The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Kama mada inavyojieleza hapo juu, nchi yetu imejaaliwa kuwa na kila fursa ya kuifanya iongoze uchumi wa Afrika Mashariki na hata Afrika nzima. Lakini tatizo kubwa sana tulilo nalo kama nchi ni mfumo wetu wa uongozi.
Mfumo wa uongozi wa nchi tulionao, hautoi nafasi ya watu kuwa huru na mawazo na upeo wao wa kusimamia mambo kwa kadri walivyojaaliwa na Mungu, bali husalimisha kila kitu mikononi mwa chama.
Na hii inatokana na katiba yetu kutoa mamlaka makubwa sana Kwa vyama vya siasakuhodhi nafasi za kuongoza.
Tumeshuhudia mara nyingi mtu akitofautiana na chama chake hata kama mawazo yake ni ya kujenga nakusaidia mwananchi, atapata misukosuko na kutshwa hatimae kunyamazishwa.
Yaani hata kama kungekuwa na mpango mbovu kiasa gani, ilimradi unaratibiwa na chama basi utalazimika kuupigia debe Ili kulinda mapenzi Yako kwa chama.