Upinzani tulizeni akili, 2025 mnachukua nchi. CCM hawana cha kutuambia zaidi ya miradi ya Magufuli

Upinzani tulizeni akili, 2025 mnachukua nchi. CCM hawana cha kutuambia zaidi ya miradi ya Magufuli

Magufuli 05

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2023
Posts
1,433
Reaction score
2,791
Nina amini kwamba
  • CCM hii imechoka
  • Imechokwa
  • CCM hii na Ile ya awamu ya nne ni baba mmoja mama mmoja.
  • kila kona ya nchi wananchi wanalalamika bidhaa kupanda bei. Hakuna mtu wa kuwatetea.
  • kiongozi mkuu ndo kabisa kachokwa ni vile nidhamu inawaongoza Watanzania. Lakini wanatamani hata kumpigia yowe kabisa.
  • CCM hii imejaa wababaishaji,waongo na wasio waadilifu kwa raslimali za nchi. Ufisadi wa kutisha kila mahala.
  • Hawana Tena Nia na mbinu ya kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi zaidi ni kila mtu ale kulingana na urefu wa kamba.
-mwamko wa mabadiliko ni mkubwa mno. Toka nianze kujitambua sijawahi kuona kiongozi mkuu wa nchi hapendwi kama huyu wa sasa.
  • upinzani kama mtaweka SILAHA chini na kutambua Nini chakufanya basi Hawa Jamaa wa kijani 2025 tunaagana nao asubuhi tu. Kuna watu wapo huko CCM wapo tayari kuondoka wanaweka mambo Yao Sawa. Tafadhali Sana wapokeeni na muunganishe nguvu. Ndo siasa ilivyo kamwe msiwabeze.
  • 2025 CCM Hawana cha kutuambia zaidi ya kuvizia miradi ya Magufuli ya SGR.bwawa la umeme na meli zinazojengwa.
Wameishiwa sera Hadi wanaita watoto wadogo kuongelea bandari kwenye majukwaa.
Watatuambia Nini na vile Hawana hata watu wenye ushawishi. Kiongozi wao hata kuongea ndo kama mnvyomuona, yeye mwenyewe anaona aibu hata kujitokeza kwasasa.
- Tulizeni akili upinzani. Huu ni muda wa kufanya research,na kuweka mkakati maridhawa.pia boresheni raslimali fedha.
-Tumechoka kuongozwa na mkoloni mweusi,tumechoka kuimbiwa mapambio ya mbio zetu toka uhuru mpaka sasa tunajivunia amani na utulivi pekee. Sasa tunataka mageuzi halisi ya kilimo,VIWANDA na matumizi sahihi ya raslimali zetu.

Najua viongozi wazuri wapo lakini wanapigwa vikumbo wasichomoze.

2025 tunataka mapinduzi ya kweli na si Hawa Jamaa wanaotuambia tuhamie Burundi.

Wananchi tumehamasika na hatupoi tayari kwa porojo na uzandiki wa kijani tena.

Mwisho kijani kwa muda mrefu sasa mmewageuza Watanzania wajinga na kuwatumia mtakavyo. Sasa mbingu imekataa, unabii unatimia. Ni muda wetu Watanzania kuwafurusha kwenye kiti cha Enzi...
 
Kama NEC wapo ....

Hata iwekwe jiwe na chadema ...NEC watatangaza jiwe ndio raisi wa Tanzania..
 
Back
Top Bottom