Upinzani umekosa hoja na muelekeo, badala kujadili hoja zenye mashiko ili mkubalike mnabaki kujadili takwimu zilizokosewa bahati mbaya


Uko sahihi kwa mtazamo wa nongwa dhidi ya upinzani, hasa ukiwa kwenye mazingira ya kusaka uteuzi.
 
wanaweza kuachiwa week nzima wanajadili halafu Ijumaa wanapewa press release....J3 next week wanaendelea na Ndugai... baada ya miezi miwili wanaletewa topic nyingine waijadili..

Wakati huo nyinyi huwa mnajadili nini? Maana wote huwa tuko hapa hapa kwenye mijadala hiyo hiyo. Labda mtuonyeshe nyinyi huwa mko kwenye mijadala ya Tanzania ya viwanda, wakati sisi tunajadili haya.
 
Wakati huo nyinyi huwa mnajadili nini? Maana wote huwa tuko hapa hapa kwenye mijadala hiyo hiyo. Labda mtuonyeshe nyinyi huwa mko kwenye mijadala ya Tanzania ya viwanda, wakati sisi tunajadili haya.

sisi ndio maproducer tunaamua uelekeo wa music kwa manufaa yetu...hahahaha
 
sisi ndio maproducer tunaamua uelekeo wa music kwa manufaa yetu...hahahaha

Mngekuwa na ujanja huo nchi hii isingekuwa masikini hivyo, wala msingelialia kuwa tunapinga kila kitu. Yaani mkujua kutwanga, sisi tunajua kuanua. Hakuna hoja inajadiliwa kwa mtazamo wenu ndio maana mnaishia kupata jazba.
 
Mngekuwa na ujanja huo nchi hii isingekuwa masikini hivyo, wala msingelialia kuwa tunapinga kila kitu. Yaani mkujua kutwanga, sisi tunajua kuanua. Hakuna hoja inajadiliwa kwa mtazamo wenu ndio maana mnaishia kupata jazba.

nchi kuendele ni issue ya pamoja shirikishi kwa watu wote kujituma kwa nafasi zao ili maendeleo yaje, Watawala kazi yao kutoa guideline na uelekeo ambao wengi wataufuata...

Kama wewe hujitumi, mimi sijitumi, na wengine hawajitumi na kodi hatulipi pia...unategemea maendeleo yaletwe na nani....

Kupinga pinga ni pale ambapo kuna issue ambazo zinamanufaa kwa maana ya chanya kwa jamii lakini nyie kwasababu ya kupata attention na kusikika lazima mpinge na kuleta translation zenu kuchanganya watu..

Mfano: issue ya Acacia na Barrick...Wakati Taifa linajaribu kuchukua approach fulani ili angalau kuleta changes kuna mtu anaitwa Lissu akawa anazunguka huku na kule kubwabwaja utafikiri sio mtanzania kwa hoja zake zisizoeleweka huku akitaka kusikilizwa yeye....

Kwa hali hiyo ya para ya 3 na 4 ndio maana mnakemewe, mkosoe na kuleta njia mbadala na msimame kwenye misingi yenu, mkosoe kwa staha panapopaswa kukosolewa na kuleta suluhu...kuna wakati mnapaswa kuwa kitu kimoja na watawala au Rais kwenye masuala nyeti yenye maslahi mapana ya Tanzania na qatu wake...
 
Mimi nilitoa maoni na wala sio mnazi wa chama chochote, huo ushindi mlioupata
2015 ni kwa sababu ya mgawanyiko uliotekea ccm na ushawishi binafsi wa Lowasa. Ninachoamini mpka leo Dr angekuwepo upinzani Angela mngekuwa na agenda madhubuti mnazosimamia.

Nakumbuka mzee Lowasa alisema mnapaswa kubadilika kutoka kwenye uanaharakati kwenda kuwa chama cha siasa lakin hamkumwelewa hasa nyie mashabiki wa mitandaoni.Chama making cha siasa hakifai kundandiadandia matukio kama kinapaswa kuwa na agenda ambazo zitaeleweka mpaka na mtoto mdogo.
 
Bila upinzani makini jeshi la polisi lingelala, umakini wa upinzani ndiyo unaloifanya serikali na CCM walihangaishe jeshi la polisi litumie nguvu badala ya akili kuwalinda.
 

Alichosema Lisu kwenye suala la Acacia na Barick alikuwa wazi, ila kwa sababu ilikuwa ni awamu ya kusaka sifa ndio maana ikatoka tafsiri tofauti. Huyo aliyejifanya anapambania madini, alikuwa kimya wakati Lisu anafuatilia mambo hayo. Kumbe kupambania raslimali za taifa ni mpaka uwe rais? Sisi kila kitu tunacho kuanzia njia mpaka suluhisho la hayo mambo. Mfano mrahisi ilikuwa ni elimu bure, wakati mkipinga tulisema inawezekana, Lakini baadae mkarukia tena sio kwa ubora tuliotaka sisi. Mnataka kupewa support na kila mtu ingieni madarakani kwa haki, lakini kitendo cha kuingia kwa kupora uchaguzi huo ushirikiano sahauni.
 
Fyi wanaoongoza kuongelea hiyo kasoro ni wanaCCM wa team JOBO. Asilimia kubwa ya wapinzani wako upande wa mama...


Watu wasikimbie vivuli vyao kwa kutumia mwavuli wa wapinzani
 
Tatizo la msingi huwa ni nini hasa?

ubovu, uongo au ubutu wa viongozi wao legelege wenye kuzingatia zaidi maslahi yao binafsi kwanza?

au

ni sera mbovu na mikakakati duni ya vyama vyao, isiyo tekelezeka na iliyokosa matumaini ya kuleta tija, mabadiliko na mageuzi kwa wananchi?

au kwa vile hawana uwezo wa kujitegemea, wala hawana ofisi za maana za kudumu, kwamba hata likitokea la kutokea kuna mahali pa uhakika unaweza kuwakuta?🐒
 
Ushawahi kuziona sera za wapinzani?

Hakuna wapinzani, kuna wapigaji tu.
 
Nini maana ya upinzani? au huko CCM kwa wajinga mna Definition tofauti kuhusu upinzani?
 
kwa sababu hawana dola, wakipata dola watawala wa sasa wakiwa wapinzani na wao watapata shida kurudi utawalani.
 
AU
Uzuri wa CCM, I mean, hawana natusi. Ilani zao ni credible, practical na zinatekelezwa. Hakuna sera yenyeni Muungano harufu ya Udini au Ukabila. Kikubwa zaidi ya vyote ni Muungano, hili hawalioni kabisa wenzetu.
 
AU
Uzuri wa CCM, I mean, hawana natusi. Ilani zao ni credible, practical na zinatekelezwa. Hakuna sera yenyeni Muungano harufu ya Udini au Ukabila. Kikubwa zaidi ya vyote ni Muungano, hili hawalioni kabisa wenzetu.
Mjinga mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…