Uchaguzi 2020 Upinzani kumsimamisha Membe: Kosa kubwa, usaliti na dhambi isiyosameheka

Nitajitahidi next time niache papara, ni Membe na sio Mwmbe. Mods watarekebisha.

Lakini ujumbe uko crystal clear, Kumsimamisha Membe ni bad idea.

Hata Membe mwenyewe ni mtumiaji sana wa mitandao, nadhani anaoona wafuasi wa upinzani wasivyomkubali. Hapa anapata ujumbe kuwa watu tumeshaumwa na Nyoka Lowassa, hivyo tukiona unyasi tunastuka.
 
Absolutely
 
Point namba 4 nimeielewa zaidi.

Weka kichwani sana hiyo.
Siasa ni mbinu zaidi ya mbinu.
 
Mimi naona bora tumsimamishe membe kuliko yule msaliti aliyekuwa anatetea Mabeberu yatuibie madini yetu
Mume wako aliyesimamishwa hajakutosha? Mbona unawashwa washwa ww kuingilia mambo yasiyokuhusu? Unaona bora ”tumsimamishe Membe kuliko yule msaliti...” hivi tokea lini wewe Umeutakia mema upinzani? Sasa basi,unachotakiwa ww kufanya ni kujitahidi kujitoa akili kwa Polepole and the like ili uendelee kutupiwa makombo kama njia peekee ya kukusaidia kuishi na familia yako.
 
Halafu Membe alivyo mnafiki,wakati akilialia kuminywa demokrasia ya ushindani ndani ya CCM na yeye katoa sharti la wapinzani kuungana halafu wampe ugombea mezani tu bila kushindanishwa!

Kwa nini asijiunge huko halafu afuate taratibu za vyama hivyo vya kumpata mgombea ikiwemo kushindanishwa? Si anapenda ushindani?
 
Ndio hapo sasa, amekwisha jiona kana kwamba upinzani unamuhitaji zaidi yeye, hivyo apewe kilakitu mezani ili awaokoe.
 
Kwanza kitendo cha Membe kusema vyama vya upinzani vikiungana na kumuomba agombee ni kuvidhalilisha sana vyama husika.

Ina maana Membe ni mkubwa kuliko vyama hivyo mpaka aende kupigiwa magoti kwenda kugombea ?

Je dhamira yake ikoje juu ya mageuzi ya nchi hii au anaenda kuingiza kutafuta uongozi wa nchi.

Membe akagombee kwa mkewe atuache na vyama vyetu tunawagombea wengi sana wa kuweza kugombea urais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…