Upinzani wa nchi hii umelala usingizi wa Pono, waoga na wako kimaslahi zaidi

Kila mtu apambane na hali yake,yaani wapoteze hela zao kukupambania wewe? Kila mtu apambane na hali yake
 
Bila shaka unaandika ukiwa na njaa
 
Labda niulize, unapozungumza upinzani kwa maana ya viongozi wa upinzani au upinzani kwa maana ya raia wa kawaida wenye mrengo wa kipinzani?
 
Upinzani Nchi hii ndio unazidi kupamba moto na CCM ndio inazidi kuchukiwa wahisani wakibana kila kona tunapata Katiba mpya na Tume huru kwelikweli

Lissu akomae na wahisani Waache kuchangia misaada ya bajeti ili mambo yawe mswanu
 
Vipi luzuku ya wale 19 inaletwa na inapokelewa? Kama hamsemi sasa kama mnapokea, vitabu vya CAG vitatuambia!
 

Twahitaji kujiuliza:

1: Wakati wanasiasa wanajitutumua kudai hayo mabadiliko tuliwaunga mkono kiasi gani?

2: Kwani hao wanasiasa wana roho za chuma? Wanasurubiwa kwaajili yetu, nasi tumekaa kimya kama hayo hayatuhusu.

3: Elimu gani twahitaji, kama si ile aliyoitoa bythen katibu mkuu Dr. W. Slaa

4: Tujitafakari watanzania wenyewe tuna shida gani?

5: Kama hatujafikia kuona hili kama hitaji letu la msingi, basi tupige kimya mpaka kusikia kwa kenge (damu sikioni). Mdogo mdogo mpaka tuwekewe vidole machoni.

Hakuna wa kumlaumu mtu mwingine , bali tujilaumu wenyewe. Katiba si hitaji la mwanasiasa hivyo kila mmoja na atimize wajibu wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…