"JokaKuu, post: 31481348, member: 221"]
..jiwe angekuwa serious dhidi ya ufisadi asingekubali kuungana na watu kama rostam azizi,babu seya, madabida,.
Nisichokielewa ni kuwa, kuwaita mafisadi ni kwasababu ya ukata katika chama au sababu za kukwamua biashara za nchi! Sijui
Kitendo cha kukaa nao tu kimepunguza kama si kuondoa hoja ya mapambano ya ufisadi
..kinachowaponza maraisi wetu ni kofia ya uenyekiti wa ccm.
Hii ni kwasababu wanataka kuwa ''secured'' dhidi ya yaliyomkuta Mbeki. Makundi ndani ya CCM yana nguvu sana kiasi kwamba ni tishio. Hata kama hayaonekani bado yanabaki kuwa na nguvu
..hiki chama hakiwezi kujiendesha bila nguvu na rasilimali za MAFISADI.
Na ndicho kilichopora mali zilizojengwa kwa nguvu ya umma na kusema ni za CCM
Inawezakanaje chama cha miaka 50 kilicho na mtandao bado kinategemea ''bakuli''
..Utakuta Raisi anaingia na spidi ya kupambana na ufisadi lakini spidi hiyo inaishia njiani...Kila Raisi alikuja na moto wake ambao ulizimika miaka 2 au 3 wakiwa madarakani.
Ni kwasababu hakuna mwongozo. Mapambano yanabaki kuwa utashi wa mtu na si utaratibu wa kisheria.Laiti vyombo kama Polisi vingekuwa huru kazi ya kupambana na ufisadi ingekuwa rahisi sana. Kwasasa ni ngumu kwasababu vyombo vyote vinawajibika kwa Rais
Usalama, PCCB, Polisi hata watendaji kama DPP na DCI. Hapa ndipo hoja ya vyombo huru inapokuwa na nguvu dhidi ya utashi wa mtu
..Mzee Mkapa [ ripoti ya Warioba / kumshtaki Nalaila Kiula na Dr.Mlingwa]
Ilikuwa moto tu wa kudhihirisha ni Mr Clean
..Mzee Kikwete [ kumshtaki Mramba na Yona].
Hapa hakukuwepo mapambano bali visasi vya kisiasa tu. Ndio mchezo unaondelea dhidi ya CAG
..Sidhani kama Magufuli atakuwa tofauti na watangulizi wake. Dalili zimeshaanza kujionyesha
Vita dhidi ya rushwa ni kubwa na ina mawaa sana. Kuna nyakati unalazimika kumkana nduguyo ili sheria ifanye kazi
Kuanzia suala la vyeti ilikuwa ni dhahiri vita ni ya kuchagua ''cherry pick'' badala ya holistic
Hili lilisabibisha ''wapiganaji' wajiulize inakuwaje na kwanini iwe hivyo na kwanini wao wafanye