongo muvie walivyokuwa wanashindana na KANUMBA tuliona ubora wao, lakini baada ya kanumba kufariki nao walifariki kifikra! Hii ni ishara walivuma kwa mgongo wa kanumba!
Kwanini nasema yanga wanaprndelewa?
1. Motisha ya goli la mama haikuzingatia hadhi ya ligi za timu hizo mbili hivyo mama kachangia kuangusha simba ( strategic destruction theory)
2. Kama mlichunguza vizuri goli la mama alibadisha dau kuwa 10mil baada ya kuona simba kapangwa na Wydad Casablanca kwao hivyo goli la mama lililenga kuwainua Yanga wapate kicheko! kwa vile MUNGU si athuman wala babu Kaju, Simba walifunga magoli ya penati ..ambayo mama aliyakataa kwamba yapo kinyume na motisha hivyo hakutoa pesa yoyote kwasababu goli ni kinyume ya mkataba!
3. Yanga katika mechi yake ya nyumbani na USM Alger baada ya simba kutolewa goli la mama lilipanda hadi 20m kwa sharti liwe ni goli la ushindi! Na alitoa hiyo kwasababu alimamini Yanga wakiwa nyumbani lazima wangepata ushindi! Bahati mabaya Yanga ilipigwa na USM hivyo hawakustahili kupatiwa pesa ya mama! Lakini ajabu Pesa ya goli la mama ililipwa! Swali mbona simba haikupewa goli la mama hata kama imefunga inje ya mkataba?
4. Mama yetu huyu amewapa yanga ndege na posho kusafiri kwenda kwenye mechi ya marudiano na USM ALGER! Hili tunashukuru kwamba Yanga inawakilisha Taifa! Lakini bahati mbaya yanga inakwenda kupasuka vipande vipande!
Kuwapa ndege Yanga kitaifa kunaishitua pia timu pinzani kitaifa!
Yanga alitakiwa kwenda kinyonge then akacheze kitaifa kama mbinu ya kuwapumbaza waione kibonde!
Bahati mbaya hilo halijazingatiwa kwa kutokana na mahaba mazito ya mama hivyo tumekusanya mayai yote kwenye kapu moja la mahaba!
Katika ulimwengu wa Roho pia anaepatiwa nguvu ya ushindi ni yule ambaye hamtegemei mwanadamu!
Yanga ikishinda atapongezwa Mama na serikali halafu Mungu atakuwa wa tatu!
Kuna elimu moja ya kiroho inasema (Mungu huchomoza juu ya Miungu ili asitukuzwe kiungu - t he superior power of the universe)
Hivyo yanga inakwenda kupasuka pasuka vipande vipande
Wanakwenda kwa shangwe watarudi kinyonge!
Kenge wewe