Uchaguzi 2020 Upinzani twende na Membe 2020!

Uchaguzi 2020 Upinzani twende na Membe 2020!

Ninaimani kubwa na Membe,hasa kutokana na ubobezi kwenye diplomasia ya kimataifa.Membe atatuvusha,ccm wakimkataa upinzani wampokee muhimu atusaidie kupindua meza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna Kosa Upinzani watarudia kufana Kosa kama ilivyokuwa kwa Edward Lowassa mwaka 2015 ndilo hilo la Kumpokea Mtu aliyekatwa kutoka Chama Cha Mapinduzi! Msirudie Kosa
 
Iwe mwaka 2020 au 2025 ni Membe
Iwe mvua iwe jua ni Membe
Iwe CCM iwe Upinzani ni Membe
Iwe kwa kura za kweli au za kuiba ni Membe
Iwe kwa Wafanyakazi au Wakulima ni Membe

Iwe wafanyabiashara au machinga ni Membe
Iwe kwa wanachuo au waalimu ni Membe
Iwe kwa Jeshi au Polisi ni Membe
Iwe kwa wagonjwa au wafungwa ni Membe
Iwe kwa wasanii au wanamichezo ni Membe
 
This time, no one will buy this rotten tactic

Wabatizane na kumalizana hukohuko Lumumba
 
Kwa nini tunasema upinzani usimsimamishe Bernard Membe kuwa mgombea urais 2020?

Sababu zi wazi kwa kila mtu ambaye amekuwa akifuatilia mwenendo za siasa za Tanzania kwa takribani miaka 10 iliyopita. Kwa uchache, hizi hapa chini ndizo sababu za msingi:

1) Ni mkakati ambao umekuwa tried and tested but has miserably floundered. Ushahidi ni kilichotokea kwa Edward Lowasa 2015 ambaye sasa amerejea CCM. Hii imepelekea embarrassment ya kiwango cha juu kwa upinzani.

2) Bernard Membe kujiunga na upinzani itakuwa si kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania bali kuitumikia nafsi yake ambayo inautaka urais by hooks or crooks. Hata ikitokea kimuujiza akashinda urais, kwenye timu yake atahakikisha anaweka watu wake (Nape, Riz1, etc) hata ikiwa at the expense of wapinzani watakaokuwa wamemsaidia kushinda.

3) Ukilinganisha kati ya Lowasa vs Membe utaona Lowasa alikuwa na political base kubwa na imara kumzidi Membe. Lakini bado alishindwa na baada ya kushindwa alinyong'onyea na hatimaye kurudi zizini (CCM).

4) Bernard Membe alishiriki kwa kiasi kikubwa kuhujumu Rasimu ya Katiba ya Warioba. Angekuwa ni mtu visionary, angeiunga mkono na leo hii tusingekuwa hata tunaongelea kuhusu yeye kuhitaji kugombea kupitia upinzani.

5) Bernard Membe ni CCM through and through na anakipenda sana chama chake (FACT). Kaeni mbali naye... rather, mwacheni apigane vita vyake mwenyewe dhidi ya mahasimu wake ndani ya chama chake.

This time upinzani mkikubali tu kutumika tena na hawa wasaka madaraka, then mjue tu kuwa that'll be that in the eyes of the voting wananchi (electorate).
Mnao wagombea credible wengi tu. Jipangeni from within. Undeni coalition ili mpate strong candidates. Mtarejesha imani ya wananchi.

Msijesema hatukuwaambia!

Zitto, John Mnyika
 
Hakuna cha kubadili gia angani yeye apambane na haliyake. Kama vipi afufue kile chama chenye jina kama ICJ"" Au aende kwa dovutwa ili kutimiza ndoto zake japo alisema sikuhizi haishi katika ndoto. Hayo aliyatamka kipindi fulani akihojiwa
 
Back
Top Bottom