Upigaji, utapeli, uliojifichika kwenye kofia ya Kampuni Binafsi za Ulinzi

Taasisi yoyote nchini ina vimelea vya wizi na upigaji.

Ila ukiona taasisi yoyote imehusisha wizara ya mambo ya ndani,kama unaweza ikimbie kabisa,huko kuna watu ni matapeli na serikali haijawahi kujua nini cha kuwafanya.

Taasisi zote za ulinzi ni za wastaafu wa ngazi za juu polisi,wachache sana jeshini,utapeli kwao ni jambo lili damuni,hawajui dhambi wala hawana huruma.
 
Kampuni za Ulinzi ni Tatu tu...Hizo nyingine zote ni wajasiriamali wa mambo ya Ulinzi na utapeli tu.
 
Maslahi sio kwa walinzi tu bali ni kwa kada zote za ajira yena hali mbaya kwenye ajira za sekta binafsi wanatumia mwanya wa ukosefu wa ajira kutesa wenye ajira
 
Ni uchunguzi wa miezi zaidi ya mitatu kwa nyakati tofauti kwenye maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam na mikoa jirani, ambapo safari yangu inakutana na Walinzi wa kampuni binafsi wakitoa kauli zenye kuashiria uwepo wa mazingira ya upigaji, utapeli na usanii.

Nini kinabainika?
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la kampuni binafsi za ulinzi nchini Tanzania, kampuni hizo kwa mujibu wa taratibu usajiliwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kwenye Idara ya Jeshi la Polisi.

Kampuni hizo licha ya kuwa na tija kwa namna moja hama nyingine, lakini zimekuwa kati ya maeneo ambayo yamejaa utapeli kwa Wafanyakazi wengi ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu ya kiulinzi.

Katika kuzungumza na walinzi wengi wanadai kukumbana na mazingira yenye viashiria vya upigaji.

Ifahamike kwamba baadhi ya makampuni binafsi ya ulinzi yanasaini mikataba moja kwa moja na taasisi, kampuni au Mtu binafsi anayehitaji huduma ya ulinzi.

Mfano, kumekuwepo na mikataba ambayo wamiliki wa kampuni wanaingia na kampuni kuwalipa walinzi kiasi cha fedha Tsh. 700,000/=, lakini kiasi kinachomfikia mlinzi ni Tsh. 250,000/= hadi 150, 000 kwa Mwezi wengine wanapata hadi Tsh. 120,000 kulingana na wenye kampuni watakavyoamua.

Wamiliki ambao mikataba imekuwa ikiwabana mfano kuwalipa walinzi Tsh. 400,000/= kwa Mwezi, wamekuwa wakitumia mbinu ya kutengeneza makosa kwa mlinzi husika na mpaka ifikie kiwango wanachokusudia kumpa licha ya kuwasilisha nyaraka zinayoonesha mlinzi alipatiwa pesa zote.

Mmoja kati ya waliokutana na suala hili anaeleza "Mimi kwa Mwezi kampuni yangu inanilipa Tsh. 300,000 lakini ni ngumu kupata hizo hela, naishia kupata 130,000/=, wanachofanya wanakuja kwa kushtukiza wakikuta upo lindo umeweka rungu chini wanakukata 30,000 au ukitoa tu kofia kichwani wanakukata mpaka waone imefikia pesa wanayoitaka ambayo ni Tsh.180,000/= au 150,000."

Mlinzi huyo anayetekeleza jukumu lake kwenye ofisi moja iliyopo Mikocheni anadai suala hilo linawakumba walinzi wengi kwenye baadhi ya makampuni, ambapo kufuatia hali hiyo anadai amezoea mshahara wake ni Tsh. 130,000 licha ya nyaraka kuonesha anapata laki tatu.

Mazingira ya umiliki wa kampuni, tenda kwenye Ofisi za Umma
Kutokana na utaratibu wa muongozo uliopo kupata kibali cha kampuni binafsi ya ulinzi, kutoka Jeshi la Polisi imekuwa ikisababisha kampuni nyingi kumilikiwa na Wastaafu kwenye vyombo vya ulinzi na usalama au vigogo waliopo karibu na mfumo wa utawala (Serikali).

