Upinzani watangaza mapambano 2008

Upinzani watangaza mapambano 2008

Hakuna chama cha upinzani hata kimoja kilichokuwa tayari kuongoza nchi. Waacheni waendelee na jukumu wanaloonekana kulimudu la kuwasaidia waandishi wa habari kupata taarifa za ufisadi na mafisadi.

Vyama hivi havina hata lengo la kuisukuma serikali kuwashughulikia mafisadi, usidanganyike. Vyama hivi vina viongozi wanasiasa walioamua kutumia ufisadi kujipatia umaarufu, kitu ambacho kina manufaa.

Kumbuka Lipumba alisema nini juu ya uteuzi wa Gavana mpya wa BoT? Kama ufisadi ungekuwa unamuuma kweli moyo, asingeunga mkono msaidizi wa Gavana mwenye kashfa kubwa kupewa cheo hicho, kwa sababu ukweli ni kwamba haiwezekani Gavana akawa "fisadi" halafu msaidizi wake wa miaka mingi akawa clean!!!.
 
Upinzani hawana strong strategic planners, na kwa njia moja au nyingine nafahamu ni kwa nini. Wale wazee wa upinzani wanaimani kwamba wako entitled na kuongoza. Mfano mzee Cheyo yeye ni chairman wa chama chake no matter what will happen.

Lipumba ana imani kabisa kwamba yeye ndie strong candidate wa kuwa raisi, sasa kwa mantiki hiyo wao ndio wanao implimante all those failed plans. I believe kama hawa viongozi wangewapa kina Zitto au Mnyika au vijana wengine kuandaa strategic winning plan then 2010 tungeona mabadiliko.

Nilitegemea kwa sasa Chadema au CUF wawe teyera washachora map za majimbo tayari kuwapa strong candidates wawe wamesha establish relations na makada wa kila kijiji, muda ukifika kila mtu yuko fired up. Wanachofanya wao ni kurun sijui kampeni ya majimbo. CCM wanaweza kutusuck mpaka kwenye mifupa.
 
vyama vya upinzani bado haviko tayari kuongoza nchi. vingi kati yao vipo tayari kutoa changamoto kwenye bunge lakini havijajipanga kuongoza nchi.
inaweza kuwa hii inasababishwa na uhaba wa pesa, na hivyo kushindwa kupiga kambi katika eneo kubwa la tanzania, au pia inaweza kuwa ni kutokana na kuwa wanasiasa wetu wa vyama tawala na upinzani wanachukulia siasa kuwa ni mchezo, na hawapo serious kihivyo.
 
Vyama vya upinzani bado havijajipanga kuongoza nchi ila viko imara kwenye jukumu kubwa kuliko la kuwa kuongoza nchi, nchi hii inapitia katika kipindi cha mpito ambacho nchi zote za ujamaa zimepitia even Rusia nao wamepitia hapa ndo wakajitokeza mabilionea kama mmiliki wa chelsea na mwenzake aliyefungwa na serikali ya Rusia, hawa walitumia nafasi zao kwenye umoja wa vija wa chama cha wakomunist wakati wa mabadiliko na kununua kwa bei ndogo makampuni yaliyokuwa yanabinafsishwa, so tanzania sio ya kwanza kupitia hapa.

Vyama vya upinzani ni muhimu kabla ya kuingia ikulu kushughurikia mambo muhimu kwanza kama, marekebisho ya katiba, kutafuta haki na kuhakikisha wote walioiba mali za umma wanashitakiwa na kufilisiwa, kuweka mfumo mzuri wa mambo yote muhimu kwa nchi, haya hayawezi kuja bila kuwa bungeni hata kama wakiwa na serikali nao mwanaweza kuwa CCM nyingine kwani kutakuwa hakuna Check balance na accountability.

Haya yanayotokea ni kwa kuwa hatuna check balance na accountability, hivi utamwambia Hosea amchunguze kikwete wakati bado yupo madarakani wakati yeye ndo alimteua na hata kama atamchunguza je ataandika report ya kweli, hivi nani anaweza kuwauliza CCM kuhusu pesa za Deepgreen Finance Hosea, AG, au mwema?

So wapinzani tuwasaidie wawe wengi bungeni kwanza waachane na uraisi ili tuweze kufanya mabadiliko ya kweli kwenye nchi yetu tuachane na kuwataka waende kugombea uraisi ambao kwa mfumo tulionao sasa wa rushwa hawataweza hata siku moja kufanikiwa kkupata.

