Wakuu amani kwenu na poleni na pilikapilika za kampeni za uchaguzi mkuu.
Jambo ninalotaka kuwashirikisha na kuwaasa wapinzani ni kuwa BILA KUIPASUA CCM KATIKATI na kufanya walau nusu ya wanaCCM wapigie kura upinzani, Lissu hawezi kushinda uchaguzi huu. Huu ndio ukweli mchungu. Angalia mahesabu hapa chini:
Jumla ya wapiga kura ni milioni 29, kwa uzoefu wa 2015 watakaopiga kura ni 60% tu ya hao maana yake kura halisi jumla ni milioni 18, si zaidi ya hapo.
Sasa CCM ina wanachama walio hai karibia milioni 8 ambao ni watiifu kwa chama. Wanabaki wapiga kura milioni 10 (18-8) ambao si wanaCCM damu. kati ya hao tuseme 20% to ndio watampigia kura JPM ambao ni sawa na milioni 2 (20% ya milioni 10). Ina maana kwa makadirio ya chini kabisa JPM atapata kura milioni 10 ambazo ni 55% ya kura zote. Hii tayari ni ushindi kwa CCM.
Ndio maana nasema bila kushawishi walau nusu ya wanaCCM kupigia kura upinzani huwezi kuishinda CCM. Sasa habari mbaya/nzuri ni kuwa mwaka huu 2020 CCM wako wamoja kuliko 2015. Tatizo lingine ni kuwa hakuna jitihada katika kampeni za kuwaomba na kuwashawishi wanaCCM wampigie Lissu, sana sana wanatukanwa na kuitwa "Ma-CCM".
Uchaguzi na ushindi ni suala la numbers naona upinzani hawajacheza vizuri namba zao na kwa hiyo wasishangae wakishindwa.
Tafiti upingwa na tafiti, kama unaona nilichowasilisha si sahihi, weka namba zako hapa tuone kama zinaubeba upinzani kushinda.