Jambo hilo linatajwa kuwa licha ya utaratibu wa wazi kuwepo lakini sio rahisi kwa Mtu mwenye sifa ambazo uainishwa katika muongozo husika kuanzisha kampuni ya ulinzi, baadhi ya vyanzo vinadai ili kufanikisha vibali stahiki uhitajika 'connection' kama kukunjua mkono.

Kutokana na mazingira hayo imekuwa ikihisiwa hicho ndicho chanzo cha makampuni mengi kutowajibika kwenye masuala mbalimbali hasa yanayogusa haki na maslahi ya Wafanyakazi kwa sababu ya ukaribu uliopo baina ya wamiliki na waliopewa dhamana ya kuwajibisha mambo yanapokuwa kinyume.

'Connection' hii imekuwa ikitumika pia katika kutoa tenda kwenye taasisi za umma bila mchakato wa kiushindani au ikitokea mchakato huo umehusika basi rushwa imekuwa nyuma ya pazia kupata tenda hizo.

Mfano zipo ofisi nyingi za Serikali hata ambazo ni nyeti kuna kampuni zimepewa tenda lakini walinzi wengi uwezo wao ni mdogo na hawana hadhi ya kuhudumu kwenye ofisi nyeti za umma.

Walinzi kadhaa wanadai mishahara sio ya kuridhisha licha ya kampuni husika kuingia mikataba inayowanufaisha zaidi wao binafsi.

Hali hii inaweza kuleta athari kubwa endapo itaendelea, ikiwemo walinzi hao kuhusika kwenye mipango uovu, mfano wizi na unyanganyi, na tayari tuhuma za aina zimekuwepo tayari ambapo baadhi ya walinzi wakiwa kwenye majukumu yao kudaiwa kujihusisha na matukio ya uovu.

'Kuna wimbi la walinzi ambao hawana weledi'
Licha ya suala la maslahi ya walinzi lakini kuna jambo lingine ambalo nimelifuatilia na kubaini sio rafiki, zamani walinzi wengi waliokuwa wanaajiriwa kwenye kampuni hizi walikuwa angalau wana A, B, C za ulinzi lakini kwa sasa makampuni mengi yanawatumia watu wengi ambao hawajapitia hata mafunzo ya Mgambo wala hawana ujuzi wa ulinzi.

Wafanyakazi wengi kutokuwa na mikataba
Nimebaini wafanyakazi wengi hawana mikataba na hili limechangia kufanikisha upigaji pia kutoa vibarua kwa Watu ambao hawana sifa.

Licha ya sekta hii kuwa nyeti kwa kugusa usalama wa raia na mali zao lakini bado wafanyakazi wengi wanafanya kazi katika mazingira magumu ambayo hayatoi matumaini yao ya kesho, ni wachache kati ya wengi ambao wanawekewa pesa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kwenye hili uchunguzi zaidi unahitajika
Inasemekana kutokana na kuaminika kwa kiwango fulani kwa Kampuni ya ulinzi ya Suma-JKT ikilinganishwa na kampuni nyingi hasa za ndani, inaelezwa kumekuwepo na Suma-JKT kivuli ndani ya Suma-JKT halisi.

Ni kwamba kuna watu wamekuwa wakipewa tenda kama Suma-JKT licha ya kuwa ni kampuni nyingine, jambo hilo limedaiwa kuwa ni ngumu kubainika kwa sababu hata walinzi upewa sare zinazofanania na Suma-JKT halisi.

Jambo hilo linaacha maswali lakini ni vyema nilifikishe hapa jukwaani ili wahusika walifanyie kazi zaidi maana nimekosa muda wa kulichunguza kwa kwa kina.

Baadhi ya makampuni yakipata tenda wahuka (wahitaji) wakahitaji huduma ya ulinzi wa Suma-JKT dili halikwami badala yake mazingira yanatengezwa kufanikisha mchongo kwa kutumia Suma-JKT kivuli.

