Aga Khan kule ukiona mtu mweusi anafanya kazi ujue aidha ni kibarua au msukule. Ndio maana wanakimbia kila siku.
Ukilinganisha huduma za serikali na sekta binafsi utajua JUHA.
Kwasababu hata gharama za matibabu ni tofauti.
Ninyi wenyewe mkienda kwenye vituo vya serikali mkaambiwa lipeni consultation fee, Tsh 5,000 mnabweka Kama mbweha. Mtatafuna mpaka madiwani, wenyeviti wa vijiji, CCM mpaka za Wizara ya Afya mtapiga kulalamikia.
Vituo vya Afya vya serikali watumishi hawatoshi, mtu anafanya kazi masaa 12 hakuna extra duty, wewe unadhani huyo mtu ni roboti?
Mtumishi wa serikali HANA NYUMBA - Amepanga.
Anafanya kazi zaidi ya muda wa kazi - HALIPWI.
Anatumia pesa zake za Mshahara huo huo kufanya kazi za serikali tena.
Na Bado hicho hicho kimshahara chenyewe anachopewa bado kinawindwa na MICHANGO YA MWENGE, VYAMA VYA WAFANYAKAZI na KODI.
Halafu huyo mtu utegemee awe na morale ya kazi kweli??
Hata robot linachoka.