Tunaitaji akina Dr. Siraa na Zito wengi bungeni kwanza kwa ajiri ya mabadiliko ya nchi yetu.
 
Huwezi kuwa na sababu ya jumla kuwa wapinzani ni wazembe.
1.Siyo kwamba sisiem na dola yake wamelala na wataachia tu upinzani uchukue nchi wakati bado hawajatosheka kunyonya wananchi,hawa ni maadui wawili kwa hiyo kila mmoja hutumia mbinu mbalimbali hata kuwanunua hata kuwanunua wapinzani dhaifu kama akina Tambwe,Ngawaiya,Kaborou,akina Kyara wa SAU n.k.
2.Pia siasa za vyama vingi tawala Afrika zinalinda maslahi ya US na UK na hao majabari wako tayari kuona unawasujudia ili utawale,kwa hiyo ni mlolongo mrefu wa kufikia kuchukua nchi,siyo tu mkato.
3.Na pia si lazima upinzani utangaze kila kitu kwa sasa kwa kuwa Tanzania kuna siasa za maji taka(Sitta,2008).
 
Vyama vya upinzani bado havijajipanga kuongoza nchi ila viko imara kwenye jukumu kubwa kuliko la kuwa kuongoza nchi, nchi hii inapitia katika kipindi cha mpito ambacho nchi zote za ujamaa zimepitia even Rusia nao wamepitia hapa ndo wakajitokeza mabilionea kama mmiliki wa chelsea na mwenzake aliyefungwa na serikali ya Rusia, hawa walitumia nafasi zao kwenye umoja wa vija wa chama cha wakomunist wakati wa mabadiliko na kununua kwa bei ndogo makampuni yaliyokuwa yanabinafsishwa, so tanzania sio ya kwanza kupitia hapa..

Huyu Putin hakutoka katika chama cha upinzani bali alipewa ukanda na Yeltsin ni sawa na CCM kaanza Mwinyi kawauzia waarabu na kubomoa viwanda vyetu kaja Mkapa hali kadhalika UFISADI tu na sasa Kikwete hajui alifanyalo kabaki kubadilisha mawaziri.

Nchi ya Russia ni miaka 10 iliyopita ilkuwa masikini sasa angalia sasa wako wapi....Hata hawo west waliosaidia wanasikia wivu...huo ndio uzalendo ambao kila mtanzania alitegemea kutoka kwa Kikwete.

So wapinzani tuwasaidie wawe wengi bungeni kwanza waachane na uraisi ili tuweze kufanya mabadiliko ya kweli kwenye nchi yetu tuachane na kuwataka waende kugombea uraisi ambao kwa mfumo tulionao sasa wa rushwa hawataweza hata siku moja kufanikiwa kkupata.

Tunaitaji akina Dr. Siraa na Zito wengi bungeni kwanza kwa ajiri ya mabadiliko ya nchi yetu.

Haswa,lakini wao wamekazana zaidi katika mikoa waliyoshinda kama vile hawana uhakika na hivyo next uchaguzi angalau wangeenda huko bariadi kwa chenge au huko lupasa kwa Mkapa ama huko Tunduru na wakenda Makete alikotoka Balali.

Nchi hii kuna watu ni kama kipofu aliyeona mwezi...hakuna wajualo ila CCM hio ngome aliyojenga Nyerere inabidi wananchi waambiwe kuna Jua vilevile sio mwezi tu
 
Huyu Putin hakutoka katika chama cha upinzani bali alipewa ukanda na Yeltsin ni sawa na CCM kaanza Mwinyi kawauzia waarabu na kubomoa viwanda vyetu kaja Mkapa hali kadhalika UFISADI tu na sasa Kikwete hajui alifanyalo kabaki kubadilisha mawaziri.

Nchi ya Russia ni miaka 10 iliyopita ilkuwa masikini sasa angalia sasa wako wapi....Hata hawo west waliosaidia wanasikia wivu...huo ndio uzalendo ambao kila mtanzania alitegemea kutoka kwa Kikwete.

Haswa,lakini wao wamekazana zaidi katika mikoa waliyoshinda kama vile hawana uhakika na hivyo next uchaguzi angalau wangeenda huko bariadi kwa chenge au huko lupasa kwa Mkapa ama huko Tunduru na wakenda Makete alikotoka Balali.