Nashauri nini?
Miezi kadhaa iliyopita niliona Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora wametoa taarifa ya kufanya uchunguzi kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za walinzi kwenye kampuni binafsi, lakini mpaka sasa sijasikia ripoti ya uchunguzi wao ikitolewa hadharani au kwenye vyombo vya habari, sijui labda wenzangu mmesikia?

Ni vyema muongozo wa kuanzisha kampuni binafsi ukaboreshwa ili kuepuka mazingira sawa katika kuanzisha kampuni hizo, lakini pia kufanya tathimini ya kampuni zilizopo mpaka sasa kubaini kama zinatimiza mashariti ya taratibu za kumungozo.

Zoezi la tathimini hiyo suala la maslahi kwa wafanyakazi lipewe kipaumbele pamoja na wimbi la kuongezeka kwa kampuni hizo pia uweledi wa walinzi kulingana sifa husika.

================
Lilivyokuwa andiko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
View attachment 3003443
View attachment 3003444
Kuna kampuni X hao hata likizo mlinzi hapati wanalazimisha kuuza likizo zao.Mshahara unaingia tarehe 10 Walinzi wanatishia kulalamika tu hamna wa kuwasaidia. Hizo kampuni za ulinzi za wazawa zina shida sana Bora kidogo hizi wa watu wa nj'e
 
Bear it in your mind. Let it sink deeply into core of your being at every part of your body,fiber, DNA, hair,nails,ears,eyes,toes,fingers etc as long they're part of you who are.

THIS IS WORLD OF ONE DOG EATS ANOTHER DOG WETHER YOU LIKE/ACCEPT OR NOT LOOK FROM RELIGION, POLITICAL , GOOD SAMARITAN, PHARMACISTS ETC ARE EATING YOU.
IT'S UP TO YOU WAKE UP AND SEE BY BRAIN EYES TO SEE WHERE/HOW ARE EATING AND ESCAPE BEING GAZELLE AND BECOME CHEETAH. IT'S HARD TO SHIFT FROM PREY TO PREDATOR GROUP IT'S POSSIBLE BUT IT'S HARD BOTH MENTALLY, EMOTIONALLY, SPIRITUALLY AND PHYSICALLY.

NONE LOVE/LIKE YOU , NOTHING IS FREE EVEN THESE SOCIAL MEDIA IS EATING YOU BUT YOU DON'T KNOW HOW THEY'RE EATING YOU. SOMEONE IS MAKING MONEY AS LONG YOU'RE SCROLLING ON REEL,TIKTKOT,JF, ETC.
IF YOU DON'T PAY FOR THEM THEN THEY'RE PAYING TO GET YOU.
 
Kuna kampuni X hao hata likizo mlinzi hapati wanalazimisha kuuza likizo zao.Mshahara unaingia tarehe 10 Walinzi wanatishia kulalamika tu hamna wa kuwasaidia. Hizo kampuni za ulinzi za wazawa zina shida sana Bora kidogo hizi wa watu wa nj'e
umeambiwa kampuni za ulinzi zipo 3 tuu hao wengine wote ni wapigajii..!
 
Nashangaa Sana Kuna tapeli moja sugu mjini hapa eti nalo Lina kampuni ya Ulinzi haya ni maajabu ya dunia
 
Ungewapa akili ukawakomboa kutoka hapo walipo. Shukuru nature imekupa jicho lenye nguvu Kali la kichwani mwenzako akaishia hapo so uungwana ungewaonyesha waone wasichokiona Ila wewe unakiona ama unafurahi wanayopitia Bali wewe unajipa sifa kwa jinsi ulivyo.
kuna ile akili yakawaida tuu binadamu timamu inatakiwa uwe nayo.haihitaji kufundishwa.

ukishaona mtu miezi miwlili hakulipi mshahara wako huyo mkimbie tafuta sehemu nyingine siohadi uambiwe
 
Ni uchunguzi wa miezi zaidi ya mitatu kwa nyakati tofauti kwenye maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam na mikoa jirani, ambapo safari yangu inakutana na Walinzi wa kampuni binafsi wakitoa kauli zenye kuashiria uwepo wa mazingira ya upigaji, utapeli na usanii.

