Upinzani hauwezi kushinda bila kuipasua CCM katikati

Upinzani hauwezi kushinda bila kuipasua CCM katikati

..hoja kwamba ccm lazima ipasuke ni ya miaka ya 90 na 2000.

..wakati huo watz wengi walikuwa hawana mazoea ya mfumo wa vyama vingi.

..vyama vya upinzani vimekuwepo kwa zaidi ya miaka 20, na watz wameuzoea mfumo wa vyama vingi kuliko hapo awali.

..maendeleo ya sekta ya Mawasiliano na Teknolojia yamefanya upatikanaji uwe mrahisi, na hivyo kurahisisha pia shughuli za uenezi na upatikanaji wa habari za vyama vyote kwa ujumla.

..katika uchaguzi huu unaweza kupata habari za kampeni za mgombea yeyote wa uraisi hata LIVE. fikiria ilikuwaje mwaka 1995 wakati Mkapa, Mrema, Lipumba, na John Cheyo, walipogombea ktk uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi.

..kwa maoni yangu, watz wa sasa hivi wanaweza kuchagua chama chochote, wanachohitaji ni KUSHAWISHIWA.
 
CCM tayari ilishajipasua yenyewe wala hakuna haja ya kuhangaika nayo! Cha kuhangaikia ni kutafta namna ya kuthibiti wizi wa kura tu!

Ndani ya hicho chama kuna kundi kubwa sana litampigia kura Lissu, hili kundi ni sehemu ya vipande vilivyopasuka ndani ya ccm. Ukitaka kulijua hilo rejea mchakato wa kura maoni ambapo wanachama walioshinda kihalali, walizibiwa nafasi zao na kupewa walishindwa!

Rejea uvunjwaji wa misingi na katiba ya hicho chama unaofanywa na mwenyekiti wake , mfano mzuri ni ule ulanguzi wa viongozi na wanachama wa upinzani, alafu kisha mtu hajamaliza hata mwezi ndani ya ccm akateuliwa kugombea ubunge huku wale waliokipigania chama hicho miaka nenda rudi wakibakia vijiweni na sifa wanazo!
acha uchizi wewe Mwenyekiti alilangua lini watu? na kama alilangua Lowassa, Nyarandu, Hamisi Mgeja, Makongoro Mahanga, na wengine wengi mlifika beo gani wakajiunga na CHADEMA?
 
acha uchizi wewe Mwenyekiti alilangua lini watu? na kama alilangua Lowassa, Nyarandu, Hamisi Mgeja, Makongoro Mahanga, na wengine wengi mlifika beo gani wakajiunga na CHADEMA?
Ni wewe tu ndo umebakia hujui chochote! Ndo mana hata leo hii akiingia humo mwanachama wa CHADEMA, kesho tu anapewa uteuzi huku wewe ukiendelea kukodoa macho yako hayo yanayotazama buk 7 tu!
 
Wakuu amani kwenu na poleni na pilikapilika za kampeni za uchaguzi mkuu.

Jambo ninalotaka kuwashirikisha na kuwaasa wapinzani ni kuwa BILA KUIPASUA CCM KATIKATI na kufanya walau nusu ya wanaCCM wapigie kura upinzani, Lissu hawezi kushinda uchaguzi huu. Huu ndio ukweli mchungu. Angalia mahesabu hapa chini:

Jumla ya wapiga kura ni milioni 29, kwa uzoefu wa 2015 watakaopiga kura ni 60% tu ya hao maana yake kura halisi jumla ni milioni 18, si zaidi ya hapo.

Sasa CCM ina wanachama walio hai karibia milioni 8 ambao ni watiifu kwa chama. Wanabaki wapiga kura milioni 10 (18-8) ambao si wanaCCM damu. kati ya hao tuseme 20% to ndio watampigia kura JPM ambao ni sawa na milioni 2 (20% ya milioni 10). Ina maana kwa makadirio ya chini kabisa JPM atapata kura milioni 10 ambazo ni 55% ya kura zote. Hii tayari ni ushindi kwa CCM.

Ndio maana nasema bila kushawishi walau nusu ya wanaCCM kupigia kura upinzani huwezi kuishinda CCM. Sasa habari mbaya/nzuri ni kuwa mwaka huu 2020 CCM wako wamoja kuliko 2015. Tatizo lingine ni kuwa hakuna jitihada katika kampeni za kuwaomba na kuwashawishi wanaCCM wampigie Lissu, sana sana wanatukanwa na kuitwa "Ma-CCM".

Uchaguzi na ushindi ni suala la numbers naona upinzani hawajacheza vizuri namba zao na kwa hiyo wasishangae wakishindwa.

Tafiti upingwa na tafiti, kama unaona nilichowasilisha si sahihi, weka namba zako hapa tuone kama zinaubeba upinzani kushinda.
UNAJIFURAHISHA tu Mkuu, kwa viboko hivi vya CCM ndani ya miaka mitano ni Mwananchi ana hamu tena na hawa WATEKA NYARA mchana kweupe?
 
Hesabu kama za motivisheni spika wa kilimo cha matikiti.
 
Back
Top Bottom