Upinzani Tanzania ni dhaifu na Kibogoyo

Nchi imejaa wajinga wanaowaza simba na yanga hakuna shida kwa kwa viongozi wa upinzani
Wanawaza simba na yanga kwa sababu hakuna wa kuwachagiza wawaze vitu vingine, leo wanaona serikali inafanya jambo hili kisha hawaoni alternative kutoka upinzani, so wanajionea vyote ni sawa tu, bora waendelee na maisha yao ya kila siku,
 
Kua kiongozi wa upinzani Tanzania ni stress tu.
Unawateteaje watu waoga na wasiojiolewa!!

Watanzania waliopiga kelele swala ya bandari ni mamilioni, lakini waliojitokeza hadharani kwenye maandamano ya kupinga ubinafsishwaji wa bandari ni 6 pekee [emoji23][emoji23][emoji23]

Halafu bado kuna mtu anawalaumu viongozi wa upinzani. Unataka wafanye nini!!

Mabadiliko ya kweli yanaanza na wewe mwenyewe.
 
wewe uyliyeshujaa weka jina lako halisi
 
Mijitu mingine mipuuzi kweli,umelala huko unasema upinzani wafanye hivi wafanye vile
Wewe unafanya nini,wapinzani ni wa kina nani?
Unafki na upumbavu wa watanzania ndiyo unairudisha nchi nyuma
 
Mijitu mingine mipuuzi kweli,umelala huko unasema upinzani wafanye hivi wafanye vile
Wewe unafanya nini,wapinzani ni wa kina nani?
Unafki na upumbavu wa watanzania ndiyo unairudisha nchi nyuma
Pendekezo langu no.2 linakuhusu sana
 

Ni kweli upinzani ni dhaifu maana hawana silaha, kwani kwa sasa hakuna siasa za ushindani wa hoja, bali matumizi ya nguvu za dola, na kwenye chaguzi waliopo madarakani ndio wanaamua matokeo yaweje, na sio kura za wananchi.

Hao wasomi unaosema wanaogopa kujiunga na vyama vya upinzani maana vina mapungufu, kwanini wao hawaanzishi vya kwao bali wanasubiri tu kuingia kwa vyama vya wenye uthubutu? Sasa kama hawawezi hata kuanzisha vyama vyao, uwezo kwenye vyama vya wenye uthubutu watautoa wapi?

Ww binafsi umeleta uzi mrefu wa lawama zenye ukweli kiasi na upotoshaji mwingi, kama unaona udhaifu uliopo wa vyama vya upinzani, na ukatoa ni nini kifanyike, kwanini ww usianzishe chama cha upinzani, kisha uzibe hilo ombwe? Au ww ni wale motivational speaker?
 
very interesting response thank you very much for challenge 🌷🥀
 
Sasa kama wanaandamwa sana Na kufanyiwa matendo ya hila kuwakandamiza wafanyeje?

Imagine hadi mikutano ya hadhara wamezuiwa kwa miaka mingi wafanyeje sasa?

Ambayo ni haki yao ya msingi kikatiba.

Wengine walifungwa , kutiwa kwenye misukosuko, jaribio la kuuawa n.k.

Ungekuwa wewe ungewashauri wafanyeje labda?
 
Nimependekeza hapo chini ndugu, fahamu ya kua Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu. Kama Taifa tusingekua wamoja hadi leo tusingepata Uhuru. Ubinafsi, chuki, na Mgawanyiko mkubwa uliopo upinzani ukiendelea, utakua dhaifu zaidi na mambo yatakuja yatapita kama yalivyo na kulalama hakuta isha hadi hapo watakapokua wamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…