Nini kinabainika?
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la kampuni binafsi za ulinzi nchini Tanzania, kampuni hizo kwa mujibu wa taratibu usajiliwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kwenye Idara ya Jeshi la Polisi.

Kampuni hizo licha ya kuwa na tija kwa namna moja hama nyingine, lakini zimekuwa kati ya maeneo ambayo yamejaa utapeli kwa Wafanyakazi wengi ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu ya kiulinzi.

Katika kuzungumza na walinzi wengi wanadai kukumbana na mazingira yenye viashiria vya upigaji.

Ifahamike kwamba baadhi ya makampuni binafsi ya ulinzi yanasaini mikataba moja kwa moja na taasisi, kampuni au Mtu binafsi anayehitaji huduma ya ulinzi.

Mfano, kumekuwepo na mikataba ambayo wamiliki wa kampuni wanaingia na kampuni kuwalipa walinzi kiasi cha fedha Tsh. 700,000/=, lakini kiasi kinachomfikia mlinzi ni Tsh. 250,000/= hadi 150, 000 kwa Mwezi wengine wanapata hadi Tsh. 120,000 kulingana na wenye kampuni watakavyoamua.

Wamiliki ambao mikataba imekuwa ikiwabana mfano kuwalipa walinzi Tsh. 400,000/= kwa Mwezi, wamekuwa wakitumia mbinu ya kutengeneza makosa kwa mlinzi husika na mpaka ifikie kiwango wanachokusudia kumpa licha ya kuwasilisha nyaraka zinayoonesha mlinzi alipatiwa pesa zote.

Mmoja kati ya waliokutana na suala hili anaeleza "Mimi kwa Mwezi kampuni yangu inanilipa Tsh. 300,000 lakini ni ngumu kupata hizo hela, naishia kupata 130,000/=, wanachofanya wanakuja kwa kushtukiza wakikuta upo lindo umeweka rungu chini wanakukata 30,000 au ukitoa tu kofia kichwani wanakukata mpaka waone imefikia pesa wanayoitaka ambayo ni Tsh.180,000/= au 150,000."

Mlinzi huyo anayetekeleza jukumu lake kwenye ofisi moja iliyopo Mikocheni anadai suala hilo linawakumba walinzi wengi kwenye baadhi ya makampuni, ambapo kufuatia hali hiyo anadai amezoea mshahara wake ni Tsh. 130,000 licha ya nyaraka kuonesha anapata laki tatu.

Mazingira ya umiliki wa kampuni, tenda kwenye Ofisi za Umma
Kutokana na utaratibu wa muongozo uliopo kupata kibali cha kampuni binafsi ya ulinzi, kutoka Jeshi la Polisi imekuwa ikisababisha kampuni nyingi kumilikiwa na Wastaafu kwenye vyombo vya ulinzi na usalama au vigogo waliopo karibu na mfumo wa utawala (Serikali).

Jambo hilo linatajwa kuwa licha ya utaratibu wa wazi kuwepo lakini sio rahisi kwa Mtu mwenye sifa ambazo uainishwa katika muongozo husika kuanzisha kampuni ya ulinzi, baadhi ya vyanzo vinadai ili kufanikisha vibali stahiki uhitajika 'connection' kama kukunjua mkono.

Kutokana na mazingira hayo imekuwa ikihisiwa hicho ndicho chanzo cha makampuni mengi kutowajibika kwenye masuala mbalimbali hasa yanayogusa haki na maslahi ya Wafanyakazi kwa sababu ya ukaribu uliopo baina ya wamiliki na waliopewa dhamana ya kuwajibisha mambo yanapokuwa kinyume.

'Connection' hii imekuwa ikitumika pia katika kutoa tenda kwenye taasisi za umma bila mchakato wa kiushindani au ikitokea mchakato huo umehusika basi rushwa imekuwa nyuma ya pazia kupata tenda hizo.

