Maelezo yako mazuri ila zingatia ushauri nilioutoa, kwamba ikiwezekana aje na huku maana sisi tunamuona mitandaoni tu, sasa vijana walio kwenye mitandao ni wachache sana.Kijana Clever505, ngoja nikupe ushauri kidogo nikianzia na kaswali kadogo kuhusu neno clever ulilolitumia kwenye avatar yako hapo juu, je unajua tafsiri sahihi ya neno hilo? Mh. Tundu Antiphas Lissu kabla ya kurejea nyumbani, dhihaka dhidi yake ziliendeshwa hivyo hivyo kwa dhana potofu kuwa mashabiki wake ni wa mtandaoni tu...
Mzee, mikoa ipi hapa Tz unayoiita wewe inajitambua na haina umasikini? Ina maana mkoa uliopo wewe wote mnajitambua na pia ni matajiri sio? Kuwa CCM ni kutokujitambua? Achana na ushabiki wa kitoto wa kuona kila aliye kinyume na wewe ni mjinga. Halafu aliyekwambia kuitwa mnyonge ni sifa nani?Mtaji wao ni watu kama nyie, ndio maana ktk mikoa mingi yenye umasikini wa kutupa/ujinga ni kama dodoma, singida, mtwara, pwani, kwani hamjitambui!! Angalia mikoa inayojitambua, na nyie msiyejitambua utofauti uliopo. Eti kuitwa mnyonge nayo ni sifa wakati ni laana!!!
Mleta mada huenda ana nia njema.Lakini Huyo mtawala alikuwa katiri sana kwa wapinzani.Hawakuruhusiwa kufanya siasa kwa miaka mitano.Wapinzani na hasa viongozi wa kuu walikuwa na kesi miaka yote.Hata uhai huu ni Mungu tu ashukuriweHali ni ngumu kuliko unavyodhani vijijini.Na kutokana na Hali ya kimaisha kuwa ngumu upinzani vijijini Ni mkubwa kuliko. Hata hivyo upinzani upite Kijiji kwa Kijiji,mtaa kwa mtaa, kanisa kwa kabisa,msikiti kwa msikiti kuhakikisha tunapata utawala mpya mwaka huu.ccm ndiyo imetufikisha hapa tulipo.kila mwaka inakuja na slogan mpya kuwatesa wananchi.
Hujanielewa, ndio maana nimesema umasikini wa kutupa!! Kila mwaka huwa kuna ripoti inatoka ya viwango vya umasikini kwa kila mkoa, itafute kwanza hiyo, uipitie, watu wa vijijini, ndio wenye tabu sana lakini wao uelewa ni mdogo sana, mtu hata maji safi tu, hakuna, lakini, haelewi, ndio hao wakija kuwekewa video za vita tayari ameogopa!! Narudia tena umasikini na ujinga wa watanzania wengi ndio kikwazo cha kupata viongozi bora!! Sasa kiongozi anapojisifia kuwa ni kiongozi wa wanyonge, na hao wanyonge wanajisifia maana yake nini? Sio kuwa kila aliyepo kinyume na mimi namuona mjinga, siasa za vyama ndio zimetufikisha hapa, kwani sisi wananchi ndio tunaumia tunapoona mambo hayaendi kama inavyotakiwa lakini mkitaka kulazimisha yaende ili kila mtu afaidike na keki ya taifa unaambiwa sio mzalendo, ili watu waendelee kulala tu!! Huwezi hubiri AMANI BILA kusisitiza HAKI kwanza!! Je haki ipo, huwezi jiuliza kwanini nchi za ulaya kuna amani, kwasababu haki ipo!!Mzee, mikoa ipi hapa Tz unayoiita wewe inajitambua na haina umasikini? Ina maana mkoa uliopo wewe wote mnajitambua na pia ni matajiri sio? Kuwa CCM ni kutokujitambua? Achana na ushabiki wa kitoto wa kuona kila aliye kinyume na wewe ni mjinga. Halafu aliyekwambia kuitwa mnyonge ni sifa nani?
Thats true kuanzia fedha mpaka human resource jamaa hawana tuwe wakweli wale viongozi wao machachar hali zao majimboni ni mbaya sana hawanauhakika wakurudi majimboni... Hawatakuwa na timu za kushambulia sehemu mbalimbali at a time ... Wakati wenzao watakuwa wanapishana ardhini na angani kushambulia kila pembe...Hawana resources kuwezesha hicho umacho kishauri..