Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,649
- 4,786
dah bubu leo unampatia jamaa kweli...ila nae hakomi naona leo katuamulia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona hata CCM kuna vyeti vya bandia vingi tu kuanzia wabunge mpaka mawaziri? au ilikuwa hulijui hilo?
Ni jambo zuri kuwa na viongozi wenye veyti vya kughushi?
Tatizo letu hatupati muda mwingi na mahali kwingi kutoa machungu yetu ya maisha na fikra,ndiyo maana wakati mwingine hoja nyingi humu ndani huwa zinajadiliwa kishabiki sana.
Sikubalini na mambo mengi yanayosemwa na kutendwa na CCM lakini siyo kwamba sikubalini nao kwenye kila kitu,na pia napenda nguvu ya Upinzani ikue na kukomaa nchini kwetu,lakini sikubaliani na mbinu zao nyingi ambazo naziona butu
kwa mfano wapinzani wamejikita kwenye mikutano na waandishi wa habari pale kwenye ukumbi wa maelezo Dar es salaam, bila ya kuwa na mikakati mbinu ya kuhakikisha kwamba na wao wanajenga Oganaizesheni imara kuanzia ngazi ya taifa hadi mitaani kwetu.
Ingawa wengi wetu tunashindwa kuangalia au kukubali kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya nadharia (Theory) na mkakati mbinu (Strategy) katika kujenga chama. Vyama vingi vya upinzani vimejikita katika kupambanua nadharia zao bila ya kujenga mikakati imara ya kuzitekeleza nadharia hizo
CCM ni dhaifu lakini uimara wake unatokana na yenyewe kumiliki dola la Tanzania,kuitoa CCM hakutafanikiwa kwa kusema tuu kwamba fulani ni fisadi,inatakikana mikakati ya uzamivu kubadili fikra za watu waliotawaliwa na CCM kwa zaidi ya miaka 30, siyo kupiga domo tu kila siku
Mfano halisi ni Mwalimu. Aliijenga TANU kwa kufika kwa watu akiwa anafanana nao na anaongea lugha yao,aliwajaza matumaini chanya na wao walimpa dhamira zao. Wapinzani wa sasa wananchi wanasema "hata wao tukiwapa nchi watakula kama CCM,tena heri CCM wameshaanza kuvimbiwa!
Ni jambo zuri kuwa na viongozi wenye veyti vya kughushi?
Mbona hata CCM kuna vyeti vya bandia vingi tu kuanzia wabunge mpaka mawaziri? au ilikuwa hulijui hilo?
Niliwahi kuona tangazo katika mtandao wakati Fulani , mmoja wa wabunge wa upinzani Tanzania ameacha namba yake ya simu atakayotumia atakapofika marekani , kwa wale ambao hawako busy wanapenda kuonana nae na vijana wengine wengi wenye muelekeo wa kipinzani .
Sitaki kubisha inaonekana wapinzani wamewashika sana vijana wa kitanzania walio nchi za nje haswa marekani kiasi kwamba zitto anapokanyaga huko wanaona mwokozi wao kafika watu wanasongamana wanataka kumwona kupiga nae picha na vitu kama hivyo .
Pamoja na kuacha hizo namba za simu na watanzania kujitokeza kuonana nae , sera na mambo anayoongea katika mikutano hii ni zile zile , za ufisadi ambazo sasa hivi ni zilipendwa , yale yale ya epa na mambo mengine ambayo kwa hakika sio ya kujenga upinzani sio ya kujenga nchi ni ya kupasua hadhi ya nchi na watu wake nje ya mipaka yake .
Namheshimu Nyepesi na Wenzake wengi kama watanzania lakini siwezi kuheshimu na kuendelea kusikiliza watu wenye mawazo ya kuvuruga wananchi wakiwa nje ya mipaka yao huwa nashangaa kama hawana masuala mengine ya kuongea zaidi ya haya .
Hao ni chadema ndio wameshikilia Epa , Ufisadi na Usalama wa Taifa , ukirudi kwa upande wa baba zako chama cha wananchi CUF , ningekuwa mimi ni mwanachama wa CUF ningehoji kwanini hao viongozi wawili wa CUF wako pale walipo mpaka sasa hivi
Tangia upinzani umeanzishwa ni viongozi wale wale wa CUF wanaowashika masikio baadhi ya wanachama wao , ni viongozi wale wale wakorofi wako madarakani katika chama hicho mpaka sasa hivi , sijui CUF hawana viongozi wengine ni lazima wawe hawa hwaw ?
Mtihani wao wa kwanza wameshaushindwa wa kuleta maelewano huko visiwani , kwa sababu wameshashindwa jaribio hilo , sioni sababu ya kwanini wasiache nafasi hizo wazi waje watu wengine wenye utashi zaidi yao , watu wanaopenda kukaa mezani na kumaliza tofauti zao .
Niliangalia hata wakati wa maandamano ya CUF visiwani wiki iliyopita mmoja wa washairi aliposema kwamba anaweza kujilipua kama mambo yataendelea kuwa hivyo , wengine wakawaambia wenzao wasipeleka bidhaa katika kisiwa kingine wakipeleka basi wao ni halali yao .
Yote hayo yanasemwa viongozi wa CUF wamekaa katika viti wanasinzia wengine wanacheka na kufurahia kwa madaha kama vile ile ni halali yao kusema vile na hakuna chochote kile mbele yake .
Nilitegemea mmoja wa viongozi hawa au msemaji wa CUF aje mbele na kusema kile kilichosomwa na yule mshairi sio msimamo wa CUF lakini hakikutokea kitu kama hicho kwahiyo tuchukulie basi kuanzia sasa hivi na mpaka hapo viongozi wa CUF watakapoamua baadaye
Kwamba sera za CUF kuanzia sasa hivi ni KUJILIPUA , KUKATAZA BIASHARA NA UNGUJA NA KUPUNGUZA UNDUGU WAO kwa sababu hawa wengine sio wanachama wao , wao ni CCM.
The author of this article is a victim of numb thinking..... a condition which makes brain vunarable to stupidity and ignorant .... as a result a victim always do something he/she know (or he/she should know) he/she shouldn't be doing but he/she do it anyway