Unasema umeombewa ila tatizo halijaisha basi habari njema inakufikia siku ya leo, wiki iliyopita nikiwa natembea nyikani nikasikia sauti ikisema, "Jipu tazama mbele yako kuna nini?" Nikajibu fimbo, sauti ikasema, "iokote fimbo iyo, nawe utaenda nayo popote ukihubiri neno langu, na kwa fimbo hii wote utakao wachapa viboko kwa fimbo hii watapata wokovu."
Leo ni siku ya sita watu wanapata wokovu, nimechapa viboko vya upako wezi, majambazi, walevi, wazinzi, wagonjwa na wote wamepata uponyaji. Nakusihi njoo na wewe nikutandike viboko vitano vya upako tatizo lako litaisha.