Dhana nzima ya demokrasia ni watu kujiamulia wanavyotaka kujiongoza, na wanayemtaka awaongoze.
Haya ya kulazimisha mtu fulani tu, au chama fulani tu, ni kinyume kabisa na dhana ya demokrasia.
Hata Mwl Nyerere pale alipolazimika kugombea mwenyewe bila mpinzani, aliitisha uchaguzi huru, kisha kuweka kivuli, ili wale wasiomtaka wachague kivuli. Ni imani yangu endapo kivuli kingemzidi kura, basi angejiuzulu kuacha uwanja watu wajitokeze kumrithi.
Ni bahati mbaya sana kwa nchi kutawaliwa mithili ya mifugo badala ya binadamu waliostaarabika.