Upinzani Tanzania ni dhaifu na Kibogoyo

Upinzani Tanzania ni dhaifu na Kibogoyo

Nchi imejaa wajinga wanaowaza simba na yanga hakuna shida kwa kwa viongozi wa upinzani
Wanawaza simba na yanga kwa sababu hakuna wa kuwachagiza wawaze vitu vingine, leo wanaona serikali inafanya jambo hili kisha hawaoni alternative kutoka upinzani, so wanajionea vyote ni sawa tu, bora waendelee na maisha yao ya kila siku,
 
Kua kiongozi wa upinzani Tanzania ni stress tu.
Unawateteaje watu waoga na wasiojiolewa!!

Watanzania waliopiga kelele swala ya bandari ni mamilioni, lakini waliojitokeza hadharani kwenye maandamano ya kupinga ubinafsishwaji wa bandari ni 6 pekee [emoji23][emoji23][emoji23]

Halafu bado kuna mtu anawalaumu viongozi wa upinzani. Unataka wafanye nini!!

Mabadiliko ya kweli yanaanza na wewe mwenyewe.
 
wasalam,

Natafakari juu ya mbadala wa Serikali Tanzania, yaani upinzani sipati majibu!!!!
Kuna umuhimu wa kua na upinzani kweli?
Umuhimu wake uko wapi? Ikiwa kila Jambo linakuja na linapita kama lilivyo bila pingamizi lolote popote, si ndani ya Bunge au nje ya Bunge. Je, kuna Serikali mbadala kweli Tanzania?
Wenye mawazo tofauti na ya serikali wakapate wapi matumaini?
Haya yote yanayotokea na yanayoendelea kutokea kungekua na upinzani makini na imara, mpaka sasa kungekua na mgogoro wa kikatiba ambao ungepelekea masahihisho na mabadiliko mengi sana ndani ya serikali na pengine kungekua hata na serikali ya Umoja wa kitaifa ya JMT.

kwa mfano:
1. Kuna wabunge wanaitwa covid 19 wamefutwa uanachama kwenye vyama vyao lakini mpaka leo wanadunda bungeni kwa madaha na mikogo kama yote bila wasiwasi. Je, upinzani umeshindwa na Bunge, Mahakama au serikali? Upinzani makini usingeruhusu muhimili wowote kati ya hii kuwakumbatia hawa COVID-19 ambao wako kinyume na Sheria. Inchi ingesimama whether kuna kesi Mahakamani au hakuna.

2. Kukamatwa na kutiwa nguvuni kwa miongoni mwa wapinzani nchini kwa tuhuma za kubambikiwa. Kungekua na upinzani makini nchi haingekua stable na kazi zote zingesimama.

3. Tozo kwenye miamala, mfumuko wa Bei na kupaa kwa gharama za maisha. Upinzani makini usingeruhusu hali hii ishamiri kiasi hiki. Ungekua aidha umeilazimisha serikali kufanya Jambo au kuhamia Burundi.

4. Ukosefu wa ajira na ongezeko la vitendo vya kihalifi mtaani na mitandaoni, vitendo vya ushoga na ukahaba. Upinzani makini ungerekebisha hali hii kwa kelele mingi za hoja na mapendekezo ya mipango mbadala kutatua tatizo.

5. Tuhuma za Rushwa iliyokithiri kwenye taasisi na mashirika ya umma. Upinzani makini haungekubali watuhumiwa wa Rushwa kuendelea kushika nafasi serikalini.

5. Mradi wa SGR na Behewa zake, Bandari na Dp world ni hoja kubwa sana inayoweza waunganisha wa Tz na kuwawajibisha wahusika na serikali kwa ujumla na hatimae kuongeza uwazi na utawala bora nchini. Upinzani dhaifu na Kibogoyo kimyaaa....