Nchi hii kuna watu ni kama kipofu aliyeona mwezi...hakuna wajualo ila CCM hio ngome aliyojenga Nyerere inabidi wananchi waambiwe kuna Jua vilevile sio mwezi tu

Kama ccm wanaiba mabilioni ya fedha BOT na kuyatumia kwenye uchaguzi wewe unategemea nini. HUkujua kuwa Chadema wameshinda hadi vijijini kule Tarime?
 
Upinzani hawana strong strategic planners, na kwa njia moja au nyingine nafahamu ni kwa nini. Wale wazee wa upinzani wanaimani kwamba wako entitled na kuongoza. Mfano mzee Cheyo yeye ni chairman wa chama chake no matter what will happen.

Lipumba ana imani kabisa kwamba yeye ndie strong candidate wa kuwa raisi, sasa kwa mantiki hiyo wao ndio wanao implimante all those failed plans. I believe kama hawa viongozi wangewapa kina Zitto au Mnyika au vijana wengine kuandaa strategic winning plan then 2010 tungeona mabadiliko.

Nilitegemea kwa sasa Chadema au CUF wawe teyera washachora map za majimbo tayari kuwapa strong candidates wawe wamesha establish relations na makada wa kila kijiji, muda ukifika kila mtu yuko fired up. Wanachofanya wao ni kurun sijui kampeni ya majimbo. CCM wanaweza kutusuck mpaka kwenye mifupa.

Kwa mtu yeyote anaye walaumu wapinzani aje agombee aende vijijii halafu aone. Hivi mnasikia wakati wa uchaguzi tu ni bilioni 133 zilichukuliwa na mafisadi zikaingia kwenye uchaguzi jamani mnategemea muujiza gani?

Kinachotumaliza siyo wapinzani ni kuweza kuziba mianya ambayo watanzania watakuwa huru kumchagua kiongozi wanayemtaka basi tu.
 
Kweli kabisa mkuu,

Ufisadi umeshinda hata vijijini na hiyo inajulikana hapa. Tatizo ni hilo kuwa wao wapinzani wanashindana na dola (mabomu dhidi ya CUF) kama ilivyotokea Kiteto karibuni, na pia wanashindana na wezi wanaotumia hazina ya watanzania wote kuendeshea uchaguzi.

Hiki ni kitu muhimu sana ambacho mwanatanu anakiacha kwa makusudi kabisa kwenye analysis yake.
 
Kama ndiyo hivyo basi labda jeshi lichukue nchi ili lituepushe na ufisadi mkubwa unaofanywa na chama cha mafisadi, majeshi nayo tunayajua huwa hayana sifa nzuri yanapochukuwa nchi. Vinginevyo nchi yetu ndiyo inaharibika na hatimaye ujangili utaongezeka kwa kasi sana na hakuna wa kulaumiwa bali ni mafisadi wote wa awamu ya tatu na ya nne akiwa fisadi Mkapa.

Pamoja na hayo bado hili la kuungana ambalo limezungumzwa na Watanzania wengi liko ndani ya uwezo wa viongozi wa vyama vya upinzani ili kujenga chama chenye nguvu. Kama viongozi wa wapinzani wakionyesha nia ya kweli ya kuweka ubinafsi pembeni na kuunda chama kimoja chenye nguvu kwa maslahi ya Watanzani na Tanzania basi hata chama cha madfisadi kiwe na trilioni katika mkoba wake wa ufisadi Watanzania watakula pilau zao na kuchukua takrima na kisha kutowapigia kura. Jamani hili la kuungana lina umuhimu mkubwa na lifanywe kabla ya uchaguzi wa 2010. Zitto, Kitilya, Myika mko wapi mchangie mawazo yenu kuhusu uwezekano wa kuunda chama kimaja chenye nguvu? Kumbukeni umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
 
Kweli kabisa mkuu,

Ufisadi umeshinda hata vijijini na hiyo inajulikana hapa. Tatizo ni hilo kuwa wao wapinzani wanashindana na dola (mabomu dhidi ya CUF) kama ilivyotokea Kiteto karibuni, na pia wanashindana na wezi wanaotumia hazina ya watanzania wote kuendeshea uchaguzi.

Hiki ni kitu muhimu sana ambacho mwanatanu anakiacha kwa makusudi kabisa kwenye analysis yake.