Mfano zipo ofisi nyingi za Serikali hata ambazo ni nyeti kuna kampuni zimepewa tenda lakini walinzi wengi uwezo wao ni mdogo na hawana hadhi ya kuhudumu kwenye ofisi nyeti za umma.

Walinzi kadhaa wanadai mishahara sio ya kuridhisha licha ya kampuni husika kuingia mikataba inayowanufaisha zaidi wao binafsi.

Hali hii inaweza kuleta athari kubwa endapo itaendelea, ikiwemo walinzi hao kuhusika kwenye mipango uovu, mfano wizi na unyanganyi, na tayari tuhuma za aina zimekuwepo tayari ambapo baadhi ya walinzi wakiwa kwenye majukumu yao kudaiwa kujihusisha na matukio ya uovu.

'Kuna wimbi la walinzi ambao hawana weledi'
Licha ya suala la maslahi ya walinzi lakini kuna jambo lingine ambalo nimelifuatilia na kubaini sio rafiki, zamani walinzi wengi waliokuwa wanaajiriwa kwenye kampuni hizi walikuwa angalau wana A, B, C za ulinzi lakini kwa sasa makampuni mengi yanawatumia watu wengi ambao hawajapitia hata mafunzo ya Mgambo wala hawana ujuzi wa ulinzi.

Wafanyakazi wengi kutokuwa na mikataba
Nimebaini wafanyakazi wengi hawana mikataba na hili limechangia kufanikisha upigaji pia kutoa vibarua kwa Watu ambao hawana sifa.

Licha ya sekta hii kuwa nyeti kwa kugusa usalama wa raia na mali zao lakini bado wafanyakazi wengi wanafanya kazi katika mazingira magumu ambayo hayatoi matumaini yao ya kesho, ni wachache kati ya wengi ambao wanawekewa pesa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kwenye hili uchunguzi zaidi unahitajika
Inasemekana kutokana na kuaminika kwa kiwango fulani kwa Kampuni ya ulinzi ya Suma-JKT ikilinganishwa na kampuni nyingi hasa za ndani, inaelezwa kumekuwepo na Suma-JKT kivuli ndani ya Suma-JKT halisi.

Ni kwamba kuna watu wamekuwa wakipewa tenda kama Suma-JKT licha ya kuwa ni kampuni nyingine, jambo hilo limedaiwa kuwa ni ngumu kubainika kwa sababu hata walinzi upewa sare zinazofanania na Suma-JKT halisi.

Jambo hilo linaacha maswali lakini ni vyema nilifikishe hapa jukwaani ili wahusika walifanyie kazi zaidi maana nimekosa muda wa kulichunguza kwa kwa kina.

Baadhi ya makampuni yakipata tenda wahuka (wahitaji) wakahitaji huduma ya ulinzi wa Suma-JKT dili halikwami badala yake mazingira yanatengezwa kufanikisha mchongo kwa kutumia Suma-JKT kivuli.

Nashauri nini?
Miezi kadhaa iliyopita niliona Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora wametoa taarifa ya kufanya uchunguzi kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za walinzi kwenye kampuni binafsi, lakini mpaka sasa sijasikia ripoti ya uchunguzi wao ikitolewa hadharani au kwenye vyombo vya habari, sijui labda wenzangu mmesikia?

Ni vyema muongozo wa kuanzisha kampuni binafsi ukaboreshwa ili kuepuka mazingira sawa katika kuanzisha kampuni hizo, lakini pia kufanya tathimini ya kampuni zilizopo mpaka sasa kubaini kama zinatimiza mashariti ya taratibu za kumungozo.

Zoezi la tathimini hiyo suala la maslahi kwa wafanyakazi lipewe kipaumbele pamoja na wimbi la kuongezeka kwa kampuni hizo pia uweledi wa walinzi kulingana sifa husika.

================
Lilivyokuwa andiko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
View attachment 3003443
View attachment 3003444
Katiba mpya!
 
Back
Top Bottom