6. Tume huru ya uchaguzi, Sheria za uchaguzi, Daftari la wapiga kura na Katiba mpya, zilitosha kua hoja za kuifanya serikali isitulie wala kulala usingiz bali kuwatumikia wananchi kadiri ya mapendekezo yao kupitia upinzani.

7. Uvunjiwaji nyumba bila fidia kupisha miradi mbalimbali ya kiserikali, kuhamishwa kwa Lazima wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine wakiwemo wamaasai wa Longido.

8. Utekaji wa watu na upotevu wa watu na watu wasiojulikana

Kwa maoni yangu hayo yalitosha kuwaunganisha wapinzani na wananchi kuisimamia na kuiwajibisha serikali vilivyo nje ya Bunge na hatimae Taifa lingeweza kupiga hatua za kimaendeleo.

Mapendekezo.
1. kuundwe Baraza la upinzani nje ya Bunge, likihusisha vyama vyote vya upinzani. Ili kusudi maoni ya wananchi yasipowasilishwa vema bungeni, Baraza nje ya Bunge lichukue nafasi hiyo.

2. Wapinzani kuepuka kuwatanguliza mbele viongozi hasa vijana wasio na maadili na wasioweza kudhibiti hisia zao dhidi ya hoja tofauti na Mawazo na mitazamo yao. Wawekwe viongozi makini, wastarabu wa kujibu hoja kwa hoja na sio matusi. Wanazuoni wengi wanatamani kujiunga upinzani lakini credibility ya upinzani inaondolewa na frontend youth ambao wanadhani kutukana na kudhihaki viongozi wa serikali ndio ujasiri au ndio aonekane kiongozi hodari kumbe anashusha weledi wa Chama kizima na hivyo wengi kusita kujiunga nao.

3. Kujizuia na Kuepuka kuongea ongea na kujieleza sana hadi inakua kero. Ni vizuri kusamarize kwa kifupi tena kwa lugha nyepesi with clearity sio unaongea hadi wasikilizaji wanasahau unaongelea nini, na ulianzia wapi na waulize maswali gani.

4. Kuepuka Kudandia dandia kila hoja hata zisizo na maana na baada ya muda mfupi inakua haina maana tena na wewe unakosa maana vilevile. Inafanya uchoke na jamii ikuchoke vilevile.

5. Kuonekana onekana mara kwa mara, yaani kiongozi hata jamii haikumisi, yaani we kila siku tunakuona tu leo umezunguzia hili kesho lile, keshokutwa umekubali hili, mtondogoo umekataa lile. Yaani haileweki lipi ni lipi. Hii sio nzuri, potea kidogo then ibuka na detailed info ya kitu ama vitu flani utakua relevant sana politically speaking.....

Mwisho,
Nadhani upinzani Tz unapaswa kua na Think Tanks ambao wao kazi yao ni kupanga, kubuni na kushauri dira na uelekeo sahihi wa upinzani kwa wakati sahihi. Kwa kufanya hivi Tanzania tunaweza kuendelea mbele na kwa kasi zaidi. Kuwa think tank na vilevile actor kunafanya uchuje na kuishiwa pumzi, mvuto na uelekeo haraka.

Aidha, Ubinafsi, Tamaa na kutokuaminiana kutaendeleza udhaifu na ukibogoyo uliopo na kudumaza maendeleo, haki, usawa na uwajibikaji.

yapi maoni yako.....
wewe uyliyeshujaa weka jina lako halisi
 
Mijitu mingine mipuuzi kweli,umelala huko unasema upinzani wafanye hivi wafanye vile
Wewe unafanya nini,wapinzani ni wa kina nani?
Unafki na upumbavu wa watanzania ndiyo unairudisha nchi nyuma
 
Pendekezo langu no.2 linakuhusu sana
 
wasalam,

Natafakari juu ya mbadala wa Serikali Tanzania, yaani upinzani sipati majibu. Kuna umuhimu wa kua na upinzani kweli? Umuhimu wake uko wapi? Ikiwa kila Jambo linakuja na linapita kama lilivyo bila pingamizi lolote popote, si ndani ya Bunge au nje ya Bunge. Je, kuna Serikali mbadala kweli Tanzania?

