SHY,
Nimekusoma. Mawazo yako umeyaelekeza kwa upinzani kwamba 'they're trying to pollute the situation'. Fahamu kwamba, hali tuliyonayo kwa sasa Watanzania, imetuunganisha pamoja kupiga kelele dhidi ya mafisadi. Si mpinzani, si yule aliyepo kwenye system au si yule asiye na chama wote tu wamoja dhidi ya hao wachache.
Wakati hao unaowabeza kuwa ni wapinzani walipoibua hoja za nchi kufilisiwa na wachache pale Bungeni Dodoma, nchi nzima ilitetema, Bunge lilitetema, wafanyakazi na wakulima walishika viuno vyao kwa mshangao usio kifani. Baada ya hapo 'Sebene' lilianzia Bungeni kwa wabunge wote kuungana bila kujali vyama vyao. Huku nje nako wananchi bila kujali tofauti za itikadi za vyama vyao nao pia wakaungana kutaka kujua ukweli wa mambo. Kwa kiasi fulani ukweli huo ulionekana kwa baadhi ya watuhumiwa kuachia madaraka, kwani walioachiwa madaraka Bw. shy ni wapinzani? ila waliachia madaraka kutokana na hoja za kweli na za msingi zilizowasilishwa na Watanzania wenye uchungu na nchi yao ambao wewe suala la upinzania limetawala bichwa yako.
Ukiwa nje ya nchi, unahitaji kujua yanayotokea nyumbani. Ukitaka kujua ukweli wa mambo pata habari kutoka pande zote, hapa ni kwamba waliopo kwenye system wanakwenda nje na wanaongea na waTZ walioko huko hali kadhalika na wapinzania wanaongea nao. Kwa vile walio nje nao wanaufahamu wao wanachuja mbichi na mbivu.
Nisingependa kwenye masuala ya msingi Bw. Shy uingize ubaguzi. Ni ubaguzi huu huu ambao unaweza kudhoofisha mshikamano ambao 'automatic' umeibuka miongoni mwa wa TZ kutaka kulinda raslimali za nchi kwa faida ya nchi na vizazi vijavyo. Suala la nani mkweli na katoka chama gani hapa halina nafaisi. Tunachotaka umeambiwa na waliotangulia 'Aluta contunue -mpaka kieleweke'.