ACT ni Zito Kabwe, na chama hiki ni matunda ya msuguano wa Zito dhidi ya chama chake cdm, kutokana na kutumiwa na ccm. Chama hiki kilikuwa na mkono wa kundi la JK, akiwemo Membe, Mwigulu, January, Nape nk, lengo la kuanzishwa chama hiki ilikuwa kiwe back up ya kuilinda ccm dhidi ya cdm. Fedha na mikakati yote ya chama hiki alipewa Zito na hilo kundi la JK. Rejea uchaguzi wa 2015 ACT iliweza kusimamisha wagombea karibu nchi nzima, huku kukiwa kichanga kabisa bila support kubwa ya watu.
Uchaguzi wa 2015 ndio ulimaliza kabisa mipango ya ACT baada ya Magufuli kuwa rais. Magufuli alipoingia madarakani alitupilia mbali mipango, mienendo na kundi lote la JK, ikiwemo support kwa ACT. Hili lilikuwa pigo kubwa sana kwa ACT kwani ilitegemea zaidi support ya ccm kufanya siasa za upinzani, kwa lengo la kuhakikisha ccm haizidiwi na cdm. Lakini Magufuli aliweza kutumia madaraka vibaya kuihujumu cdm kuliko kutumia mbinu za kisiasa kupambana na cdm, hivyo hakuwa na uhitaji wa hiyo ACT hasa ukizingatia Magufuli hakutaka mambo ya JK kabisa na kundi lake.
Hali hii ilimfanya Zito awe mkosoaji mkubwa wa Magufuli, kwani ni kama aliharibu matarajio yote ya kuikuza ACT, ifahamike Zito anajiona ni superior kuliko Mbowe, hivyo alitarajia kumkomoa Mbowe iwapo ACT ingefanikiwa kuwa mbadala wa CDM kwenye siasa za upinzani, hasa huku Bara. Ni bahati tu uchaguzi wa 2020 ACT ilifaidika na mgogoro wa CUF baada ya Maalim Seif kuondoka na wafuasi wake na kutua ACT. Lakini bahati hiyo inaifanya ACT kuwa na nguvu huko Zanzibar hasa Pemba, bali sio kwa ushawishi wa Zito.
Kwa sasa Zito ana kazi ya kuijenga ACT huku Bara, hivyo hana namna zaidi ya kutumia ushawishi wa JK kwa mama Samia, ili warudishwe kwenye upinzani unaotakiwa na ccm. Hivyo Zito anawajibika kwenda kwa tahadhari ili kumrahisishia JK kumshawishi mama Samia awabebe ACT, tatizo ni moja kwenye mazingira haya, mama Samia urais na uenyekiti wake wa ccm ni wa kurithi, na hasa ukizingatia ni Mzanzibari anajikuta hana nguvu ya maamuzi hayo. Hata ushiriki wa Zito kwenye hizi chaguzi za marudio, ni kujaribu kusaka huruma ya rais Samia kwa chama chake, lakini matokeo ya uchaguzi aliyoyapata kwenye chaguzi alizojichanganya kushiriki huku Bara, zimeishia kumfubaza kisiasa. Kwa sasa Zito yuko njia panda, na iwapo uchaguzi ujao kama hakutakuwa na mabadiliko ya kisiasa yatakayofadisha chama chake, namuona Zito kwa aibu akirudi Cdm, au aamue kukata mzizi wa fitina kwa kujiunga na ccm mshirika wake wa muda mrefu kwa kificho, ili akajaribu bahati yake. Sioni Zito akiendelea kuvumilia kuishi bila hata ya kuwa waziri, kwani anajiamini kutokana na elimu yake na huku umri wake ukienda.
Cc:
Zito, Act Wazalendo, bams, Paskali Mayalla, Salary slip, sky eclat, Kiranga, joka kuu, mag3, nguruvi3