Niliwahi kuona tangazo katika mtandao wakati Fulani , mmoja wa wabunge wa upinzani Tanzania ameacha namba yake ya simu atakayotumia atakapofika marekani , kwa wale ambao hawako busy wanapenda kuonana nae na vijana wengine wengi wenye muelekeo wa kipinzani .
Sitaki kubisha inaonekana wapinzani wamewashika sana vijana wa kitanzania walio nchi za nje haswa marekani kiasi kwamba zitto anapokanyaga huko wanaona mwokozi wao kafika watu wanasongamana wanataka kumwona kupiga nae picha na vitu kama hivyo .
Pamoja na kuacha hizo namba za simu na watanzania kujitokeza kuonana nae , sera na mambo anayoongea katika mikutano hii ni zile zile , za ufisadi ambazo sasa hivi ni zilipendwa , yale yale ya epa na mambo mengine ambayo kwa hakika sio ya kujenga upinzani sio ya kujenga nchi ni ya kupasua hadhi ya nchi na watu wake nje ya mipaka yake .
Namheshimu Nyepesi na Wenzake wengi kama watanzania lakini siwezi kuheshimu na kuendelea kusikiliza watu wenye mawazo ya kuvuruga wananchi wakiwa nje ya mipaka yao huwa nashangaa kama hawana masuala mengine ya kuongea zaidi ya haya .
Hao ni chadema ndio wameshikilia Epa , Ufisadi na Usalama wa Taifa , ukirudi kwa upande wa baba zako chama cha wananchi CUF , ningekuwa mimi ni mwanachama wa CUF ningehoji kwanini hao viongozi wawili wa CUF wako pale walipo mpaka sasa hivi
Tangia upinzani umeanzishwa ni viongozi wale wale wa CUF wanaowashika masikio baadhi ya wanachama wao , ni viongozi wale wale wakorofi wako madarakani katika chama hicho mpaka sasa hivi , sijui CUF hawana viongozi wengine ni lazima wawe hawa hwaw ?
Mtihani wao wa kwanza wameshaushindwa wa kuleta maelewano huko visiwani , kwa sababu wameshashindwa jaribio hilo , sioni sababu ya kwanini wasiache nafasi hizo wazi waje watu wengine wenye utashi zaidi yao , watu wanaopenda kukaa mezani na kumaliza tofauti zao .
Niliangalia hata wakati wa maandamano ya CUF visiwani wiki iliyopita mmoja wa washairi aliposema kwamba anaweza kujilipua kama mambo yataendelea kuwa hivyo , wengine wakawaambia wenzao wasipeleka bidhaa katika kisiwa kingine wakipeleka basi wao ni halali yao .
Yote hayo yanasemwa viongozi wa CUF wamekaa katika viti wanasinzia wengine wanacheka na kufurahia kwa madaha kama vile ile ni halali yao kusema vile na hakuna chochote kile mbele yake .
Nilitegemea mmoja wa viongozi hawa au msemaji wa CUF aje mbele na kusema kile kilichosomwa na yule mshairi sio msimamo wa CUF lakini hakikutokea kitu kama hicho kwahiyo tuchukulie basi kuanzia sasa hivi na mpaka hapo viongozi wa CUF watakapoamua baadaye
Kwamba sera za CUF kuanzia sasa hivi ni KUJILIPUA , KUKATAZA BIASHARA NA UNGUJA NA KUPUNGUZA UNDUGU WAO kwa sababu hawa wengine sio wanachama wao , wao ni CCM.