Mbona ghafla tu umenyanyua mikono?...swala muhimu sasa ni Je tunafanya nini ili tuweze kuondoa ufisadi.

Angalia, hoja nyingi tunazotoa humu JF hata magazetini ni kuikosoa serikali,ndio ni wajibu wetu na ni swala ambalo wote tunaelewa lakini hatutoi maoni au silaha za kuweza kupambana na hili NGULI.

Kinachohitajika sasa hivi ni mbinu sio malalamiko ambayo yanagonga ukuta kila mara.
 
Kama ccm wanaiba mabilioni ya fedha BOT na kuyatumia kwenye uchaguzi wewe unategemea nini. HUkujua kuwa Chadema wameshinda hadi vijijini kule Tarime?

Ukraine chama tawala wakti wa uchaguzi walifanya hivyo hivyo lakini walikuja shindwa.Hakuna haja ya kukubali kushindwa ni kuendeleza mapambano......where is roman empire? or british empire?.
 
"Ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country." JFK

Mwananchi anapokaa chini na kulaumu kuwa Wapinzani ni wazembe, mimi binafsi napata shida sana kumwelewa.

Kwa nini?

Kwa sababu wazembe si wapinzani bali ni wananchi wenyewe kwa jumla. Vyama vya siasa kazi yake kubwa sana ni kuwapatia wananchi platform ya kisiasa waitumie kama nguvu ya umma ili kuiletea nchi yao mwelekeo wanaokusudia.

So far in Tanzania, wananchi wengi sana wameamua kujinufaisha wenyewe binafsi badala ya kuinufaisha nchi yao kupitia CCM. "Mwenye kilanga, haliliwi."

Siku wananchi, watakapochoshwa na CCM kikweli kweli. Watawaunga mkono Wapinzani na kuubadilisha mustakabali wa nchi yao.

Unaposema viongozi wazunguke nchi nzima, una maana wazunguke kwa miguu au kwa helikopta? Gharama hii yao italipwa na nani, kama sio wewe uliyekaa kando na kuagiza tu?

Unawalaumu viongozi, unataka wamuongoze nani, kama sio wewe uliyekaa kando na kuangalia tu? unapomchagua kiongozi, umeshajiuliza unamchagua akuongozee wapi?

Usikae kando na kukiangalia kijito. "Usipoutia mguu wako majini, hutavuka mpaka kufa."

"Play your part, it can be done." JKN. Usikae kando na kulaumu tu. Hakuna uzembe kama huo! Wazembe ni sisi wananchi wenyewe wala sio viongozi wa upinzania.
 
"Ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country." JFK

Mwananchi anapokaa chini na kulaumu kuwa Wapinzani ni wazembe, mimi binafsi napata shida sana kumwelewa..

Sehemu ipi ambao hujaelewa?

"Kwa sababu wazembe si wapinzani bali ni wananchi wenyewe kwa jumla. Vyama vya siasa kazi yake kubwa sana ni kuwapatia wananchi platform ya kisiasa waitumie kama nguvu ya umma ili kuiletea nchi yao mwelekeo wanaokusudia.

So far in Tanzania, wananchi wengi sana wameamua kujinufaisha wenyewe binafsi badala ya kuinufaisha nchi yao kupitia CCM. "Mwenye kilanga, haliliwi."

Siku wananchi, watakapochoshwa na CCM kikweli kweli. Watawaunga mkono Wapinzani na kuubadilisha mustakabali wa nchi yao.

Huo ndio uzembe naozungumzia.....wangoje mpaka lini?

"Unaposema viongozi wazunguke nchi nzima, una maana wazunguke kwa miguu au kwa helikopta? Gharama hii yao italipwa na nani, kama sio wewe uliyekaa kando na kuagiza tu?.

Labda hujaelewa hoja yangu,sioni kama kuna haja ya viongozi wa upinzani kuzunguka nchi nzima...ninavyoelewa kuwa vyama vina wawakilishi wao huko vijijini na hao kazi yao kubwa ni inabidi kujitangaza na kuwaelewesha wananchi ukiumwa na kichwa si lazima ule aspirin(CCM) bali unaweza kunywa maji mengi (UPINZANI)tu na ukapona
 
Kinachohitajika sasa hivi ni mbinu sio malalamiko ambayo yanagonga ukuta kila mara.

unaambiwa usimuamshe aliyelala, otherwise utalala weye- nafikiri kama wataelewa hilo watu basi nadhani wataanza kuamka !
 
