Upinzani Tanzania una matatizo? Vyama havina Succession Plan hivyo vina Usultani! CHADEMA kuna Usultani? Usultani huu Utakiinua au Utakiangamiza?

Baada ya plan yenu kushindwa ku work mtaandika sana makala za kujifariji na kujaribu kuushawishi umma juu ya kuuchukia upinzani.

Ila eleweni moja tu wapinzani ni chaguo la wananchi wengi kwa sasa ndio mdomo wa wanyonge wanao onewa na hii serikali isiyoyajali maslahi yao.

Ninaamini hata mtambike vipi, kama upinzani utaendelea kuumia kwa ajiri ya kero za mwananchi siku zote wananchi wataendelea kuwa pamoja nao maana ndio pekee wanaobeba maumivu ya wananchi.

Hata muwapige vipi upinzani, kama ccm itaendelea kupuuza changamoto za;

1. Wafanyakazi
2. Wakulima na
3. Wafanya biashara

Kamwe hawatowaunga mikono, mnaongea mengi mazuri lakini mnasahau ;

1. watumishi wanapunjwa malipo yao na wanahitaji promotion zao

2. Wakulima wanataka masoko bora ya mazao yao na pembejeo

3. Wafanyabiashara wanafunga biashara zao kwa kufilisiwa mitaji na kodi zisizo uhalisia.

Wananchi wanalemewa na gharama za matibabu zimekuwa juu.

Ujinga wenu mmekalia kuviua vyama kwa mikono yenu, mnasahau wananchi ndio watakaoviuwa vyama hivi kwa kura zao endapo kama mkiwaboreshea maisha yao.

Upumbavu wenu ni kudhani wananchi watawaunga mkono kama mtawanunua wapinzani na kuacha kuzishughulikia changamoto zao.

Huu ni uendawazimu
 
Huyu mwanapropaganda anasahau kiti kilitakiwa kuwa cha Rowasa kutokana na ushawishi uliokuwa ndani ya chama ila kutokana na Club ccm hiyo hiyo anayoisema kwa chadema ikampa Rais Magufuli
 
Unalaumu upinzani ambao umefungwa miguu na mikono kwa kamba za chuma na mdomo umetiwa kofuli na serikali kupitia ccm? mbona huisemi ccm ambayo imejaa ushetani wa kila aina?
 
umesema vizuri. kuna succession na kuna succession plan. mleta uzi mwenyewe haelewi kuwa kuna tofauti. ameandika succession plan akaongelea succession. hata nayo kuna sehemu kaiacha na kumvaa mbowe! naomba iwe imetokea hivyo kwa bahati mbaya. namheshimu P
mfano hai. kuna tofauti kubwa ya kukaa madarakani muda mrefu kwa vova putin na angela merkel. tena ajabu merkel ni cheo hicho hicho cha kansela. putin mara rais mara waziri mkuu. merkel yuko safi. putin ni zuga tu. lakini kwa wote wawili hakuna succession achilia mbali succession plan. mchawi uchaguzi huru na wa haki. hata bila ya ukomo wa urais. ukomo wa urais nao pia ni ubaguzi. sanduku la kura liamue. hilo ndilo chaguo la watu kwa muda huo. si ajabu kuwa kinyume na katiba!
succession plan ni ya usultan na ukomunisti hasa. wanaweza kusema wanachagua kiongozi. uchaguzi bila kuchagua. mfano mzuri ni korea kaskazini. kwenye vyama vya kidemokrasia succession plan ipo lakini sio kama hiyo. chama kinataka kushinda uchaguzi ulio huru na wa haki. sio kiishie hapo bali pamoja na ushindi kizidi kunawili kama chama. ukada hautoshi. nafasi ya makada kindakindaki. wanajulikana wanatayarishwa wenye vipaji kiuongozi. hao watavusha chama ndani ya chama chenyewe na hata kitaifa na kimataifa.
kwetu ni vigumu kuelewa waziri mkuu au makamu wa rais mstaafu kutoingia hata kwenye ishirini bora ya watia nia ya urais. maelezo yake ni kilio cha mzee pinda hadharani! hakuna kabisa succession plan. hata hili suala la kutia nia watu mia kwa nafasi moja ndani ya chama ni uhuni. hatujuani? hatuheshimiani? limebatizwa jina la demokrasia! tunadharauliana na kuzalisha makundi bila sababu ya msingi.
2015 ilionyesha kukosa succession plan kwa vyama vikuu viwili. wapeperusha bendera za vyama hawakuwa wanachama wa hivyo vyama. lowassa akisema ccm oyee! magufuli akipiga pushups! ccm wakiogopa kusema chagua ccm! na wengi walichagua magufuli bila kuchagua ccm! athari zake hizo. cdm hawakushtuka lowassa kurudi ccm! ccm wanakuja juu jamaa akisema serikali ya magufuli. wanamuonea bure. alipigiwa kura yeye na sio ccm.
na sio ccm, magufuli. lini alikuwa kada? alikuwa akidhaminiwa na ccm kugombea kama cdm ilivyowadhamini lowassa na haji duni! magufuli alipata shida kujaziwa fomu za udhamini mikoa fulanifulani. hawamjui ati kichama! na hivi sasa ndio anaonyesha naye hawajui makada. anawafyekelea mbali akiwajua. anawawekea katibu mkuu wa cuf. hata hivyo ni kubalance mambo. cuf nao wana mwenyekiti wa ccm.
hii mada nzuri kwa hali ya kisiasa nchini. ilivyoandikwa sio sahihi. kichwa cha mada sicho.kavamiwa mbowe bure. uzi kama huu na sio mada ni saizi ya akina phillipo bukililo, nyamemba, 1000 digits, victorie, barbarosa, jingalao, themagufulianz, magu2016 and the like. kuletwa na pasko mayalla sio sahihi hata kidogo.
 
Utakuwa mwendawazimu, sikuhitaji maelezo.
Nilihitaji jibu.

Kwa kuwa umeona haiwezekani watu wasio mageuzi oriented kupewa dhamana kubwa katika chama chenu.

Vivyo hivyo elewa hata upande wa pili umejifunza kuanza kuheshimu hisia za wanachama wake na sio kufuata ya viongozi tu.
Nadhani una mfano mzuri wa Lowasa na Ukawa alivyoitelekeza na kwenda kupiga goti.
Kwa hiyo watu wa aina hii wateteeni ninyi wendawazimu
 
Enzi za mkoloni zilikua ni ngumu zaidi.
Kwa sasa ni busara tu inahitajika.
Busara ina maana pana.
Kuna wakati busara ya mahakama ni kumhukumu mtu kunyongwa kukingana na kesi iliyopo mbele yake.
Sijui umenielewa.
 
You suffer from psychiatric trauma.
We will be here waiting to see your fate.
 

Katika mazingira na barabara vinapotembelea vyama vya upinzani ikiwemo Non level playing field na politics of power, wanalazimika kufikiri na kutenda kimkakati zaidi kuliko chama tawala, sio swala la copy and paste au stereotyping na kufanya kwa sababu vitabu vinasema hivyo au kwa sababu wengine wanafanya hivyo is a trip to Armageddon!
When the going gets tough; the tough get going!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…