Upinzani wa nchi hii umelala usingizi wa Pono, waoga na wako kimaslahi zaidi

Upinzani wa nchi hii umelala usingizi wa Pono, waoga na wako kimaslahi zaidi

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
1,000
Wapendwa salaam!

Kama kuna kitu kinanisikitisha katika nchi hii ni vyama vya upinzani kulala usingizi wa wa pono. Tulidhani kua wao ndio mbadala wa pili wa serikali lakini wamekaa kimya huku mambo mengi yakienda ndivyo sivyo.

Kwahiyo baada ya kuporwa vitu vingi kwenye uchaguzi ndio kifo chako kabisa hawasikiki tena?

Kuna suala zito na gumu la KATIBA MPYA limeachwa wanasubiri kila inapokaribia wakati wa uchaguzi kuilaumu serikali wakati wakijua kua haiwezi kutenda tofauti na mfumo uliopo ndani ya katiba. Tulitegemea kua upinzani ungekua front line kuhamasisha umma wa Watanzania kuelewa maana na umuhimu wa katiba mpya.

Huwezi kuwalaumu Watanzania kua ni wajinga wakati hujawaelemisha, huwezi ukamkuta machinga na mitumba yake pale msimbazi Kariakoo umwambia tuandamane kudai katiba mpya wakati hajui itamsaidia nini yeye na atakuona wewe ni mvunjifu wa amani, mwelimishe kwanza ajue maana ya katiba na umuhimu wake katika maisha yake.

Hakuna Mtawala yeyote duniani atakayekuletea katiba mpya yenye kumpunguzia power au yenye kuleta usawa katika jamii. Atakua radhi kubadili katiba iwe na favori kwake yeye. Si wajibu wa mtawala kukuletea katiba, ni lazima alazimishwe apende au asipende maana nchi ni yetu sote si mali ya mtu na kila mmoja ana haki ya kuishi na kupata haki yake ya msingi.

Hakuna chombo chochote cha dola kinachoweza kuumiza ama kupoteza mbele ya macho ya dunia kwakua unadai haki yako ya msingi na kikatiba. Huwezi kwenda mahakamani kudai kitu ambacho pia waamuzi ndani ya mahakama watawala wamewawekea. Ni haki ya kila mtu kudai katiba mpya kwa sababu ni ya msingi na ni muhimu.
 
Kwanza ningekuona wa maana kama ungekemea ule uhuni uliofanywa kwenye uchaguzi mkuu uliopita, lakini umezungumzia kama upepo fulani ambao kwako tayari umeshapita, hapo umefeli, ule uhuni lazima ulaaniwe vikali na kila mpenda demokrasia.

Baada ya hapo ndio unataka elimu itolewe kuhusu katiba mpya, nikuulize baada ya hiyo elimu yako kutolewa (theory) unadhani itatosha kupatikana kwa katiba mpya bila elimu hiyo kuambatana na vitendo vya kuidai hiyo katiba? (refer movement ya Askofu Mwamakula)

Jibu utakalo pata hapo ndio ujue hili suala la upatikanaji wa katiba mpya chini ya utawala wa CCM inayojua fika inalindwa na dola kuendelea kutawala sio la midomoni tu, lipo practical zaidi.

Sasa naamini wewe ambae unaonesha tayari unaujua umuhimu wa katiba mpya utakuwa wa kwanza kwenye uhamasishaji kule field wa upatikanaji katiba mpya badala ya kumuachia Mwamakula peke yake kwasasa, hii theory yako hapa iwe ya mwisho, twende uwanjani.
 
Ngoja nisiwe mnafiki wakati ata katiba ya zamani siijui🚶🚶
 
Shughuli zote za siasa hapa nchini zimepigwa marufuku.unadhani Nani atathubutu kuitisha mkutano?
 
Sema watawala wa kiafrica na sio watawala wote,kule kuna viongozi watawala wanapatika uncivilized country.
Wananchi ndio wamewasaliti wapinzani.
 
Mtoa hoja inaelekea unaishi in a Lala land endelea kuishi kwenye AC na kuchimbia kichwa chako mchangani na kujifanya huoni hali halisi ya Tanzania yetu na kwa taarifa yako kuwa nchi imepigwa na covid 19 waves,amka na smell the coffee!!
 
Umuhimu wa katiba mpya huwa unaonekana ukishatoka madarakani.Thus membe,mkapa, Sumaye, Lowasa waliidai wakiwa nje baada ya mfumo kuwatupa japo waliweka pamba walipokuwa mezani.Jiwes and company ni hadi mfumo ukimtupa ndipo atajua umuhimu wa katiba mpya na demokrasia.Tumeona Nyerere amekuja kuyahubiri makosa yake baada ya mfumo kumtupa.Upo msemo mtawala wa kiafrica huwa na akili akishatoka madarakani.
 
Kamuulize askofu Mwamakula ni nini maana ya kudai katiba mpya atakuambia.
By the way hao wapinzani ni wapi wakati mkakati wenu na wenzako tangu mwanzo ulikuwa ninkuuwa upinzani? Avha ufe ili nyie muishi vizuri
 
Kama uliamua kuwaacha kama yatima ulitegemea nini sasa? Maana walihitaji ushiriki wako, wewe ulilala mbele, ulikula kona ilihali walikuwa wakipigania maslahi ya wote, ukawatenga na yule atwangaye marungu alipoona hawana nguzo ya kuegemea ikamrahiaishia kazi ya kuwawamba msalabani. "Enyi wanaume n wanawake wa nchi yangu, msiwalilie hao wapinzani bali jililieni nyinyi na watoto wenu."
 
Tuanze na wewe, umewahi au unafanya nini kusaidia hayo mabadiliko?
 
Upinzani bado upo Tanzania? Si mwenye nchi alishaufuta? Au ni upinzani gani unaongelea? Nisaidie.
 
Katiba ya mpya lengo lake ni nini?
 
Back
Top Bottom