Wapinzani wasafishiwa njia

na Sauli Giliard
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

BAADA ya vuta nikuvute ya miaka kadhaa, hatimaye serikali imeridhia kuandaa Muswada wa Sheria ya Vyama vya Siasa ya Mwaka 2008, ambao pamoja na mambo mengine, utatoa ruhusa ya kisheria kwa vyama kuungana na kusimamisha mgombea mmoja wa urais, ubunge na udiwani.

Uamuzi huo ambao sasa utawezesha muswada huo kusomwa kwa mara ya kwanza katika mkutano huu wa Bunge la Bajeti kabla ya kuwasilishwa rasmi Novemba mwaka huu, umetangazwa katika gazeti la serikali la Julai 18, mwaka huu.

Kwa sababu hiyo basi, iwapo wabunge watapitisha muswada huo na kuwa sheria, vyama vya siasa vitakuwa na uwezo wa kuungana na kuunda chama kimoja cha siasa, sambamba na kuwa na uwezo wa kusimamisha mgombea mmoja kama ilivyo katika nchi nyingine duniani zinazotumia mfumo wa vyama vingi.

‘‘Muswada unatoa mapendekezo ya kutunga sheria ya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa kwa lengo la kuondoa kasoro zinazojitokeza katika utekelezaji wa sheria. Madhumuni ya kuondoa kasoro hizo ni kudumisha demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini,” unasomeka muswada huo wa sheria.

Muswada huo unakuja wakati kuna jitihada za vyama vya siasa vya upinzani kujaribu kuungana au kuunda ushirikiano rasmi, vikianzia na ule waliopata kuuita NOF na baadaye Umoja wa Demokrasia Tanzania (Udeta) miaka ya 1990 kukwama na kufa. Aidha, muswada huo wa sheria unakuja wakati huu, vyama vinne vya upinzani vilivyounda ushirikiano usio rasmi vya CHADEMA, NCCR-Mageuzi, TLP na CUF vikijaribu kutibu majeraha ya kunyosheana vidole na kuhitilafiana katika siku za hivi karibuni.

Kwa upande mwingine, muswada huo ukipitishwa kuwa sheria, basi lawama ambazo serikali imekuwa ikiandamwa nazo kuwa imekuwa chanzo cha kuzorotesha na kukwamisha kukua kwa demokrasia ya vyama vingi zitapungua kama si kumalizika kabisa.

Mwaka jana Rais Jakaya Kikwete wakati akihojiwa na jarida maarufu la New African, alilazimika kujitetea akipinga tuhuma dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kwamba vimekuwa chanzo na kiini cha kuzorota kwa vyama vya siasa nchini.

“Kwa kweli tunauhitaji upinzani. Mimi siwezi kuujenga upinzani, ingawa siwezi kuchukua hatua za kuunyonga. Tuko makini katika kuhakikisha kuwa wanastawi, na tunawapa fursa na uhuru wa kukua. Hilo ndilo jambo pekee tunaloweza kulifanya. Kinachobaki ni jukumu lao,” alisema Kikwete wakati akijibu swali la mhariri wa The New African, Baffour Ankomah, wakati wa mahojiano hayo mwaka jana.

Majibu hayo ya Kikwete yanaweza yakawa na maana kubwa leo hii kutokana na uamuzi huo wa serikali kuandaa muswada huo ambao pamoja na mambo mengine utaipa mamlaka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya maamuzi makubwa pasipo kupata ridhaa ya waziri mwenye dhamana ya vyama vya siasa kama ilivyo sasa.

‘‘Marekebisho yanayopendekezwa yanakusudiwa kumpa uwezo msajili wa vyama vya siasa kusajili viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa katika daftari maalumu na pia kufanya usajili mpya endapo vyama vitakuwa vimeungana na kuwa chama kimoja,” inasomeka sehemu moja ya gazeti hilo la serikali.

Juu ya kuungana kwa vyama vya siasa, muswada huo unasema kutakuwa na viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa kama ilivyopendekezwa katika vifungu vya 7 na 9, ambao watatakiwa kuomba usajili kwa msajili wa vyama vya siasa, ambaye ndiye atahusika na masuala yote ya vyama.

Muswada ambao umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge), umegawanyika katika sehemu kuu mbili, ambapo sehemu ya kwanza inahusu jina la sheria itakayoundwa wakati sehemu ya pili inahusika na mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa.

