Upinzani hauuliwi kwa mabavu, udikteta, vitisho na ukatili, ukitaka kuua upinzani mpe Hussein Mwinyi nchi aufute upinzani

Upinzani hauuliwi kwa mabavu, udikteta, vitisho na ukatili, ukitaka kuua upinzani mpe Hussein Mwinyi nchi aufute upinzani

Upinzani ni spirit ambayo kamwe haijawahi kuuawa kwa kuwateka wapinzani, kuwatesa, kuwafunga kwa makosa ya kubambikiza etc.

Njia rahisi ya kuua upinzani ni kupitia upendo na kuwaridhisha watu licha ya kwamba hakiwezekani kuwaridhisha watu wote kwa wakati, lakini hili linawezekana akipatikana rais mwenye akili kama Hussein Mwinyi.
Tayari Mwinyi ameshagundua kuwa kodi kubwa kwa wawekezaji ni mzigo, ambao in future, wote tutakuwa losers, muwekezaji atashindwa kufanya biashara, atafunga. Serikali itapate kodi mfanyabiashara akifunga biashara? Mwananchi atapataje bidhaa na huduma supply chain ikikatika?

Pia tunahitaji watu wenye mitaji waje kuwekeza nchini. Nani yuko tayari kuona diaspora wakileta mitaji yao bila kuulizwa umepataje pesa.

Nachelea kusema kwamba Mwinyi Yuko much visionary kuliko kaka Mandege.

Mwinyi alipita nyumba kwa nyumba akiongea na Wanzibari ana kwa ana wakimjulisha shida na dhiki zao.

Huyu mwingine alikuwa ananunua majogoo kwa laki moja, akipita kwenye msururu wa MAVIEIEITE YA KIJANI. Akimwaga tu sera zake kutoka kwenye kauntabuku la kurasa mia tatu na tatu bila kuwasikiliza wananchi wanataka nini.

Mwaka 2025 nadhani mtu sahihi wa kumshindanisha na Tundu Lissu ni Hussein Mwinyi tu.
Kwani Tundu Lissu atagombea tena!! Kwa mawazo yangu aache tu kwani itakuwa anapoteza wakati. Watanzania tayati wamemjua na kimdharau. Hakuna ubishi kuwa Lissu ni kibalaka wa mabeberu.

Akipata uraisi ataishi Tanzania lkn akikosa uraisi anawakimbia watanzania. Tena kwa visingizio vya kijinga vya kuichafua nchi. Eti na Lema anatishiwa kuuawa. Bora mzee wa Faru John hana makuu na nchi yake
 
Upinzani Tanzania umejifia kutokana na:

1. Elimu bure msingi mpaka sekondari
2. Umeme kila kijiji
3. Vituo vya afya kila kijiji
4. Miradi ya maji kila mahali
5. Kukomesha wizi na ufisadi
6. Vita dhidi ya rushwa
7. Nidhamu utumishi wa umma
8. Wanyonge kwanza
9. Kufufua huduma za reli
10. Ujenzi wa meli maziwa makuu
11. Kudhibiti utoroshaji madini
12. Kufufua shirika la ndege
13. Ujenzi wa reli
14. Ujenzi bwawa la kufua umeme
15. Kutokomeza korona
16. Kuingia uchumi wa kati
17. Maendeleo bila kujali chama
18. Upinzani kwenda chama tawala ruksa
19. Muda wa kazi, Muda wa siasa
20. Kufanyia kazi hoja za upinzani
21. Kudhibiti ujangili na ujambazi
22. Endelea na wewe......
23.
24.
25.
Upinzani ni zaidi ya hayo. Mwenza mwenye kupewa kila kitu anaweza asiridhike na tabia ya mwenziwe.
Mwenye kuleta hayo ana behave vipi kwa critics wake? Hilo ndilo tatizo
 
Umekariri kwani lazima umma umiliki ndege?
Nini maana ya secta binafsi au ppp.

Mimi sijakariri, mimi nilimnukuu The Big boss wa ndege aliposema: "Tunashindwa na Vinchi vidogo vina ndege sisi hatuna hata moja". Sasa huyo the Big boss aliposema maneno hayo hakujua kama kuna Precision air na fast jet nk,???.

Kwanza Vinchi vidogo unavijua??, hivyo vinchi vinazo public airliners (mashirika yao ya ndege ni ya umma) sio ya binafsi.