Wenye mawazo tofauti na ya serikali wakapate wapi matumaini? Haya yote yanayotokea na yanayoendelea kutokea kungekua na upinzani makini na imara, mpaka sasa kungekua na mgogoro wa kikatiba ambao ungepelekea masahihisho na mabadiliko mengi sana ndani ya serikali na pengine kungekua hata na serikali ya Umoja wa kitaifa ya JMT.

Kwa mfano:
1. Kuna wabunge wanaitwa covid 19 wamefutwa uanachama kwenye vyama vyao lakini mpaka leo wanadunda bungeni kwa madaha na mikogo kama yote bila wasiwasi. Je, upinzani umeshindwa na Bunge, Mahakama au serikali? Upinzani makini usingeruhusu muhimili wowote kati ya hii kuwakumbatia hawa COVID-19 ambao wako kinyume na Sheria. Inchi ingesimama whether kuna kesi Mahakamani au hakuna.

2. Kukamatwa na kutiwa nguvuni kwa miongoni mwa wapinzani nchini kwa tuhuma za kubambikiwa. Kungekua na upinzani makini nchi haingekua stable na kazi zote zingesimama.

3. Tozo kwenye miamala, mfumuko wa Bei na kupaa kwa gharama za maisha. Upinzani makini usingeruhusu hali hii ishamiri kiasi hiki. Ungekua aidha umeilazimisha serikali kufanya Jambo au kuhamia Burundi.

4. Ukosefu wa ajira na ongezeko la vitendo vya kihalifi mtaani na mitandaoni, vitendo vya ushoga na ukahaba. Upinzani makini ungerekebisha hali hii kwa kelele mingi za hoja na mapendekezo ya mipango mbadala kutatua tatizo.

5. Tuhuma za Rushwa iliyokithiri kwenye taasisi na mashirika ya umma. Upinzani makini haungekubali watuhumiwa wa Rushwa kuendelea kushika nafasi serikalini.

5. Mradi wa SGR na Behewa zake, Bandari na Dp world ni hoja kubwa sana inayoweza waunganisha wa Tz na kuwawajibisha wahusika na serikali kwa ujumla na hatimae kuongeza uwazi na utawala bora nchini. Upinzani dhaifu na Kibogoyo kimya.

6. Tume huru ya uchaguzi, Sheria za uchaguzi, Daftari la wapiga kura na Katiba mpya, zilitosha kua hoja za kuifanya serikali isitulie wala kulala usingiz bali kuwatumikia wananchi kadiri ya mapendekezo yao kupitia upinzani.

7. Uvunjiwaji nyumba bila fidia kupisha miradi mbalimbali ya kiserikali, kuhamishwa kwa Lazima wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine wakiwemo wamaasai wa Longido.

8. Utekaji wa watu na upotevu wa watu na watu wasiojulikana.

Kwa maoni yangu hayo yalitosha kuwaunganisha wapinzani na wananchi kuisimamia na kuiwajibisha serikali vilivyo nje ya Bunge na hatimae Taifa lingeweza kupiga hatua za kimaendeleo.

Mapendekezo
1. kuundwe Baraza la upinzani nje ya Bunge, likihusisha vyama vyote vya upinzani. Ili kusudi maoni ya wananchi yasipowasilishwa vema bungeni, Baraza nje ya Bunge lichukue nafasi hiyo.

2. Wapinzani kuepuka kuwatanguliza mbele viongozi hasa vijana wasio na maadili na wasioweza kudhibiti hisia zao dhidi ya hoja tofauti na Mawazo na mitazamo yao. Wawekwe viongozi makini, wastarabu wa kujibu hoja kwa hoja na sio matusi. Wanazuoni wengi wanatamani kujiunga upinzani lakini credibility ya upinzani inaondolewa na frontend youth ambao wanadhani kutukana na kudhihaki viongozi wa serikali ndio ujasiri au ndio aonekane kiongozi hodari kumbe anashusha weledi wa Chama kizima na hivyo wengi kusita kujiunga nao.