“Muswada huo utatoa mapendekezo ya kutunga Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa kwa lengo la kuondoa kasoro zinazojitokeza, madhumuni ya kuondoa kasoro hizo yanakusudia kudumisha sheria ya vyama vingi vya siasa,” inasomeka sehemu ya muswada huo.

Pia imeelezwa kuwa muswada huo, una lengo la kupunguza na kudhibiti maadili na vitendo vitakavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani.

Katika hilo, muswada huo unapendekeza kufutwa kwa usajili wa chama cha siasa ambacho kitaonekana kujihusisha na mambo yanayotishia uvunjifu wa amani.

“…Inapendekezwa kuzuia na kukataza chama cha siasa ambacho kitakachoruhusu wanachama wake kutoa lugha ya matusi ya udhalilishaji dhidi ya chama kingine,” unasomeka muswada huo katika sehemu moja.

Muswada huo pia umekusudiwa kuwabana wanachama kuwa na uanachama katika vyama viwili ama zaidi, huku viongozi katika vyama vya siasa, wakitakiwa kuwa na vigezo kama vya mtu anayetakiwa kuwa mbunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, Ibara ya 67.

Pia inapendekezwa kuwepo kwa baraza la vyama vya siasa litakalokuwa chini ya uenyekiti wa msajili wa vyama vya siasa, wakati wajumbe wake watatoka miongoni mwa vyama vilivyosajiliwa.
 
Last edited by a moderator:
Duh,safi lakini kusije kuwa na mazingaombwe ya kuuchelewesha huu mswada.Itakua vyema kama utaharakishwa ili vyama hivyo viungane hata election zijazo za local governments
 
Rejea maagizo yangu kwa Vyama vya Upinzani katika Thread ya "Instructions to Opposition Parties".

There are more to come.

Dont ask me where I do get the information, I am an Alien. Just follow my good instructions.
 
Wapinzani wakiamua kuegemea katika sheria hii watakuwa wanajichimbia kaburi wenyewe. Wasije wakadanganyika kuwa nguvu ai zitatokana na kuungana. Kwani CCM wanapata nguvu kutokana na kuungana nani?
Muungano wao utakuwa ni Muungano wa wanyinge na kwa mfumo wa siasa za upinzani ambao tumeushuhudia tangu kurejeshwa kwa mfumo huo nchini, bado wataendelea kuwa wanyonge chini ya mfumo huo mpya wa muungano.
Wajenge vyama na vikiimarika na kukubalika kutokana na yale iliyoyafanya, hata aihitaji kuungana na yeyote ili wananchi wakukubali.
Hiyo sheria, kimsingi na nionavyo mimi, itafacilitate katika mazingira kama tutaondokana na mfumo wa winner takes all kwenye uchaguzi. Sheria kama hizi zina-save pale ambapo chama kinkaribia kufikisha kiwango cha ushindi kinachotakiwa kisheria, kinapewa nafasi ya kuungana na underdog ili kupata kiwango cha ushindi iinachotakiwa ili kuunda serikali.
 
Hakika ni lazima sasa tuwe na mtizamo mwingine kabisa, nilisema hawa wapinzani wenza wa CHADEMA wanataka umaarufu, watu wakasema haaaa .... mwana wa mwita mnafiki,nimegundua kichapo ndiyo dawa yao. haiwezekani Dr.MVUNGI ahusishe kifo cha marehemu Wangwe na Mgogoro wa Mwenyekiti Mbowe, TUNAKATAA, TENA TUNAKATAAA.......

31/08/008, ilikuwa ni mkutano wa wanaNCCR mageuzi hapa nyumbani Tarime, Dr akaendelea kuhutubia bila kujua tumemtega na ndipo alipojikuta matatani, nasema uwanja huu ulikuwa mdogo na naomba ajue kuwa sisi wana Tarime si Malaya.

TaMko letu, kwa kuwa mwanzoni wapinzani walikuwa wamoja na bado umoja wao tunauthamini sana, bado hatujajua kama ile ndoa yao wametarakiana na hivyo tuna sema tutawaelewa kama watakuwa wamoja na si vinginevyo.

Sasa tunamngejea Lipumba na MIWANI YAKE ILE, HAKIKA MTACHEKA SANA MWAKA HUU,

Tunasema hata hawa CCM kazi wanaijua kazi kwao.
 
Back
Top Bottom