Mimi naunga mkono kwamba huduma za ndege ziwe private na serikali ikusanye kodi ya viwanja nk. Serikali iachane kabisa na biashara, lakini the big boss hataki na anataka tuwe kama hivyo vinchi vidogo.
 
Ile biashara pasua kichwa
 
Tatizo la Mandege ni roho, ana roho mbaya aliyozaliwa nayo ukichanganya na ushamba aliousema Nnape inakuwa balaa.
 
Kuua upinzani ni kauli za mzee dingi, anawachukia, anawasingizia.
Hivi kama wilaya ya Kisarawe haina maendeleo kabisa, haijawahi kuwa na mwakilishi yeyote wa upinzani, lakini lawama za Kisarawe kukosa maendeleo wanapewa wapinzani, ETI WAMETUCHEREWESHA.
Hivi wakati wenzako wanasoma, hadi wanaongea Kingereza kilichonyooka, wapinzani walikuwa wamekuficha wapi?
Mkuu maendeleo ya mtu huletwa mtu mwenyewe. Hakuna serikali Duniani inamletea mtu maendeleo bali serikali inaandaa miundombinu ya kukuwezesha ww kupata maendeleo. Kama barabara nzr, tiba ya uhakika, elimu nzuri nk

Lakini wanasiasa wetu hawawafumbui macho wananchi wao waliyowachagua matokeo yake wanawaongopea kuwa serikali inaleta maendeleo kwa mtu. Nao watu wa aina yako bado mnawaongopea watu kuwa serikali inamletea mtu maendeleo.
 
Mwaka 2025 nadhani mtu sahihi wa kumshindanisha na @Tundu Lissu ni Hussein Mwinyi tu.
Mmeanza kumrukia mwinyi sasa
Ndio maana ccm tunaamini tutatawala milele
Mfuasi wa chadema anatutafutia mgonbea mzuri kwa ajili ya 2025
Tundu lissu ameshaomba uraia wa ubelgiji,hiyo 2025 labda agombee umeya Genk
 
Tanzania hakuna tena uchaguzi labda Magufuli afe kabla ya 2025 kitu ambacho pia kinawezekana maanake yeye sio malaika.

Upinzani hauwezi kamwe kufa kisa fulani ndio rais kwani hata nchi zilizoendelea zinazotupa "Handouts" zote zina upinzani.
 
Mkuu maendeleo ya mtu huletwa mtu mwenyewe. Hakuna serikali Duniani inamletea mtu maendeleo bali serikali inaandaa miundombinu ya kukuwezesha ww kupata maendeleo. Kama barabara nzr, tiba ya uhakika, elimu nzuri nk

Lakini wanasiasa wetu hawawafumbui macho wananchi wao waliyowachagua matokeo yake wanawaongopea kuwa serikali inaleta maendeleo kwa mtu. Nao watu wa aina yako bado mnawaongopea watu kuwa serikali inamletea mtu maendeleo.
Maendeleo makubwa kuliko yote ni kugawa elimu iliyo bora na viwango, serikali pamoja na wawakilishi wao imewanyima/inawanyima kwa makusudi
iendelee kuwalaghai wananchi wake.
 
Mmeanza kumrukia mwinyi sasa
Ndio maana ccm tunaamini tutatawala milele
Mfuasi wa chadema anatutafutia mgonbea mzuri kwa ajili ya 2025
Tundu lissu ameshaomba uraia wa ubelgiji,hiyo 2025 labda agombee umeya Genk
Kutawala milele pasipo na utawala bora ni jehanamu.
 
Bila kuisimamia upande wowote kisiasa. Rais Dr. Hussein Mwingi is the best president. Ataibadilisha Zanzibar kiuchumi, kijamii na Kisiasa. Ataimarisha umoja Zanzibar mpaka tushangae. Ukweli sijui Wazanzibar walimuombaje Mungu akasikia kiluo chao. Nanikuhakikishie 2025 Hussein Mwinyi atashindakwa kura nyingi mno ambazo haxitakuwa na kumwaga damu wala mitutu kuwahofisha wananchi. Hongereni zenu Zanzibar.
 
Tza anaestahili kuabudiwa ni mmoja tu msianze kumchongoea ya Robert Ouko yakamfika.
Mawe ni hatari Sana kwa ujenzi wa nyumba bora
 
Hingereni wa Zanzibar kwa kumchagua rais makini ambae sasa hadi Bavicha wanamuona ni mtu makini mno
 
Back
Top Bottom