Upendo Nkone: Mayai ya kisasa yanaongeza matiti kwa wanaume

Upendo Nkone: Mayai ya kisasa yanaongeza matiti kwa wanaume

Wakaka kina boniyai wanatoa povu balaa coz washaota manyonyo makubwa na hawakujua yaliwapataje, sasa Upendo kaweka wazi kisababishi weeeh hahahaaa boniyai wametoa povu lile la omo 😂😂😂
Nimecheka hadi bas, 😂😂😂😂
 
Kwani mwanaume akiwa na matiti na anaendelea na kazi zake vizuri na mayai ananunua kwa hela yake we unaumia wapi?
Kazi ya matiti ni kunyonyesha, mwanaume mwenye matiti makubwa hana tofauti na mwanamke, ni aibu kwa mwanaume kukuza matiti
 
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Upendo Nkone, ametoa angalizo kwa wazazi kuhusu ulaji wa mayai ya kuku wa kisasa kwa kudai kuwa yanaongeza ukuaji wa matiti kwa watoto wa kiume.

Muimbaji huyo aliandika ujumbe huo kupitia akaunti yake ya Instagram akisema..''Jamani wazazi natoa ushauri tuu kwamba, tusiruhusu watoto wa kiume kula mayai ya kisasa, yanaleta manyonyo kwa wanaume. Hayo madawa nadhani yanayotumika, kama ni chips kula kavu au ule tuu mayai ya kienyejii, wanaume hili ni la muhimu sana"

Alimalizia kwa kusema "ila mnisamehe kama nitakuwa nimekosea au nimewaudhii️. Waachieni wanawake wale japo kwa kiasi pia. Nashindwa namna ya kuliwasilisha vizuri hilii ila mnisamehe wanaume''

Chanzo: Gazeti la Pambazuko.
Hilo jinga lifanye mambo inayoyaweza. Ye ni daktari wa nini
 
Back
Top Bottom