Mkaruka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 19,932
- 34,918
Hii nchi ni ya wananchi na ndio waliolala usingizi wa pono.Wapendwa salaam!
Kama kuna kitu kinanisikitisha katika nchi hii ni vyama vya upinzani kulala usingizi wa wa pono. Tulidhani kua wao ndio mbadala wa pili wa serikali lakini wamekaa kimya huku mambo mengi yakienda ndivyo sivyo.
Kwahiyo baada ya kuporwa vitu vingi kwenye uchaguzi ndio kifo chako kabisa hawasikiki tena?
Kuna suala zito na gumu la KATIBA MPYA limeachwa wanasubiri kila inapokaribia wakati wa uchaguzi kuilaumu serikali wakati wakijua kua haiwezi kutenda tofauti na mfumo uliopo ndani ya katiba. Tulitegemea kua upinzani ungekua front line kuhamasisha umma wa Watanzania kuelewa maana na umuhimu wa katiba mpya.
Huwezi kuwalaumu Watanzania kua ni wajinga wakati hujawaelemisha, huwezi ukamkuta machinga na mitumba yake pale msimbazi Kariakoo umwambia tuandamane kudai katiba mpya wakati hajui itamsaidia nini yeye na atakuona wewe ni mvunjifu wa amani, mwelimishe kwanza ajue maana ya katiba na umuhimu wake katika maisha yake.
Hakuna Mtawala yeyote duniani atakayekuletea katiba mpya yenye kumpunguzia power au yenye kuleta usawa katika jamii. Atakua radhi kubadili katiba iwe na favori kwake yeye. Si wajibu wa mtawala kukuletea katiba, ni lazima alazimishwe apende au asipende maana nchi ni yetu sote si mali ya mtu na kila mmoja ana haki ya kuishi na kupata haki yake ya msingi.
Hakuna chombo chochote cha dola kinachoweza kuumiza ama kupoteza mbele ya macho ya dunia kwakua unadai haki yako ya msingi na kikatiba. Huwezi kwenda mahakamani kudai kitu ambacho pia waamuzi ndani ya mahakama watawala wamewawekea. Ni haki ya kila mtu kudai katiba mpya kwa sababu ni ya msingi na ni muhimu.
Sasa umekaa kama msukule ukisubiria kina Mbowe wapambane kwaajili yako wakati wewe unagonga mvinyo siyo.
Kwanza wao washafanya sehemu yao. Pili, ukiwaacha wapambane peke yao na wao siku wakipata wanakuwa CCM part two, maana hawalazimiki kukutumikia wewe Kwasababu walipambana wenyewe wakati wewe unakula gambe.
Anyway, MITANO TENA NA TENA