Kama CHADEMA na ACT - WAZALENDO na washirika wao wataingia kwenye mtego huu wa wazi kabisa wa CCM, tutawashangaa mno....!!
Kuna dalili kuwa ACT - Wazalendo watampokea Benard Membe na watampa fursa ya kuwania Urais....
ACT - Wazalendo wakifanya hivyo, tayari kutakuwa na mgogoro kwenye muungano wao na mkakati wa "SYSTEM" kuudhoofisha upinzani utakuwa umefanikiwa....
Sisi kazi yetu ni kutahadharisha. Bernard Membe na CCM ni pete na kidole. Wako pamoja tangu mwanzo hata sasa....
Kubwabwaja bwabwaja kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwa Bernard Membe huku akionekana kukishambulia chama chake (CCM), serikali na Rais aliye madarakani sasa toka ndani ya chama chake, yote hiyo ni sehemu ya mkakati uliopangwa vyema huku wasiojua wakipumbazika...
Yote haya ya kufukuzwa uanachama yeye MEMBE na wenzake wale kujifanya walikosea na kuomba radhi na kisha kuonekana kama wamesamehewa ni sehemu ya mkakati thabiti na kuwapumbaza wapinzani wanaotaka kui - replace CCM ktk utawala wa nchi na dola....
Watch out, mtaingia mkenge wa hatari...!!