Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Ilani ya Uchaguzi au kwa kiingereza huitwa Election Manifesto ni kabrasha litolewalo na chama cha siasa ambalo limesheeni mawazo na sera zote.
Mara nyingi chama cha siasa kikishinda uchaguzi huweza kupimwa mafanikio yake kutokana na utekelezwaji wa ilani yake ya uchaguzi.
Kwa miaka mitano ilopita haitii shaka yoyote kwamba CCM imesimamia ilani yake ya uchaguzi na kuhakikisha inatekelezwa kwa asilimia 80 au zaidi.
Sasa bila kuoindapinda kona CHADEMA na vyama vingine vya upinzani wanatakiwa watoe ilani zao za uchaguzi kila mmoja kwa wakati wake.
Ilani ya uchaguzi huandaliwa na kundi la watu ambao wote hukaa pamoja na kwa lengo moja kushinda uchaguzi na kushika dola.
Dalili zote kwamba upinzani unaenda kwenye uchaguzi kupoteza viti vingi bungeni zajionyesha.
Ni makosa yaleyale ya miaka nenda rudi tangu sheria ya vyama vingi ipitishwe mwaka 1992.
Mpaka sasa Agustino Mrema ndie kiongozi pekee wa upinzani ambae alitoa ilani ya uchaguzi ya NCCR mageuzi na akatoa upinzani wa kutosha kwa mgombea wa CCM mwaka 1995 marehemu Benjamin Mkapa.
Sasa basi, mwaka huu hali si kama ile ya 1995 hali ni ngumu na ni vigumu kuishinda CCM, tusiwe wanafiki.
Ila bado CHADEMA ya Tundu Lissu na vyama vingine toeni ilani zenu za uchaguzi ili wananchi angalau waone mmejitahidi.
Hata kama ni mdahalo mnaouhitaji lakini kwenye mdahalo mtakinzana kwenye ilani zenu za uchaguzi na si shutuma za yule kafanza nini ama yule vipi.
Ndo maana ni vigumu kwa Tanzania kufanya midahalo kama hakuna sera kila upande.
Acheni porojo na blahbla za oh! mara jogoo kanunuliwa na kadhalika.
Karibu.