KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Wapinzani wanatumia ujinga wa watu kujieneza. Wanatambua nchi hii wenye uelewa wa mambo ni wachache na hao wachache wapo kimya Kwa sababu hawataki kuonekana ni wanasiasa.
Kuhusu hili la bandari, ni uthibitisho tosha kundi la wasio na uelewa linaburuzwa na kukokotwa bila kujijua. Wanatumia mbinu za kuchochea hasira ili watu walipuke, ni kama bomu linategwa.
Hili bomu bahati mbaya litawalipukia wategaji bila kujua Muda wa saa wa kulipuka kwake. Siku ambayo watanzania wataanza kuona faida za uwekezaji bandarini ndio siku ambaye Imani Kwa upinzani itafutika kabisa mioyoni mwa wanaoumini.
Maana siku hiyo watanzania watamjua adui yao wa kweli kwenye maendeleo yao. Ni siku ambayo watamjua ni nani aliyekuwa hataki ajira zitengenezwe au ziwepo, ni siku ambayo watanzania watajua ni nani hasa mnufaika mkuu wa umasikini wa watu.
Bado hawachelewa kabla ya kujizika wenyewe kwenye kaburi la zege. Hili la uwekezaji wa bandari ni kaburi la zege Kwa upinzani, mwenye macho na atazame yaliyo mbeleni.