3. Kujizuia na Kuepuka kuongea ongea na kujieleza sana hadi inakua kero. Ni vizuri kusamarize kwa kifupi tena kwa lugha nyepesi with clearity sio unaongea hadi wasikilizaji wanasahau unaongelea nini, na ulianzia wapi na waulize maswali gani.

4. Kuepuka Kudandia dandia kila hoja hata zisizo na maana na baada ya muda mfupi inakua haina maana tena na wewe unakosa maana vilevile. Inafanya uchoke na jamii ikuchoke vilevile.

5. Kuonekana onekana mara kwa mara, yaani kiongozi hata jamii haikumisi, yaani we kila siku tunakuona tu leo umezunguzia hili kesho lile, keshokutwa umekubali hili, mtondogoo umekataa lile. Yaani haileweki lipi ni lipi. Hii sio nzuri, potea kidogo then ibuka na detailed info ya kitu ama vitu flani utakua relevant sana politically speaking.

Mwisho
Nadhani upinzani Tz unapaswa kua na Think Tanks ambao wao kazi yao ni kupanga, kubuni na kushauri dira na uelekeo sahihi wa upinzani kwa wakati sahihi. Kwa kufanya hivi Tanzania tunaweza kuendelea mbele na kwa kasi zaidi. Kuwa think tank na vilevile actor kunafanya uchuje na kuishiwa pumzi, mvuto na uelekeo haraka.

Aidha, Ubinafsi, Tamaa na kutokuaminiana kutaendeleza udhaifu na ukibogoyo uliopo na kudumaza maendeleo, haki, usawa na uwajibikaji.

Yapi maoni yako?

Ni kweli upinzani ni dhaifu maana hawana silaha, kwani kwa sasa hakuna siasa za ushindani wa hoja, bali matumizi ya nguvu za dola, na kwenye chaguzi waliopo madarakani ndio wanaamua matokeo yaweje, na sio kura za wananchi.

Hao wasomi unaosema wanaogopa kujiunga na vyama vya upinzani maana vina mapungufu, kwanini wao hawaanzishi vya kwao bali wanasubiri tu kuingia kwa vyama vya wenye uthubutu? Sasa kama hawawezi hata kuanzisha vyama vyao, uwezo kwenye vyama vya wenye uthubutu watautoa wapi?

Ww binafsi umeleta uzi mrefu wa lawama zenye ukweli kiasi na upotoshaji mwingi, kama unaona udhaifu uliopo wa vyama vya upinzani, na ukatoa ni nini kifanyike, kwanini ww usianzishe chama cha upinzani, kisha uzibe hilo ombwe? Au ww ni wale motivational speaker?
 
very interesting response thank you very much for challenge 🌷🥀
 
Sasa kama wanaandamwa sana Na kufanyiwa matendo ya hila kuwakandamiza wafanyeje?

Imagine hadi mikutano ya hadhara wamezuiwa kwa miaka mingi wafanyeje sasa?

Ambayo ni haki yao ya msingi kikatiba.

Wengine walifungwa , kutiwa kwenye misukosuko, jaribio la kuuawa n.k.

Ungekuwa wewe ungewashauri wafanyeje labda?
 
Nimependekeza hapo chini ndugu, fahamu ya kua Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Kama Taifa tusingekua wamoja hadi leo tusingepata Uhuru. Ubinafsi, chuki, na Mgawanyiko mkubwa uliopo upinzani ukiendelea, utakua dhaifu zaidi na mambo yatakuja yatapita kama yalivyo na kulalama hakuta isha hadi hapo watakapokua wamoja.
 
Back
Top Bottom